Stories by Uncle Fafi on Medium
Captain Gardner G Habash
Zimekuwa ni siku 4 ngumu sana kwa kila mwanafamilia wa Clouds Media, kuanzia wafanyakazi hadi wasikilizaji. Kila mmoja kwa namna yake ameguswa na msiba wa Gardner G Habash aliejulikana kwa jina lake maarufu la “Captain” kutokana na kuwa nahodha wa kipindi cha Jahazi alichokiasisi.
Nimefanya kazi na Gardner ilikuwa inaelekea miaka mitano, yeye kama Brand Manager “BM” wa kipindi cha Jahazi na mimi nikiwa Mkuu wa Idara ya Digital. Katika kipindi chote hicho sikumbuki kuwahi kukwaruzana nae, kitu ambacho ni mara chache sana kutotokea kutokana na ushindani wa ndani uliopo baina ya vipindi vya redio ambavyo vyote vinaitegemea idara ya Digital kupeleka maudhui yake mtandaoni, hivyo ni kawaida mara nyingine kupokea malalamiko toka kwa BM pale inapotokea mkwamo wa aina yoyote.
Nakumbuka mara ya kwanza kumtafuta kushauriana nae kuhusu utendaji kazi ilikuwa ni baada ya kipindi cha Jahazi kutoka kwenye safari ya kazi ya mteja iliyochukua karibu wiki nzima. Kwa kawaida vipindi vinapotoka nje ya ofisi kunakuwa na watangazaji, mtayarishaji vipindi (producer), na watu watatu toka idara ya Digital (visual production na msambaza maudhui). Wakati kipindi kinaendelea kufanyika kule kuna baadhi ya malalamiko niliyapokea toka kwa mtu mmojawapo upande wa team ya radio (sio Captain) kuhusu utendaji kazi wa Digital. Kwa kawaida ikitokea malalamiko unawasiliana na team kujua changamoto ni nini na kushauriana na cha kufanya. Waliporejea Dar siku iliyofuata nilimtafuta, nikamueleza kuhusu malalamiko niliyopokea na kumuuliza kama kuna kingine chochote ili tuweze kurekebisha kwa kazi nyingine za nje zitakazojitokeza. Jibu lake lilinishangaza, na sikutegemea. Aliniambia “Hakukuwa na tatizo lolote lililosababishwa na team, changamoto ilikuwa ni mazingira ya kazi, tulikuwa eneo ambalo internet ilikuwa tatizo na umeme tulikuwa tunaupata baada ya kurudi hotelini, tunapokuwa nje ya ofisi wote tunakuwa team Clouds kwa hiyo hata huyo aliekulalamikia nitamshauri tujifunze kutafuta solution next time tukiwa field”. Mwisho akawapongeza vijana kwa kujituma kwenye mazingira magumu.
Hili lilikuwa somo langu la kwanza kujifunza toka kwa Captain, hekima ya uongozi na kutafuta suluhisho linapotokea tatizo linalosababisha mambo kwenda nje ya matarajio.
Niliendelea kuona namna anavyowachukulia kwa usawa watu wote walio kwenye team yake, hadi anaondoka Anderson Dickson (Content Manager), Ally Mapichapicha na Octagraphy (Videographers) ambao wanasimamia Jahazi upande wa Digital walikuwa kama sehemu ya familia yake. Ilishakuwa kawaida kwa watoto wa Octa kwenda kucheza na mjukuu wa Gardner siku ambayo Karen anampeleka akamuone babu yake, Anderson Dickson ni kama alishamu-adopt kama mtoto wake wa kiume kwa namna alivyokuwa amemuweka karibu na kumshauri mambo mbalimbali ya kazi na maisha.
Unahodha wa Captain haukuishia kwenye kipindi cha Jahazi pekee, hata nje ya ofisi aliendelea kuhakikisha team yote ya Jahazi inaendelea kuwa na bond. Alijenga utamaduni wa kuchoma nyama nyumbani kwake wikiendi mojawapo kila mwezi na kuikaribisha team nzima ya Jahazi kuanzia watangazaji, producer hadi team ya Digital inayosimamisha maudhui ya kipindi. Kwake hii ilikuwa kama sehemu ya kuhakikisha familia ya Jahazi inakuwa na ukaribu, na aliitumia kama sehemu ya kuwakutanisha na marafiki zake wengine aliowakaribisha ambao asilimia kubwa ni wako kwenye nafasi nzuri kwenye makampuni, biashara au taasisi. Kupitia mikusanyiko hii vijana wameweza kupata michongo ya kuwaongezea kipato cha ziada.
Niliendelea kujifunza mengi kwa Gardner, nakumbuka siku moja kulikuwa na tafrija inafanyika parking ya ofisini siku ya Ijumaa usiku. Ikatokea wakati napita sehemu aliyokuwa amekaa akaniita na kunipa gentleman hug na kuanza kunipigisha stori, asilimia kubwa ilikuwa ni kunieleza namna anavyopenda ufanyaji kazi wa vijana wa idara yangu na nidhamu waliyo nayo. Wakati namshukuru na kumwambia ni kwa sababu wanajielewa na wanaipenda kazi yao akanikatisha na kuniambia ili timu ifanye vizuri ni lazima iwe na kiongozi mzuri, kwa hiyo ameniita kunipa maua yangu. Akaniambia kitu ambacho kilibadili mindset yangu kwa 100%, nakumbuka alisema “Unapofanya kazi kwenye taasisi kama Clouds ambayo kazi yake ni ubunifu na kutengeneza personalities wewe kama kiongozi kaa nyuma acha vijana wako wang’ae, wasaidie pale wanapokwama na watetee pale unapoona kuna tatizo ikiwemo kukubali kubeba lawama zao; wakiona hivyo watakuheshimu na kukupigania kuhakikisha haufeli”. Ni maneno niliyoyachukua na kuyaweka moyoni, ukizingatia ule msemo kuwa hakuna mtu anaeongea ukweli na uwazi kama yule ambaye tayari ametupia glasi kadhaa za vinywaji vyenye asilimia.
Ni baada ya kufariki ndio stori nyingi za namna alivyoweza kuyagusa maisha ya mtu mmoja mmoja ndani na nje ya Clouds zimejulikana. Ni rahisi kwa mtu kuhoji kwa nini haya hayakusemwa wakati Captain akiwa hai, ila kama kuna kitu Captain alikuwa hapendi ilikuwa ni kujionyesha baada ya kumsaidia mtu iwe ni kwa kumpa connection ya mchongo au kumpa msaada mwenye uhitaji.
Namaliza kwa kunukuu kile alichokisema kwenye interview aliyofanya na Suzette McKenzie na kuulizwa kwa nini pamoja na umaarufu wake lakini ameendelea kuwa humble. Alijibu, “Duniani hapa kila mtu kila alichonacho kinatokana na watu, kwa hiyo usipoheshimu wale watu usiponyenyekea wale watu hata huyo Mungu mwenyewe aliekupa wale watu wakupe kile ulichonacho atakunyang’anya”.
Uncle Fafi on Twitter: ""Duniani hapa kila mtu kila alichonacho kinatokana na watu, kwa hiyo usipoheshimu wale watu usiponyenyekea wale watu hata huyo Mungu mwenyewe aliekupa wale watu wakupe kile ulichonacho atakunyang'anya" - Gardner G Habash pic.twitter.com/8Lp29JYMBu / Twitter"
"Duniani hapa kila mtu kila alichonacho kinatokana na watu, kwa hiyo usipoheshimu wale watu usiponyenyekea wale watu hata huyo Mungu mwenyewe aliekupa wale watu wakupe kile ulichonacho atakunyang'anya" - Gardner G Habash pic.twitter.com/8Lp29JYMBu
Kwa heri Captain Gardner G Habash. Pengine hatutaweza kuwa manahodha bora kukufikia wewe lakini tutajitahidi kuyaishi yale tuliyojifunza kwako na kuyagawa kwa kizazi kijacho. Tuko tayari kung’oa nanga ya Jahazi liendelee kuwasafirisha Watanzania katika safari ya kufungua dunia wawe kila wanachotaka.
