Stories by Erica Musa Mwakitwange on Medium
In the midst of it all.. Nakutamani!!
Rahisi sana kukupoteza. Sio kwamba kweli unapotea ila mimi ndio napotea na kupotezwa na purukushani nyingi za maisha. Paap siku inaanza.. Inawezekana una muda unasali asubuh kabla hujatoka kitandani, pengine una ratiba yako ya "devotion" Namna ambayo unajua unaitumia kumshirikisha Mungu siku yako lakini mara paap siku inaisha.
Ndio niliomba, sawa pengine niliabudu, kuna muda inawezekana kabisa nilisoma na biblia ila kuna namna unasikia ndani yako haitoshi. Kuna namna unaona kabisa imekuwa ratiba. Nimeingia nimetoka. Nimekaa nikamaliza nikainuka na kuendelea na siku. Lakini bado kuna kiu. Ndani yangu kuna kiu, kuna namna kuna kitu naona kabisa hakijapata jibu wala suluhu. Ni kama kutaka maji afu kunywa soda, unajua kabisa utamaliza soda ila bila maji unabaki pale pale.
Najua kuna zaidi ya hapa. Najua. Na nakusikia, unaongea, nakusikia kuna mda tunatembea kabisa ila ndani yangu najua kuna zaidi.
In the midst of ALL of it.. The chaos, the busyness, the routine that gets thrown out almost all the time because of all the LIFE that has to happen... In all of it I KNOW there's more to you, more to this. More to our relationship and how much even more REAL you can be. More evident you can be. The one who is not even closer than anyone. The one who is ME than even I can be.. For you are me and I died on the cross. My life is YOU..
Today I am expressing my absolute consuming need for you! I dont even want to know you... I seek a demonsteation of the you in me. I seek to be who you say I am. I seek to live, breathe, and be you, for you! Jesus.. I don't only love you.. I want you! Nakutamani!!! Show me more of you.. Reveal yourself to me!! And this... This is my absolute cry!!! My NEED!!!
IN THE MIDST OF IT ALL, NAKUTAMANI!!!
Ni ndoa... Sio uchumba!!!
Hivi unakumbuka mwanzo mwanzo ulipokutana na huyo unayemuita mume au mke? Unakumbuka (kama umewahi ku experience) kukutana na mtu ambaye aliushika moyo wako vizuri?
Unakumbuka ilikuwaje? Unakumbuka ulijisikiaje? Ulipokutana nae? Uliweza hata kukaa muda bila kuwasiliana nae? Si ulitamani kila wakati uwe karibu nae? Usikie sauti yake? Uione sura yake? Asipokuwasilisha ugomvi unakuwa wa kwanini hajakutafuta au amekutafuta mara moja tu siku hiyo? Ugomvi flani tu usio ugomvi.
Halafu kama mlifanikiwa ku graduate kufikia kuwa ndoa basi unajua kwamba kuna namna, inaweza kuwa ni majukumu, au ndio mazoea, au muda, kuna kanamna ile hali ya kwanza sio inakufa, inapungua. Haiwi kama zamani. Na majukumu yanafanyaga hata maongezi msipokuwa makini yanageuka kuwa ni ya majukumu tu, sio kutia chachu kwenye mahusiano. Infact, wengi tukiwa tunaingia tunapewa na maonyo ya kuhakikisha hili halituharibu.
Wakati tuna juhudi kwenye mahusiano ya hapa duniani, wengi tunasahau uhusiano wa muhimu kuliko yote tuliyonayo na tutakayowahi kuwa nayo hapo duniani. Uhusiano wetu na Mungu. Wengi wetu tunau treat huu uhusiano kama uchumba, tunataka tujisikie kale ka hali, ka excitement kama kaleeee ka uchumba wa mwanzo. Unataka ujisikie hamu ya kuwa nae, hamu ya kuongea, hamu ya kuwasiliana na hata Yeye ndo akuwasilishe wewe, umringie akutafute Yeye.
Tunasahau huu uhusiano ni NDOA. Biblia inatuita kanisa ma bibi harusi wake na Ye Bwana harusi wetu. Na kwingine yeye kasemwa kama mume na sie kama wake zake. Haya mahusiano ni ndoa. Kuna juhudi zinatakiwa ili kuhakikisha kwamba hayavunjiki. Kuna majukumu yapo ndani ya haya mahusiano lakini hayatakiwi kututoa kwamba kwanza na kabla ya yote lazima mahusiano yabaki baina ya mume na mke. Focus inatakiwa kuwa Yeye na wewe. Mume na mke. Talanta ni ziada, kazi ni ziada, huduma ni ziada, vingine vyote ni ziada.