Shafiq.
Naanza kuiandika hii nikiwa safarini nikirejea Dar ikiwa ni baada ya siku mbili Iringa, moja ya mikoa ambayo ningekuwa na mchongo wa uhakika wa kuniweka huko wala nisingewaza mara mbili kuihama Dar.
Kutokana na wingi wa abiria wanaotoka kwenye graduation za ndugu zao kwenye vyuo vikuu vya Mkwawa na Ruaha nilijikuta napata siti za mwisho mwisho kabisa kwenye bus la ABC Upper Class, na mbaya zaidi haikuwa ya dirishani ikimaanisha view ya Kitonga na Mikumi ambayo kwa sasa ni full green nimeikosa. Jirani yangu nimekaa na mshua ambaye njia nzima anaongea na simu kwa lugha ambayo nadhani kama sio kihehe basi ni kibena, inaonekana kuna mgonjwa anaenda kumuona Dar kutokana na kuokota maneno ya hapa na pale kwenye mazungumzo yake na watu wa upande wa pili.
Playlist ya Bongoflava iliyokuwa ikipigwa kwenye screen za bus haikunipa mzuka, sababu niliikariri siku mbili zilizopita wakati niko safarini kitu nilichoamua kufanya ni kuvaa headphone na kuweka music kwenye full blast ili kuua sauti ya mshua pembeni yangu na kelele za spika za bus.
Wakati safari inaendelea macho yangu yakahama kuangalia siti ya mbele yangu upande wa kushoto ambao ni pembeni yangu nikawaona abiria wengine wawili ambao inaonekana ni couple wakiwa na mtoto mdogo mwenye umri wa miaka kama minne au mitano hivi. Muda wote dogo yuko busy na simu ya mmoja ya wazazi, kwa makisio ya haraka haraka inaonekana anacheza game kutokana na excitement yake. Muda huo tulikuwa tunashuka Kitonga na kama kawaida ya hilo eneo mtu anaetokea Iringa view ya bonde inakuwa kushoto kwakwe. Mdada anaonekana kuwa na uoga kwamba huenda bus likatumbukia bondeni kutokana na anavyoweka mikono usoni kila dereva akilipita lori au tukipishana na mabus mengine, mchizi yeye macho yake yako nje inaonekana anaipenda view kama mimi.
Baada ya muda usingizi ukanichukua, nakuja kushtuka tuko ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, kwa kuangalia fasta kwenye dirisha la mshua naona tunapita kundi la swala na pundamilia wengi. Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kijani imekubali Mikumi, baadhi ya maeneo yana mabwawa ya muda na ninaona wanyama wanakunywa maji, sehemu nyingine tunapita kundi la nyani ambao wamejazana pembeni ya barabara wakitegemea kurushiwa vyakula na abiria. Ni kitu kilichozuiwa kwa sababu kabla ya hapo niliona bango la DO NOT FEED THE ANIMALS.
Siti ya pembeni dogo anaonekana bado yuko na simu hana habari na kinachoendelea ingawa wazazi wake wote macho yako nje wakifurahia wanyama tunaowapita, ghafla tunalipita kundi la twiga na mdada anaonekana kufurahia zaidi.
Macho yangu yakarudi tena kwa dogo, nikaanza kuwaza namna gani anavyopitwa na moment ambazo wazazi wake wanaonekana kufurahia. Nikafikiria watoto wa mikoa ambayo iko mbali na hifadhi, wanyama wanaishia kuwaona kwenye TV. Akili yangu ikarudi mpaka wakati niko darasa la nne, ikiwa ni safari yangu ya kwanza kutoka nje ya kanda ya ziwa nikiwa na Bimkubwa.
Ilikuwa ni likizo ya December na binamu yangu alikuwa akipata ubarikio au kipaimara Arusha. Mama yangu mkubwa alisisitiza kuwa lazima niwepo kwa hiyo Bimkubwa akakubali kunipeleka.
Tulikata tiketi kwenye bus la Mwanza — Arusha linalopita ndani ya hifadhi ya Serengeti, nakumbuka namna nilivyokuwa excited kwenda Arusha sidhani kama nilisinzia usiku ule wa kuamkia siku ya kusafiri. Safari ilianza saa kumi na mbili alfajiri, Bimkubwa aliniacha nikae siti ya dirishani. Sikumbuki nililala kwa muda gani lakini niliposhtuka bus lilikuwa linavuka geti la kuingia Serengeti. Kilichofuatia baada ya hapo hakijawahi kufutika kichwani kwangu.
Njiani tulikuwa tunapishana na magari mengi yaliyokua yamebeba watalii, ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona wazungu wengi namna ile, baadhi wakiwa wamening’inia juu ya magari ya tour operators wakipiga picha au kutumia binoculars. Kadri tulivyozidi kuingia ndani ya Serengeti ndio idadi ya wanyama ilivyozidi kuongezeka, ilikuwa mara ya kwanza kuwaona nyumbu kwa wingi namna ile, uzuri wa pundamilia uliniacha nikijiuliza kama yule aliewachora kwenye kitabu cha cartoon nilichosoma alikuwa amewahi kuwaona. Kuna sehemu tulikuwa tunapita makundi ya nyati wakiwa kama sita au saba, tukavuka daraja moja nikashuhudia kundi la viboko wakiwa wanaogelea. Mbele zaidi tukaanza kuwaona Twiga na shingo zao ndefu wakila majani ya kwenye matawi ya juu kabisa ya miti.
Muda wote huo Bimkubwa alikuwa akinijibu maswali yote niliyokuwa namuuliza kwa excitement; “Mama ona twiga, mama yule ni nyani au tumbili, mama wazungu hawaogopi kuliwa na simba?, mama kwa nini nyumbu na pundamilia wako pamoja lakini swala wamejitenga?”. Kuna sehemu na yeye alikuwa ananionyesha baadhi ya wanyama hasa waliokuwa mbali kama tembo na kundi la simba. Abiria wa pembeni yetu nadhani walikuwa wanafurahia show yangu maana nakumbuka nilivyokuwa sijui kuongea kwa sauti ya chini. Bimkubwa nae alifanya kazi nzuri ya kuwa tour guide siku ile.
Hadi tunaimaliza Serengeti kichwa changu kilikuwa na information overload, nilianza kutamani turudi nyumbani nikawasimulie marafiki zangu kitu nilichokiona. Cousin yangu mpaka leo ananikumbusha jinsi nilivyomueleza adventure yangu ya Serengeti, kwake hakikuwa kitu kigeni kwa sababu advantage waliyonayo wanafunzi mikoa ya Kaskazini ni school tour za kwenda mbungani mara kwa mara. Nilirudi nyumbani siku chache kabla ya shule kufunguliwa, ila nikwambie tu darasa la tano lote lilijua nilienda Serengeti na niliona wanyama, nilitunga hadi stori za vitu ambavyo sikuviona mfano kumuona Simba akimla nyati.
Tangu wakati huo nimeshaenda hifadhi na mbuga tofauti lakini sijawahi kupata mzuka kama ule wa safari yangu ya kwanza kwenda Arusha.
Baada ya memories za Serengeti kupita kichwani kwangu nikaanza kujiuliza; hivi kama miaka ile ningekuwa nimeanza kucheza games au kuangalia cartoons kwenye smartphones na tablets ningekuwa na ile excitement? Kama Bimkubwa wakati ule angekuwa na smartphone angepata muda wa kujibu maswali niliyokuwa namuuliza au kunionyesha wanyama ambao siwajui na kunitajia majina yao?
Hii pia ikanikumbusha baadhi ya tweets ambazo nimewahi kuziona kwenye timeline ya X watu wakiongelea namna ambavyo njia pekee ya wazazi wa kisasa kuhakikisha watoto wanatulia safari za ndege ni kuwapa simu na tablets wacheze game kuanzia muda wa checkin mpaka take off.
https://medium.com/media/7b0fea85f2bd43e5a4bf3303758677eb/href
Ikanikumbusha pia namna ambavyo ukienda maeneo kama beach au migahawa ambako familia nyingi zinapenda kufanya mitoko ni kitu cha kawaida kuona wazazi wako busy na simu wakati watoto wanacheza, au kuona watoto wako na tablets zao mida ambayo oda za misosi zinasubiriwa.
Kwa kifupi huu ndio uhalisia wa familia za kisasa hasa kwa wazazi ambao ni millenials.
Wazazi wa kisasa teknolojia imekuwa ni njia rahisi ya kuwafanya watoto wajifunze vitu vingi kupitia gadgets, mfano binafsi naamini kama ningekuwa na access ya material ya kujifunzia wakati niko olevel kama ambavyo watoto wa kisasa wanayo naamini nisingehitaji kabisa kwenda tuition hasa ya chemistry ambayo ilikuwa inanisumbua.
Lakini teknolojia vile vile imekuja na hasara yake ambayo nadhani kwa sababu sisi ni kizazi cha kwanza cha wazazi wa watoto wenye access ya teknolojia tumekosa muongozo wa namna ya kutengeneza uwiano kati ya muda mtoto anaotumia kwenye gadget na muda ambao mzazi anatakiwa kukaa kuzungumza na mtoto kutengeneza bond.
Inawezekana kwa sababu unaweza kutimiza majukumu ya kawaida kama kulipa ada, matibabu, chakula etc ikakufanya uhisi kwamba inahalalisha wewe kutumia muda mwingi kwenye kutafuta pesa bila kuwa na muda wa kutosha wa kukaa na watoto na kuacha teknolojia ifanye asilimia karibu 50% ya malezi iliyosalia, bila kujua tunatengeneza kizazi cha watoto ambao emotional connection kubwa wanayo na watu wanaokutana nao mtandaoni kuliko wazazi wao.
Hii pia inatengeneza kundi kubwa la vijana watakaodhani kwamba wao ni “introverts” wakati uhalisia ni kwamba hawana social skills za kukaa na watu kufanya mazungumzo, wanachojua ni kuandika kwenye screen za vifaa vyao.
Ishu ya dogo wa safarini na wengine ambao gadgets ndio zinawalea kwa kiasi kikubwa inaonesha namna gani wazazi wanapoteza nafasi adimu ya kumtengenezea mtoto kumbukumbu ambayo itadumu kwenye maisha yake.
Naomba nimalize na hii tweet niliyoiandika miaka kadhaa nyuma.
https://medium.com/media/2fbd16b29c1081d864a806e5dd6f836f/href
Wasalaam.
Wajibu wa Vijana Katika Ulimwengu wa “Fake News”
Habari Potofu au “fake news” ni kitu ambacho ni gumzo duniani kwa sasa. Tafsiri rahisi yake ya nyepesi ni aina ya habari au propaganda ambayo ina taarifa za kupikwa zinazosambazwa kupitia vyombo vya habari vya kawaida au mitandao ya kijamii na kusambaa kwa kasi kutokana na kuaminika kuwa za ukweli.
Mataifa makubwa yenye mfumo wa demokrasia yamejikuta yakiwa wahanga wakuu kutokana na watengeneza taarifa hizi kutumia mwanya wa uhuru wa kujieleza kusambaza makala, video au mfumo wa sauti kwa lengo la kupotosha. Mfano ni uchaguzi mkuu wa Marekani ambao ulizua utata kutokana na uchunguzi kuonyesha kuwa Urusi ilitumia vita ya taarifa (information war) kumsaidia Donald Trump kwa kutengeneza habari potofu dhidi ya wapinzani wake ndani ya chama cha Republican mpaka kwa mgonbea urais kupitia Democrat, Hillary Clinton na hatimaye kushinda uraisi.
Haikuishia hapo tu, Urusi ilishutumiwa kuingilia baadhi ya chaguzi barani Ulaya kwa kuwaunga mkono wagombea wenye mlengo wa kulia unaohusishwa na siasa za kibaguzi, hii ilipelekea Jumuiya ya Ulaya kupitisha azimio la namna ya kupambana na habari potofu.
Afrika hatujabaki salama katika “fake news” ambapo uchaguzi wa Kenya uliingia katika dosari kwa kampuni ya Cambridge Analytica kutumia taarifa za watumiaji wa mtandao wa Facebook kutengeneza habari potofu zilizowalenga wapinzani wa Rais wa sasa, Uhuru Kenyatta.
Nchini Nigeria, Atiku Abubakar mpinzani mkuu wa Rais Muhammad Buhari alijikuta akishambuliwa na wananchi pamoja na viongozi wa dini baada ya habari ya uongo iliyoanzia Twitter ikionyesha akaunti feki yenye jina lake ikishukuru muungano wa taasisi za kutetea haki za mashoga kwa kumuunga mkono, habari hiyo baadae ilichapishwan katika mojawapo ya magazeti makubwa Nigeria.
Tanzania pia sio wageni wa fake news, mfano katika mojawapo ya magazeti ya leo limechapisha habari kuhusu taharuki iliyozuka hospitali ya muhimbili kufuatia tetesi za kuwepo mwanamke ambaye usiku anageuka ndege na kurejea asubuhi, habari hii ilianzia mtandao wa whatsapp na kusababisha uongozi wa hospitali kutolea ufafanuzi na kukanusha kutokana na ukweli kwamba video hiyo asili yake ni Afrika Magharibi. Kumekuwepo pia matukio ya watu maarufu kuzushiwa taarifa za vifo au kuhusishwa na mahusiano, zote zikianzia kwenye mitandao ya kijamii.
Nini nafasi ya vijana?
Taasisi ya Tanzania Bora Initiative iliandaa mjadala wenye lengo la kujadili namna gani habari potofu zinavyoathiri vijana ambao ndio kundi kubwa la watumiaji wa mitandao ya kijamii. Mjadala pia uligusia njia za kusaidia kupunguza tatizo hili kwa kutumia teknolojia.
Nilibahatika kuwa kwenye jopo la kwanza lililojadili hali halisi ya fake news Tanzania na mbinu gani zimekuwa zikitumika kukabiliana na hili Tatizo. Mike Mushi wa Jamii Forums alielezea kwa kina namba ambavyo mtego-bofya (clickbait) imekuwa chanzo kikuu cha habari potofu kutokana na bloggers au wamiliki wa Online TV wanavyotengeneza vichwa vya habari vya kupotosha ili kuwafanya watumiaji wabofye habari na kuwawezesha kupata pesa kupitia matangazo. Hii iliungwa mkono pia na Antu Mandoza ambaye ni mmiliki wa Radio 7, alielezea uzoefu wake namna ambavyo habari zinazowagusa wasanii wenye majina zimekuwa zikitiwa chumvi hasa kwenye vichwa vya habari.
Vincesia Fuko wa taasisi ya Media Space alienda mbele zaidi na kufafanua uwepo wa waandishi habari jamii (citizen journalist) kunavyochangia kwa kiasi kikubwa kusambaa kwa habari potofu kutokana na kutofahamu miiko ya uandishi wa habari ambayo hupatikana vyuoni. Waandishi habari jamii ambao kwa sasa ni wengi kutokana na kuwa na vifaa ambavyo kwa zamani vilikuwa gharama kubwa na vilimikiwa na vyombo vikubwa vya habari lakini kwa sasa vinapatikana kiurahisi ndani ya simu, yaani kamera na chombo cha habari (mtandao wa internet).
Muwakilishi wa mamlaka ya mawasiliano (TCRA) alijikuta akitupiwa maswali mengi kutokana na namna ambavyo mamlaka hiyo imekuwa ikisimamia sheria ya makosa ya kimtandao ambayo kiuhalisia ndiyo inatakiwa imlinde mwananchi dhidi ya habari potofu. Majibu yake mengi yalionyesha umuhimu wa majadiliano haya kumhusisha muwakilishi wa jeshi la polisi ambao ndio watekelezaji wa sheria hii linapotokea kosa.