Mazoea (unaenda kanisani, unasali, unatoa sadaka, ni utaratibu wa maisha ila mawasiliano hai hakuna), majukumu-hata yanayotoka kwake (umepewa kazi, unamtumikia ndio, unapanda madhabahuni etc lakini moto haupo), kutokusamehe au hisia mbaya (kuona hakujibu, hupokei, amekupungukia etc) kusitutoe kwenye mstari, haya mahusiano ni ndoa sio uchumba. Kila wakati na tukumbuke, haijalishi unajisikia, hujisikii, haya mahusiano ni ndoa!!
Tengeneza ndoa yako!
Shalom!!
Ni ndoa... Sio uchumba!!!
Hivi unakumbuka mwanzo mwanzo ulipokutana na huyo unayemuita mume au mke? Unakumbuka (kama umewahi ku experience) kukutana na mtu ambaye aliushika moyo wako vizuri?
Unakumbuka ilikuwaje? Unakumbuka ulijisikiaje? Ulipokutana nae? Uliweza hata kukaa muda bila kuwasiliana nae? Si ulitamani kila wakati uwe karibu nae? Usikie sauti yake? Uione sura yake? Asipokuwasilisha ugomvi unakuwa wa kwanini hajakutafuta au amekutafuta mara moja tu siku hiyo? Ugomvi flani tu usio ugomvi.
Halafu kama mlifanikiwa ku graduate kufikia kuwa ndoa basi unajua kwamba kuna namna, inaweza kuwa ni majukumu, au ndio mazoea, au muda, kuna kanamna ile hali ya kwanza sio inakufa, inapungua. Haiwi kama zamani. Na majukumu yanafanyaga hata maongezi msipokuwa makini yanageuka kuwa ni ya majukumu tu, sio kutia chachu kwenye mahusiano. Infact, wengi tukiwa tunaingia tunapewa na maonyo ya kuhakikisha hili halituharibu.
Wakati tuna juhudi kwenye mahusiano ya hapa duniani, wengi tunasahau uhusiano wa muhimu kuliko yote tuliyonayo na tutakayowahi kuwa nayo hapo duniani. Uhusiano wetu na Mungu. Wengi wetu tunau treat huu uhusiano kama uchumba, tunataka tujisikie kale ka hali, ka excitement kama kaleeee ka uchumba wa mwanzo. Unataka ujisikie hamu ya kuwa nae, hamu ya kuongea, hamu ya kuwasiliana na hata Yeye ndo akuwasilishe wewe, umringie akutafute Yeye.
Tunasahau huu uhusiano ni NDOA. Biblia inatuita kanisa ma bibi harusi wake na Ye Bwana harusi wetu. Na kwingine yeye kasemwa kama mume na sie kama wake zake. Haya mahusiano ni ndoa. Kuna juhudi zinatakiwa ili kuhakikisha kwamba hayavunjiki. Kuna majukumu yapo ndani ya haya mahusiano lakini hayatakiwi kututoa kwamba kwanza na kabla ya yote lazima mahusiano yabaki baina ya mume na mke. Focus inatakiwa kuwa Yeye na wewe. Mume na mke. Talanta ni ziada, kazi ni ziada, huduma ni ziada, vingine vyote ni ziada.
Mazoea (unaenda kanisani, unasali, unatoa sadaka, ni utaratibu wa maisha ila mawasiliano hai hakuna), majukumu-hata yanayotoka kwake (umepewa kazi, unamtumikia ndio, unapanda madhabahuni etc lakini moto haupo), kutokusamehe au hisia mbaya (kuona hakujibu, hupokei, amekupungukia etc) kusitutoe kwenye mstari, haya mahusiano ni ndoa sio uchumba. Kila wakati na tukumbuke, haijalishi unajisikia, hujisikii, haya mahusiano ni ndoa!!
Tengeneza ndoa yako!
Shalom!!
Asante: Ni neno tu?
Nimekaa najikuta neno asante linanijia sana ndani ya moyo wangu. Neno dogo sana lenye maana kubwa haswa kama litabeba moyo wa yule anayelisema.
Naangalia picha ya nje ya yale yanayoendelea na kuna namna kunakuwa kama na ukungu machoni unaotaka kuzuia kuiona sababu ya kutoa neno asante, kwa kumaanisha, kutoka moyoni. Nashukuru, kwanini? Namshukuru nani?