Hata hivyo hii haikuzuia mjadala kuangalia namna gani ambavyo vijana wanaweza kuepuka kuwa wasambazaji wa habari potofu. Nilipenda alichokisema Given Edward, muasisi wa MyElimu ambaye alifananisha taarifa tunazozipokea kwenye mitandao ya kijamii sawa na mtu anaekula chakula kingi kwa wakati mmoja na kuishia kuvimbiwa, kutokana na ukweli kwamba mitandao ya kijamii imesababisha upatikanaji kirahisi wa taarifa na hivyo kupelekea watumiaji kushindwa kuzichambua, akatoa ushauri umuhimu wa kutafakari kabla hujaweka taarifa yoyote kama ina umuhimu kwa atakaeiosoma au kama ni lazima wewe ndio uiweke. Paschal Masalu wa Elimika Wikiendi aliongezea kwa kusisitiza umuhimu wa mtu kutambua anachoweka kwenye mtandao ndio kinaakisi yeye ni nani kwenye maisha ya kawaida na kuondoa ile dhana iliyozoeleka kwamba unaweka vitu kwa kujifurahisha kutokana na ukweli kwamba baadhi ya taasisi kabla ya kuajiri hupitia unachokifanya mitandaoni. Lello Mmasy ambaye ni mtunzi wa vitabu aligusia juu ya muhimu wa kutotaka kuwa “makilakitu” kwa kizungu “Jack of all trades” kwa kutaka uwe wa kwanza kuandika kila kitu mtandaoni, badala yake kuchagua vitu vichache ambavyo ni rahisi kufuatilia chanzo chake na kupata uhakika kabla hujakiweka.
Zahra Tunda na Musa Kipanya ambao wote ni waandishi wa habari walijaribu kwa kifupi kueleza miiko ya uandishi wa habari wanayopitia kabla ya kutangaza au kuandika habari yoyote, kitu ambacho kwa citizen journalist hawana na kutoa dondoo za namna ambavyo kijana anatumia mtandao wa kijamii kuhabarisha anaweza kujifanyia uhariri.
Kitu kimoja ambacho wote tulikubaliana ni umuhimu wa vijana kuwa wadadisi na kupenda kujifunza ili kuepuka kuwa wasambazaji wa habari potofu. Pia suala la vijana wenye ushawishi kutumika na wanasiasa liliibuka hasa tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwakani, ambapo wanasiasa hutumia fursa hii kusambaza habari potofu dhidi ya wapinzani wao.
Kwa kifupi vijana tunao wajibu mkubwa wa kupunguza au kumaliza tatizo la fake news. Unaweza kupitia mjadala kupitia hashtag hii kwa kiswahili na hii kwa kiingereza.
Orodha ya Vitabu Nilivyosoma 2018
Mwaka 2018 ndio tunaumaliza na tunajiandaa kuuanza rasmi 2019. Kama ilivyo ada mwanzoni mwa mwaka huwa najiwekea lengo la kusoma vitabu kadhaa, na kwa 2018 lengo ilikuwa ni kusoma vitabu 100. Bahati mbaya sikuweza kutimiza kutokana na hekaheka za vitu binafsi na masuala ya kazi kuingiliana na kunipunguzia kasi ya usomaji katika miezi mitatu ya mwisho wa mwaka.
Hii ndio orodha ya vitabu vyote nilivyosoma ambapo nitachambua 10 ambavyo vimekuwa bora kwangu na kisha vingine vilivyosalia vitafuatia kwa chini.
Unfu*K Yourself — Gary John Bishop
Nilikisoma kitabu hiki wakati napitia msukosuko na kilipendekezwa na rafiki yangu Neelam Babul ambaye ni msomaji mzuri wa vitabu. Nilichopenda ni namna mwandishi anavyotumia lugha rahisi inayofanya uhisi anaelewa kinachoendelea kichwani mwako. Nakipendekeza kila mtu akipata nafasi akisome, kuna vitu vingi vya kujifunza ndani yake.
2. Gunning For Greatness — Mesut Ozil
Kila mpenzi wa mpira wa miguu anafahamu namna Ozil anavyosifika kwa aina yake ya uchezaji mpira. Hata hivyo nyuma ya mafanikio yake kuna vitu vingi vigumu amepitia mpaka kufikia hapo alipo, akiwa kama mtoto wa wahamiaji nchini Ujerumani toka Uturuki. Kwenye kitabu hiki Ozil anaelezea kwa kirefu safari yake toka kwenye kukabiliana na ubaguzi, kusumbuliwa na waandishi wa habari na kuendana na maisha ya soka katika klabu zote alizopitia mpaka alipo Arsenal kwa sasa.
3. I Can, I Must, I Will — Reginald Mengi
Kwa muda mrefu tumekuwa tukilalamika namna ilivyo rahisi kujifunza kupitia kwa vitabu vya mabilionea wa nchi nyingine kama Warren Buffer, Bill Gates, Aliko Dangote, Jeff Bezos nk lakini ni ngumu kupata vitabu vya wafanyabiashara waliofanikiwa nchini, nadhani Mzee Mengi alisikia kilio chetu na akaamua kuandika kitabu hiki ambacho kinaelezea kwa kirefu namna alivyofikia hapo alipo. Pia anaongea kuhusu changamoto za siasa nchini kwa sekta ya biashara akitolea mifano ya vigingi alivyokutana navyo katika awamu zilizopita na namna vilivyomjenga.
4. Fascism: A Warning — Madeleine Albright
Madeleine Albright anajulikana kwa umahiri wake kama mwanadiplomasia mkongwe na katika kitabu hiki anatumia ujuzi wake kuonyesha namna siasa ya dunia inavyopiga hatua nyuma sawa na ilivyokuwa enzi za madikteta wa zamani. Ameeleza namna Marekani inayojihesabu kama baba wa demokrasia isivyokuwa tofauti na watu kama Musolin kwa sasa chini ya utawala wa Donald Trump. Ni kitabu kizuri kwa mtu anaependelea siasa na diplomasia, utajifunza vitu vingi hata kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini.
5. From Dictatorship to Democracy — Gene Sharp
Katika kitabu hiki Gene Sharp ambaye ni Profesa wa Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Massachusetts anatoa somo zuri kwa nchi zinazopitia tawala zenye dalili ya udikteta au viongozi wanaotumia mkono wa chuma. Humu anatolea mifano ya nchi zilizofanikiwa kuziondoa tawala hizi bila kutumia umwagaji damu. Ni moja ya vitabu vilivyonibadilishia mtazamo wa namna ya kuleta mabadiliko.
6. This is Me — Chrissy Metz
Chrissy Metz ni muigizaji katika TV Series ya This Is Us. Baada ya wazazi wake kuachana Chrissy alilazimika kuishi na mama yake baada ya baba yake kukataa kujihusisha na maisha yake hivyo kulazimika kukabiliana na baba wa kambo na pia kumsaidia mama yake kulea wadogo zake. Kutokana na kuwa na unene uliopitiliza Chrissy alijikuta akipitia unyanyasaji toka kwa baba zake wa kambo mpaka wanafunzi wenzake na watu wengine. Inaweza kuwa somo zuri kwa ambao wamezoea kuwatania watu wenye matatizo ya uzito uliopitiliza bila kujua tunawajengea matatizo gani ya kisaikolojia.
7. Mtafiti — Hussein Tuwa
Huwezi kuongelea watunzi bora wa riwaya nchini bila kumtaja Hussein Tuwa. Aina yake ya uandishi inakufanya ufuatilie kwa makini mwanzo mpaka mwisho huku ukikutana na taharuki za kutosha katika riwaya zake, na katika Mtafiti hakutuangusha wasomaji wake.
8. It Happened at the Wall — Reiner Hildebrandt
Kitabu hiki kilichochapishwa kwa lugha tatu ndani yake kinaonyesha picha za matukio ya kipindi cha utawala wa Adolf Hitler mpaka kuanguka kwa ukuta wa Berlin. Nimependa namna picha zilivyokusanywa kwa mtiririko mzuri na kinavyoelezea matukio waliyokumbana nayo wahanga.
9. Multipliers — Liz Wiseman
Kitabu kizuri sana kwa waanzilishi wa Startup kikielezea namna nzuri ya kuwa kiongozi mara biashara inapoanza kukua na kujikuta unasimamia watu wengi.
10. Obama: An Intimate Potrait — Pete Souza
Pete Souza aliekuwa mpiga picha wa Rais Obama katika kipindi chote alichokuwa madarakani anaeleza kwa kirefu picha mbalimbali alizompiga Obama na familia yake na kuweka nyingine nyingi ambazo hazikupata nafasi ya kuonekana katika vyombo vya habari. Ni kitabu kizuri kwa wanasiasa na wapiga picha wa watu maarufu.
11. Mobinomics — Alan Knott-Craig
12. I’ll Be Gone In the Dark — Michelle McNamara
13. Russian Roulette — Michael isikoff & David Corn
14. Hujuma — Elvis Musiba
15. Njama — Elvis Musiba
16. Kufa na Kupona — Elvis Musiba
17. Kikosi Cha Kisasi — Elvis Musiba
18. Nine Parts Of Desire — Geraldine Brooks
19. Bulls Eye — James Patterson
20. The Book Of Negroes — Lawrence Hill
21. The Vacationers — Emma Straub
22. The Girl On The Train — Paula Hawkins
23. One Step Ahead — Timothy Spangler
24. Gunning For Greatness — Mesut Ozil
25. Scaling Up — Verne Harnish
26. All The Light We Can Not See — Anthony Doerr
27. The Aeronauts Windlass — Jim Butcher
28. Trust — Jana Aston
29. Wrong — Jana Aston
30. A Man Called Ove — Backman Fredrik
31. Someone to Love — Mary Balogh
32. Our 50 State Border Crisis — Howard G. Buffet
33. Jack Reacher’s Night School — Lee Child
34. A Higher Loyalty — James Comey
35. The Wrong Side Of Goodbye — Michael Connelly
36. The Dictator’s Learning Curve — Dobson William J
37. Leopard’s Fury — Christine Feehan
38. Order To Kill — Vince Flynn (Kyle Mills)
39. The Whistler — John Grisham
40. Russian Roulette — Michael Iskoff & David Corn
41. This Was A Man — Jeffery Archer
42. The Chemist — Stephenie Meyer
43. Say You Want Me — Corrine Michaels
44. Enemy Of The State — Vince Flynn (Kyle Mills)
45. Pound Foolish — Helaine Olen
46. 12 Rules For Life — Jordan B Peterson
47. Killing The Deep State — Jerome R Corsi
48. Small Great Things — Jodi Picoult
49. One Snowy Night — Jill Shalvis
50. Astrophysics for People in a Hurry — Neil Degrasse Tyson
51. At the Sign of Triumph — David Webber
52. Educated — Tara Westover
53. Fire and Fury — Michael Wolff
54. Turning Pro — Steven Pressfield
55. Superficial — Andy Cohen
56. Fadhili Msiri wa Naugua — Ali Kondo Chuma
57. Magnolia — Gaines Chip
58. Strangers in Their Land — Hochschild Arlie Russel
59. When Breath Becomes Air — Paul Kalanithi
60. Settle For More — Megyn Kelly
61. Testimony — Robbie Robertson
62. Alexander Hamilton — Ron Chenrow
63. Our Revolution — Bernie Sanders
64. Born To Run — Bruce Spingsten
65. Hillbilly Elegy — J.D Vance
66. Legacy of Force — Aaron Allston
67. Solo Command — Aaron Allston
68. Jedi Academy — Kevin Anderson
69. The Phantom Menace — Terry Brooks
70. One of a Kind — Paul Danner
71. The Boys in the Boat — Daniel James Brown
72. The Burning Room — Michael Connelly
73. Diary of a Wimpy Kid — Jeff Kinney
74. Dark Places — Gillian Flynn
75. If I Stay — Forman Gayle
76. You Were Mine — Abbi GLines
77. Jason — Laurell K Hamilton
78. Revival — Stephen King
79. House of Robots — James Patterson
80. Wild — Cheryl Strayed
81. Money — Tony Robbins
82. The World Is Flat — Thomas L. Friedman
83. The Food Of Love — Anthony Capella
84. House Rules — Jodi Picoult
85. After Blair — Kieron O’hara
86. The Top Ten Mistakes Leaders Make — Hans Finzel
87. The Shadow Of The Wind — Carlos Ruiz Zafon
88. Heartbroken — Jackson Fute
89. The Lean Startup — Eric Ries
90. The Solution Focus — Paul Z Jackson
91. Siri ya Rais — Ragin Mbaga
92. Comfort & Joy — Kristin Hannah
93. Isara — Wole Soyinka
94. The Liar — Nora Roberts
95. Thoughtful — S C Stephens
Wiki iliyopita August 22–23 nilipata fursa ya kuwa sehemu ya kongamano la wadau wa Rasilimali madini, gesi na mafuta lililofanyika jijini Nairobi, lengo hasa likiwa ni kubadilishana ujuzi na kujifunza huku likihusisha wadau sekta za kijamii (CSO) zinazoshughulika maeneo yenye rasilimali hizi na pia wanahabari ambao wamejikita kwenye sekta hii.
Miaka ya karibuni Afrika Mashariki imekuwa kitovu cha uchimbaji rasilimali za mafuta, gas na madini kufuatia ugunduzi wa gas mikoa ya kusini mwa Tanzania bila kusahau uchimbaji madini maeneo mbalimbali nchini, wakati huo Kenya wamegundua mafuta na makaa ya mawe katika eneo la Turkana huku Uganda nao wako katika hatua za kuanza uchimbaji wa mafuta yaliyogunduliwa katika eneo la Hoima ambapo mradi wa bomba la kuyasifirisha mafuta hayo mpaka bandari ya Tanga tayari upo mbioni.
Ugunduzi wa rasilimali kwa masikio ya wengi inakuwa habari njema kutokana na kuwaza faida itakayopatikana kutokana na uwezekaji bila kusahau maendeleo yatakayoletwa kupitia mgao wa faida serikali inaopata. Hata hivyo uzoefu toka baadhi ya mataifa yaliyotutangulia kugundua rasilimali hizi umeonyesha namna gani ambavyo badala ya kuwa neema kwa wananchi imeishia kuwa chanzo cha mkosi uliopewa jina la laana ya rasilimali (resource curse) kutokana na mataifa hayo kuishia kuingia kwenye mgogoro au machafuko yaliyosababishwa na upande mmoja kuhisi haupati unachostahili katika rasilimali hizi. Chukulia mfano Sudani Kusini na Congo.
Ni kwa kupitia uzoefu huu shirika la Oxfam ambalo linafanya kazi katika nchi zote hizi tatu kwa kuendesha na kufadhili miradi yenye lengo la kuondoa umaskini iliamua kuwakutanisha wadau wa taasisi binafsi na wanahabari kuweza kushauriana namna gani wanaweza kusaidiana katika kuhakikisha mataifa haya yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki yanajiandaa kukabiliana na changamoto zinazoweza kusababisha laana ya rasilimali.
Siku ya kwanza ilijikita katika kufahamu hali ilivyo katika jamii zilizo kwenye maeneo ya mradi kiuchumi na mazingira, mgawanyo wa faida ya rasilimali hizi na uwazi wa mikataba.
Jopo la kwanza lilikuwa na wawakilishi toka maeneo yenye mradi ambapo kwa Tanzania alikuwa ni Hamisi Juma, Mtendaji kata Wilaya ya Lindi, Winfred Ngabiirwe Mkurugenzi Mtendaji taasisi ya Global Rights Alerts, Rose Birgen Meneja Programu wa taasisi ya Natural Justice na Titus Gwemende wa Oxfam.