Halafu nakumbushwa asante, inaweza kubeba nguvu la kusababisha furaha na amani ndani ya moyo wa anayejisikia kupungukiwa. Kwake yule anayeona na kudhani amefanya kidogo sana, na kwamba hakitoshi wala kustahili kuthaminiwa, neno hili linaweza kuwa uthibitisho wa kwamba kidogo chake kina thamani kubwa sana. Kidogo chake kina maana sana.
Nakumbushwa asante inabeba dhana nzima ya shukrani kwa nguvu na jasho analokuwa amelitoa mtu kwa ajili ya yule anayeshukuru. Kumbe asante inaweza kubeba shukrani kwa ajili ya damu anayoweza kuwa ameimwaga mtu kwa ajili ya mwingine. Neno dogo, pengine halina thamani ya jasho, nguvu wala ile damu, lakini linapotoka linaweza kubeba moyo unaoonyesha kuitambua thamani ya hiyo sadaka iliyotoka.
Nakumbushwa asante inaweza kubeba uthibitisho wa imani aliyonayo mtu kwa anayemshukuru. Nikiwa mdogo nilienda kwa baba yangu, nikaweka ombi langu, na anaponiambia tu ombi limefika analishughulikia, na muda mwingine bila hata kunijibu kitu, neno asante lilinitoka ikiwa kumbe ni ishara ya uhakika nilionao kwake kwamba atanisaidia kwenye ile shida yangu.
Vile vile ninakumbushwa kwamba Yesu aliwasafisha wakoma kumi, katika hao, mmoja tu ndio alirudi na kushukuru tena kabla hata hajakamilisha maelekezo ya kwenda kuonana na kuhani ili kuuthibitisha uponaji wake. Na aliporudi Yesu alimwambia amekuwa mzima kwa kule kurudi kwake, ingawa wenzake walisafishwa tu. Inamaanisha nini? Kuna ukamilifu, utimilifu, uzima ulio kwenye shukrani. Kwenye kusema asante. Ni neno linaloweza kuweka muhuri kwenye kile kilichoanza kama kusafishwa tu, kikawa uzima kwenye mwili wote.
Baada ya kukumbushwa yote haya nimeelewa. Naelewa sasa kwanini asante imekaa moyoni mwangu. Kwanini ingawa nje hapafananii, ndani yangu panalia panaiita asante... na kwahiyo basi nimekaa hapa najikuta nasema asante. Asante kwa kila tulilopitia, asante kwa hapa tulipo, asante kwa tunapoelekea.
Asante Roho Mtakatifu.
Asante Yesu wangu!
Asante Mungu, Baba Yangu uliye mbinguni.
Influencers-ushawishi tunaohitaji?
Hii ni jamii nyingine kabisaa. Ni aina mpya ya maisha ambayo yamezaliwa kutokana na mitandao. Kila mtu, kila mahali anajua kitu na anajaribu kuwa 'influencer' kwenye hiko. Huyu kwa kishwahili ni mshawishi. Hakuna lugha nyepesi nyingine ya kumuita.
Mshawishi inatokana na ushawishi, unaotafsiriwa kama uwezo wa kuathiri tabia ya wengine kwa mwelekeo flani, kwa kutumia mbinu zinazoweza kuvuta hisia za watu wengine. Ndio maana ukiingia mtandaoni unaona kabisa kurasa unazoletewa ni za wale ambao wana vitu vinavyoendana na wewe. Lengo ni USHAWISHI. Uvutwe. Kuna wanaovuta ununue, kuna wanaotaka kuvuta uache, na kuna wanaovuta uingie au ufanye. Kivyovyote vile lakini lengo ni kubadili tabia yako.
Hii zana sio mbaayaaa... lakini kuna namna pia sio nzuuriii. Kuna namna. Na hii ni kutokana na sisi binadamu tulivyoumbwa. Binadamu ni roho, mwenye nafsi, anayeishi katika mwili. Mwili ikiwa ndio tunachokiona duniani, roho ikiwa ndio mtu mwenyewe na nafsi ikiwa ndio uwanja wa kupambanua mambo ambao mtu anautumia, huku ikijalisha anapambanua mambo kiroho au kimwili. Nafsi ndio inayokupa wewe maamuzi kutokana na kile kimetokea ili uweze kufanya yanayotakiwa sasa. Najua nimeongea maneno mengi sana, ila pia najua utanielewa.