Katika mjadala wa kwanza uliohusisha panel discussion ilionekana changamoto nyingi katika maeneo yenye rasilimali zinafanana, mfano wakazi wa Turkana walioombwa kupisha muwekezaji mpaka sasa hawajapatiwa maeneo mengine kwa shughuli za kilimo, sawa na wale wa Hoima Uganda ambao wamejikuta wakiwa kama wakimbizi kutokana na kukosa maeneo ya kufanyia shughuli za uzalishaji mali kama kilimo na ufugaji. Vilevile uharibifu mazingira ambao unasababishwa na shughuli za uchimbaji rasilimali hizi bado unaonekana haujapatiwa suluhisho kutokana na ukweli kwamba hakuna utashi wa dhati wa serikali za nchi zote katika kukabiliana na kasi ya uharibifu mazingira.
Hata hivyo Tanzania ilitolewa mfano kwa namna ambavyo taasisi za kijamii zimeweza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kuhoji na kufuatilia haki zao za msingi kwenye uchimbaji rasilimali. Hamisi Juma ambaye ni Mtendaji wa Wilaya ya Lindi alielezea namna ambavyo kumekuwa na mawasiliano kati ya wananchi, serikali na wawekezaji ili kuepusha migogoro toka awali. Hii inaweza kuwa imesaidiwa na uzoefu ambao Tanzania imeupata toka katika miradi ya uchimbaji madini hasa Mkoani Mara. Pamoja na kwamba bado hawajalipwa kwenye eneo la mradi wa gas lakini angalau hakuna migogoro mingi iwe ya watu kuhamishwa kiholela au uharibifu mazingira kulinganisha nan chi jirani.
Wadau wengine wa mashirika na taasisi waliweza kuelezea ujuzi na uzoefu wao katika maeneo yao ya kazi, pengine walionivutia zaidi walikuwa ni Dr Claude Kabemba wa Southern Africa Resource Watch (SARW) na Silas Olang wa Natural Resource Governance Institute. Wote kwa nyakati tofauti walielezea kwanza namna gani taasisi za kijamii zinapaswa kuacha kufanya kazi kimazoea kwa kutoka nje ya eneo lao walilolizoea (comfort zone) ambapo nyingi zimekuwa zikifanya kiuharakati zaidi.
Dr Claude Kabemba alisisitiza umuhimu wa taasisi hizi kufanya kazi kwa mtindo wa kukaa mezani na serikali kwa ushirikiano (partnership) badala ya ule utaratibu uliozoeleka wa kuzisuta mamlaka. Alienda mbali zaidi kwa kukumbusha umuhimu wa kuwafunda watunga sera kuhusu sheria za kimataifa na hata kuwapa taarifa za muhimu toka katika tafiti zilizofanywa kuhusu makampuni au biashara inayohusisha rasilimali hizi kwa ujumla.
Silas Olang alieleza umuhimu wa kuhakikisha wanahabari wanasaidia kujenga jamii yenye taarifa sahihi na yenye kuhoji akisisitiza umuhimu wa kuandika taarifa zenye kuelimisha kuhusu rasilimali ili wananchi watambue kwamba kuna siku zitaisha kwa hiyo wajue namna gani wanafaidika na kinachopatikana.
SOMO TOKA NAIROBI
Kwa mimi kama mtumiaji mzuri wa mitandao ya kijamii hasa Twitter na Blogs nilijifunza namna gani tuna nguvu ya kuwa sehemu ya mabadiliko kwenye sekta ya rasilimali. Kuna mifano mingi ambayo changamoto zimetatuliwa baada ya kuletwa hadharani pamoja nguvu kubwa inayotumika kuvizuia vyombo vya visiziandike; na kwa sekta ya madini, gesi na mafuta hili nalo linawezekana kwani mwisho wa siku hakuna kampuni inayopenda kuhusishwa na biashara chafu.
Ilikuwa kama bahati kongamano hili lilifanyika wakati Afrika Mashariki nzima ikiwa imeunganishwa na tukio la kukamatwa mwanamuziki Bobi Wine na ilitolewa mfano namna ambavyo ushirikiano huu unaweza kuhamia katika masuala la Rasilimali Madini, Mafuta na Gas. Niliweza kuona namna ambavyo kuna haja ya kuwa na ushirikiano na wadau wa nchi nyingine za Afrika Mashariki katika kupaza sauti pale mambo hayaendi sawa, kwa kutilia maanani kwamba nchi zote tatu zimepitisha sheria kali za kuwabana watumiaji wa mitandao ya kijamii hivyo kufanya kuwe na umuhimu Blogger au Social Media Influencer alieko Lindi kuguswa na tatizo linalomgusa mtu wa Turkana au Hoima na kusaidia kupaza sauti kunapokuwa na changamoto kubwa.
Na la umuhimu kabisa ambalo tunahitaji kulibebea bango, ni uwazi katika mikataba mikubwa serikali inayoingia na wawekezaji ili kufahamu kiasi gani kinapatikana. Hiki ndio chanzo kikuu cha yote yaliyotajwa hapo juu na endapo tutafanikiwa kushawishi serikali zetu kuwa na uwazi na kuruhusu maoni ya wataalam kabla hatujaingia mikataba hii naamini kila mwananchi ataona faida ya rasilimali zetu badala ya kulalamika.
Wasalaam.
Jumanne wiki hii nilikaribishwa katika uzinduzi wa huduma tatu mpya za Benki ya NMB uliofanyika Hyatt Hotel na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya fedha, teknolojia na baadhi ya wateja wa NMB. Huduma hizo zilikuwa ni uwezo wa mwananchi kufungua akaunti kupitia simu yake ya mkononi, App yenye huduma zote ambazo mteja anaweza kufanya mwenyewe badala ya kwenda kwenye tawi na Scan to Pay huduma ya kufanya malipo kwa kutumia QR code.
Moja ya kitu kilichonivutia ilikuwa ni jopo la majadiliano ambalo liliwahusisha Irene Mlola toka FSDT, Eng. George Mulamula wa DTBi, Scholastica Kevela wa YONO Auction Mart na Emmanuel Mung’ong’o wa Benki Kuu Tanzania. Majadiliano yalijikita katika kujadili namna Tanzania inavyoweza kupiga hatua katika Ushirikishaji Kifedha (Financial Inclusion) na kutengeneza jamii yenye mfumo wa malipo usiotegemea fedha taslimu (Cashless Society).
Nilichokipenda ilikuwa ni jibu la Engineer Mulamula alipokuwa akijibu swali ni namna gani ubunifu wa teknolonia unaweza kufanya benki ziwahudumie Watanzania wengi zaidi ambapo alisema Benki zinatakiwa kuwaza nje ya boksi toka kwenye mazoea ya kwamba kazi yao ni kufungua akaunti za kutunza fedha za wateja na kutoa mikopo, akasisitiza kwamba zinatakiwa kubuni huduma zitakazoboresha maisha ya Mtanzania wa chini. Wakati anatoa jibu hili tulikuwa bado hatujafahamu NMB wanazindua nini hasa, na baada ya kutajiwa kwamba uzinduzi huu ni wa huduma za kumuwezesha mwananchi wa kawaida kufungua akaunti kwa simu yake na kisha kuwa na uwezo wa kufanya huduma zote ambazo angepaswa kwenda kwenye tawi ndio nikaanza kuwaza alichokisema Engineer Mulamula.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na CEO wa NMB ni 17% tu ya Watanzania waliofikiwa na huduma za benki nchini, lakini wakati huo 70% wanatumia simu zao za mkononi kufanya miamala ya kifedha, kwa hiyo kiuhalisia Benki zimelazimika kuhamia kwenye simu za mkononi ili kupata kipande cha hiyo keki inayopendwa na 70% ya Watanzania.
Cha kujiuliza ni je watafanya nini cha ziada kumfanya mtu wa kawaida ambaye ameshazoea kutumia huduma za kifedha kupitia mtandao wa simu kama M-Pesa, Tigopesa na Airtel Money arudi Benki. Hapo ndo alichokisema Mulamula kinakuja, KUWAZA NJE YA BOKSI.
KUTOKA NJE YA BOKSI
Mitandao ya simu ilitumia udhaifu wa sekta ya Benki nchini ambazo ukiachilia mbali kwamba hazikuwa na matawi ya kutosha nchini, pia utaratibu wa kufungua akaunti ulikuwa na mlolongo mrefu na hapo hujagusia foleni kwenye matawi machache yaliyokuwepo.
Kitu cha kwanza ambacho naamini Benki zinaweza kuwaza nje ya boksi ni kuwa sehemu ya Ushirikishaji Kifedha toka hatua ya awali kabisa kwa mwananchi wa chini, hapa tunamzungumzia mkulima na mjasiriamali mdogo ambapo haya ndio makundi makubwa mawili ambayo hayajafikiwa na huduma za Kibenki.
Ukianza na mkulima wote tunajua namna ambavyo ili aweze kupata mazao ya kutosha anahitaji kuwa na pembejeo bora, na mara baada ya kuuza atahitaji soko la uhakika. Hata hivyo wakulima wengi wamekuwa wakihangaika kutokana na ukweli kwamba mara baada ya kuvuna na kuuza kiasi wanachobali nacho ni kidogo kuweza kujiandaa na msimu mpya wa kilimo na kupelekea wengi kuishia kuuziwa mbegu au mbolea ambazo hazina kiwango. Natarajia kuona Benki zikitumia ubunifu wa kitenolojia kuwa sehemu ya mnyororo wa thamani, mfano kupitia vyama vya ushirika zinaweza kuwaunganisha wakulima na wauzaji pembejeo na kisha wanunuzi. Yote haya yanaweza kufanyika bila fedha kupita mkononi (cashless) ikimaanisha benki inamuunganisha mkulima na msambazaji wa pembejeo ambaye atahakikisha anapata mbegu, mbolea na hata ushauri inapobidi. Benki haiishii hapo, inaweza kuwakutanisha wanunuzi wa mazao na mkulima huyu ikimaanisha baada ya mavuno mkulima ana uhakika wa soko la mazao. Mwisho wa siku kila mmoja anapata.
Hii inaweza hata kwenda kwa mfanyabiashara mdogo mwenye mgahawa lakini hana mtaji wa kutosha kuweza kuwafikia wateja wengi, lakini ni rahisi kwa Benki kuwa mtu wa kati na kumuunganisha mjasiriamali huyu na Azam au Mo Enterprise wampatie ngano, sembe, mafuta, katoni za maji nk. Kwa kifupi ni kwamba Benki zina wajibu wa kuunganisha kila mdau wa kwenye mnyororo wa thamani ili kusaidia kuongeza mzunguko wa fedha katika kila sekta.
Naamini hiki ni kitu kinachowezekana sana ukizingatia kwamba Benki tayari zimejijengea kuaminika na kila mhusika kwenye mnyororo wa thamani na zina kila miundombinu ya kufanikisha ushirikishwaji kifedha kwa kila mwananchi.
Ni matumaini yangu NMB inaweza kuongoza usukani katika hili kutokana na namna ilivyoweza kusambaa nchi nzima ikiwa na matawi katika kila wilaya na mawakala wengi kushinda benki zote. Natarajia kuona vitu kama hivi kupitia Menu mpya ya NMB KliK iwe ni kwenye *150*66# au App. Na isiishie kwa NMB pekee, benki nyingine nazo ziige.
Heri ya Mwaka Mpya
Mwaka 2017 kwa upande wangu ulikuwa umejaa mchanyato wa vitu tofauti lakini hiyo haikuzuia utamaduni wangu wa kujisomea vitabu ingawa sio kwa kiasi kile nilichotaka kutokana na majukumu kuwa mengi. Niliweza kusoma jumla ya vitabu 30 asilimia kubwa ikiwa ni vya kuongeza Maarifa/Ujuzi ikifuatiwa na vya simulizi na vingine kadhaa vya Wasifu wa baadhi ya watu.
Kwa watumiaji wa Twitter wanafahamu nilikuwa na Thread ambayo nilikuwa naweka vitabu nilivyokuwa navisoma kwa wakati huo ingawa kuna vingine nilivisahau.
Naomba nikushirikishe vitabu vyenyewe:
1. Death of a Mafia Don — Michele Giutari
Kilikuwa kitabu cha kwanza na sababu kubwa ya kukichagua nilihitaji kitu cha kuuchangamsha ubongo safarini. Ni simulizi inayoelezea vita baina familia za wauza madawa ya kulevya. Hakijafikia utamu wa The Godfather.
2. Grit — Angela Duckworth
Katika kitabu hiki Angela Duckworth anajaribu kuelezea kwa nini watu waliozaliwa na karama wanashindwa kufanikiwa tofauti na wale ambao wamezaliwa kawaida lakini wanachagua kukomaa usiku na mchana mpaka kufikia malengo yao.
3. Shoe Dog — Phil Knight
Nina uhakika kila mmoja wetu katika maisha yake amevaa au kutumia bidhaa mojawapo ya Nike, ni kati ya kampuni zinazoingiza mabilioni ya dola kila mwaka ikiwa imetoa ajira lukuki duniani bila kusahau namna inavyowaneemesha wanamichezo. Lakini nyuma yake yupo Phil Knight ambaye ndie muasisi wake na katika kitabu hiki ameelezea kila kitu tangu anaianzisha Nike mpaka ilipofikia hapo ilipo. Ni kitabu kizuri kwa wajasiriamali wanaoanza.
4. Disrupted — Dan Lyons
Statup nyingi zilizofanikiwa zimewajengea watu picha kuwa ni sehemu nzuri sana za kufanyia kazi. Hata waanzilishi wake wanatumia nguvu kubwa hasa kwenye social media kuwaaminisha watu kuwa mambo ni mteremko, na kufanya vijana wengi watamani kukimbilia huko. Hata hivyo Dan Lyons ambaye amefanya kazi Forbes, Newsweek, ReadWrite na HubSpot anafichua “siasa” za ndani ya Startup na kuonyesha kuwa maisha sio rahisi kama tunavyodhani kufuatia uzoefu wake ndani ya HubSpot.
5. The Panther — Nelson Demille
Kwa wapenzi wa riwaya za kiupelelezi lazima watakuwa wanaomfahamu John Corey watakuwa wanaijua shughuli yake, na katika mfululizo huu hajatuangusha.
6. #AskGaryVee — Gary Vaynerchuck
Huwezi kuzungumzia nguli wa masoko mtandaoni “digital marketing gurus” bila kumtaja Gary Vaynerchuck na katika kitabu hiki amekusanya maswali mengi ambayo amekuwa akiulizwa na watu wanaotaka kujifunza kupitia kwake na kuyaweka kwa pamoja.
7. The Elements of Content Strategy — Erin Kissane
Naomba niseme wazi sikukisoma kwa kupenda, nilikuwa naangalia moja ya TedTalk na mmoja ya wasemaji akakitolea mfano nikaamua kukitafuta. Hata hivyo sikujuta.
8. Digital Fortress — Dan Brown
Kama umesoma vitabu vingine vya Dan Brown unaelewa aina yake ya uandishi ambayo kwa kiasi kikubwa inakutesa na kukufanya ushindwe kutabiri nini kitatokea mbele ya safari na nani atakuwa mtuhumiwa mkuu. Digital Fortress ni aina ile ile.
9. The Alliance — Reid Hoffman, Ben Casnocha & Chris Yeh
Waasisi wa LinkedIn na Comcate wanaelezea kwa kirefu kwa nini imekuwa ngumu kwa makampuni na biashara kuwazuia wafanyakazi wake bora hasa vijana kuhama toka kampuni moja kwenda nyingine pamoja na kuwaahidi maslahi mazuri.
10. The Girl With The Lower Back Tattoo — Amy Schumer
Amy Schumer ni kati ya wachekeshaji wazuri sana wa jukwaani na pia muigizaji mzuri wa filamu na katika kitabu chake hiki cha wasifu amejaribu kuelezea maisha yake kwa lugha ambayo imejaa ucheshi mwingi lakini inakuonyesha kuwa hapo alipo amehangaika mno hadi kupafikia.
11. Deliver Us From Evil — David Baldacci
Ni riwaya kipelelezi ikiwa ni ya pili katika mfululizo wa A. Shaw na Katie James. Kusema kweli sikukifurahia kama ilivyo kwa vitabu vingine vya Baldacci.
12. Business Model Generation — Alexander Osterwalder and Yves Pigneur
Kitabu kizuri kwa wanaoanzisha biashara au ambao tayari wana biashara kujifunza namna ya kutengeneza mkakati wa kuzifanya ziweze kujiendesha kwa ufanisi hata pale wasipokuwepo. Tatizo pekee nililoliona ni kuwa baadhi ya vitu haviwezi kufanyika kwa mazingira ya Afrika kwa hiyo za kuambiwa changanya na za kwako wakati unakisoma.
13. Msukule — Jackson Fute
Rafiki yangu Jackson Fute ni mwandishi mzuri wa simulizi na nilikuwa mmoja ya watu wa kwanza kusoma kitabu chake hiki ambacho kipo kwenye mfumo wa ebook.
14. Simulizi za Azimio la Arusha — Profesa Issa Shivji
Mwamko wa Azimio la Arusha umekuwa mkubwa tangu awamu ya tano iingie madarakani kwa hiyo ilikuwa ni muda muafaka wa kujikumbusha lilikuwa na lengo gani na kama kwa upepo wa siasa za sasa linaweza kufanya kazi miaka 50 tangu lilipoanzishwa.
15. The Divine Comedy — Dante Alighieri
Niliamua kukirudia kitabu hiki ambacho nilikisoma kwa mara ya kwanza 2010 baada ya kuwa mojawapo ya vitabu tulivyokuwa tunavifanyia mapitio kwenye Book Club.
16. Macbeth — William Shakespeare
Kiliwekwa iSwapMyBooks nikakichukua kujikumbushia enzi hizo za shule wakati tunajaribu uigizaji bila mafanikio.
17. The Rain Maker — John Grisham
Ukisoma vitabu vingi vya John Grisham unaweza tamani kurudi shule kusomea sheria kutokana na namna anavyoweza kuandika simulizi zenye mchuano unaohusisha mahakama au sheria kwa namna moja au nyingine, The Rain Maker ni kati ya vitabu hivyo.
18. The Burning Room — Michael Connely
Mpelelezi Harry Bosch anarudi tena kwenye mfululizo huu kutatua kesi ambayo inawapasua kichwa baada ya kumsaka mdunguaji aliefanya mauaji na kupotelea kusikojulikana.
19. This How You Lose Her — Junot Diaz
Rafiki yangu Joyceline alipoweka Twitter picha ya cover la hiki kitabu wakati anakisoma nikajua ni maufundi ya namna ya kufanya usimpoteze asali wa moyo lakini kumbe ni riwaya ya mahaba yenye wahusika wa Latin America. Hata hivyo nilikifurahia aina yake usimuliaji.
20. Tough Times Never Last But Tough People Do — Robert Schuller
Askofu Robert Schuller anatumia mifano ya vikwazo alivyopitia yeye, familia na watu aliokutana nao katika maisha kukumbusha kuwa kila gumu katika maisha lina mwisho. Hiki nacho nilibadilishana na Joyceline.
21. The Courtship Of Princess Leia — Dave Wolverton
Kila mpenzi wa Star Wars ana kitabu anachokipenda, na kwangu hiki ndio bora zaidi. Nilikisoma kwa mara ya kwanza mwaka 2002 na kila mwaka nimekuwa na utaratibu wa kukirudia nikihitaji kuchangamsha ubongo.
22. Born A Crime — Trevor Noah
Trevor Noah anajulikana kama mmoja ya wachekeshaji bora duniani na alizaliwa Afrika Kusini. Ukifuatilia ucheshi wake amekuwa na tabia ya kuzungumzia maisha yake wakati anakulia Afrika Kusini yenye ubaguzi hadi inapata uhuru na kufikia hapa ilipo sasa. Namshukuru Queen Saidi kwa kunitumia kitabu hiki.
23: Elon Musk: Tesla, SpaceX, and the Quest for a Fantastic Future — Ashlee Vance
Mara ya kwanza namsikia Elon Musk ilikuwa ni 2012 wakati wa Barack Obama na Mitt Romney wanachuana kwenye mdahalo ambapo Romney alimlaumu Obama kwa kutumia hela za walipa kodi kusaidia makampuni ambayo yalikuwa yanaelekea kufikilisika wakati mdororo wa kiuchumi 2008 wakati yalikuwa hayajaanza kuingiza faida. Tesla ambayo muasisi wake ni Elon Musk ilitolewa kama mfano. Hata hivyo muda mchache baada ya Obama kuchaguliwa kwa awamu ya pili Tesla ilianza kuingiza faida huku hisa zake zikifanya vizuri na wakafanikiwa kurudisha mkopo ndani ya muda mfupi. Baada ya hapo nilijikuta napenda kumfuatilia Elon Musk ambaye anafananishwa na Tony Stark ambaye ni anawakilisha character ya Iron Man kwenye filamu na comic book za Marvel. Kitabu hiki naweza kusema ni kati ya vitabu bora 5 nilivyosoma 2017.
24: The Strongman: Vladimir Putin and the Struggle for Russia — Angus Roxburgh
Nilikiona kwa mara ya kwanza kwenye orodha ya vitabu alivyovisoma Zitto Kabwe 2016 nikaamua kukiweka kwenye orodha yangu. Kimenisaidia sana kuelewa hali ya siasa ambayo dunia inapitia kwa sasa, sikushangaa hata iliposemekana kuwa Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani.
25: Origin — Danny Brown
Ni kitabu kipya kilichotoka 2017 kikiwa ni mfululizo wa Dr Robert Langdon ambaye safari hii anakwepa wauaji wanaomsaka wakati huo akijaribu kupata majibu ya nini kimemuua rafiki yake aliepigwa risasi wakati akijiandaa kuitangazia dunia kuhusu uvumbuzi ambao ungebadili suala la binadamu na imani kwa Mungu.
26. Meditations — Marcus Aurelius
Ni kitabu kilichotokana na machapisho binafsi ya Marcus Aurelius aliekuwa mtawala wa dola ya Roma miaka ya 160 na 180 AD. Machapisho yake nimekuwa nikikutana nayo kwenye vitabu vya maarifa ninavyosoma nikapata hamu ya kukisoma hiki.
27. The Special One — The Secret World of Jose Mourinho — Diego Torres
Kimeelezea vizuri yaliyo nyuma ya pazia kwa maisha ya kocha wa Man United Jose Mourinho.
28. Thomas Jefferson and Tripoli Pirates — Brian Kilmeade & Don Yaeger
Ukikisoma kitabu hiki kinakupa picha ya kuwa Marekani iko hapo ilipo kwa sababu waasisi wake waliamua kutengeneza taifa lenye nguvu duniani. Ni matukio yaliyowekwa kwa mfumo wa simulizi yanakufanya usitake kuacha kukisoma.
29. The Innovators DNA — Jeff Dyer & Clayton M. Christensen
Ilikuwa zawadi toka kwa mmoja ya watu waliohudhuria uzinduzi wa iSwapMyBooks. Kitabu kinaeleza vitu vitano ambavyo wagunduzi wote wakubwa wanavyo na vinaendelea kuwabeba mpaka sasa.
30. Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi — Yericko Nyerere
Naomba niseme tangu kitabu hiki kipo kwenye hatua za muswada nilikuwa nakipitia lakini sikuweza kukisoma kwa uvivu wa kuwa nakifahamu, ila ilibidi nikisome vizuri ili nibishane na rafiki yangu Yericko.
Hii ndio orodha kamili ya vitabu nilivyovisoma 2017, lengo langu 2018 ni kusoma vitabu angalau 50 na nusu yake iwe ni vitabu vya waandishi wa Afrika.
Heri ya mwaka mpya 2018.