Biblia yangu inanifundisha kuulinda sana moyo wangu sababu ndio chem chem za uzima zinapotoka. Pale pale Paulo anapomwandikia mwanae Timotheo anamwambia atunze nafsi yake na mafundisho yake maana ndio namna atajiokoa nafsi yake yeye na wanaomsikia. Ni kama vile hili ni neno la kutunza moyo (soul, nafsi) limejirudia rudia kutokana na msisitizo tunataka wekewa..ila tunatakiwa pia kuangalia ni nani anayeweka msisitizo huo? Aliyekuumba! Ambaye hawezi kusema tu sababu alijisikia kusema, lazima kuna sababu ya kusema kwake.
Kama haitoshi, biblia inasema:
Rum 12:2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Ukiisoma hii, inataka tusifuatishe namna za dunia hii ili tupate kujua mapenzi yake na ule ukamilifu KWA KUGEUZWA KWA KUFANYWA UPYA NIA ZETU. Kugeuzwa kunawezekana kwa kufanywa upya nia zetu, na hiki kinatokea tunapoacha kufuatisha namna za dunia hii, ambacho kinaanza kutujuza mapenzi ya Mungu ambayo ndo tunaishi humo kuupata ukamilifu. Ni series sio movie. Kimoja kinazaa mengine. Na iko clear, namna za dunia hii hazitupi kujua mapenzi yake wala ukamilifu, na kugeuzwa hakupo bila kuacha namna za dunia hii. Na yote yanafanyika kwenye nafsi. Mahala nia na maamuzi yanakaa. Hatuwezi pia jua mapenzi ya Mungu bila kumsikiliza, kujua neno lake linasemaje, Yeye anasemaje?
Hapa ndio vita ilipo. Adui hajapambana kuhakikisha tu hupati mda, hamu wala msukumo wa kusoma neno na kumjua Mungu kwa namna hiyo, anapambana kutujaza na ujuzi nyingine nyingiii kinyume na mapenzi ya Mungu, ili sasa hata unapopata neema ya kusoma, ugomv kati ya unachodhani unakijua, na kweli ya Mungu unakuwa mkubwa sana na iwe rahisi kukushinda vita. Na moja ya mbinu inatumika, haswa kwa sisi wa kipindi hiki ni huu ushawishi wa mitandaoni.
Swali la kujiuliza sasa, kwanini waitwe influencers? Lengo ni kukubadili tabia, na tabia ni mazoea, matokeo ya kilee kimekujaza nafsini mwako, matokeo ya maamuzi yako ya mara kwa mara, ambayo hayawezi kuwepo isipo kuna kitu unakijua, umekikubali, umekichukua. Lengo ni kukushawishi, lakini je? Wanashawishi kitu gani? Unashawishiwa kuelekea wapi?
Sio kwamba kila influencer ni mbaya. Ila sasa inabidi kukumbuka kunaye mfalme wa ulimwengu huu ambaye lengo lake ni kuwapoteza watu na kuwaweka mbali na Mungu. Maana yake ni lazima 'wateule kuwa macho' huwezi ku follow kila kitu, kusikiliza kila kitu, kufuata kila kitu, sababu huwezi jua nini kiko nyuma yao. Na zaidi utashawishika na kila kitu. Macho yawe wazi kujua huyu mshawishi anataka kunipeleka wapi? Ni salama kwangu?
Wakati unafollow influencer, mshawishi, follow, sikiliza lakini kumbuka, wao ni WASHAWISHI, angalia usije shawishika nao kinyume na ushawishi wa Roho Mtakatifu ndani yako.
Shalom!
2 Sam 1:14-16 SUV
[14] Daudi akamwambia, Jinsi gani hukuogopa kuunyosha mkono wako umwangamize masihi wa BWANA? [15] Ndipo Daudi akamwita mmoja wa vijana, akamwambia, Mwendee, ukamwangukie. Basi akampiga hata akafa. [16] Daudi akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi wa BWANA.
Karibu tutafakari
Jana tuliona Sauli alikufa kwa kujiua ili asije akauliwa na Wafilisti. Lakini leo kijana anaenda kwa Daudi anamwambia ni yeye ndio alimuua Sauli kwa huruma na kwamba alimwomba so akaona amsaidie asije akauliwa na wafilisti, itakuwa mbaya. Poor him.. Wakati anadhani anachosema kitampa kibali mbele za Daudi kwa namana alimpenda baba yake. Daudi anamuua kwa kumuua masihi wa Bwana. Sasa maneno anayosema baada ya oda ya kumuua ndio yamenitafakarisha hapa leo
Damu yake na iwe juu yake maana alijishuhudia nafsi yake kwamba amemuua Sauli. Sababu Daudi alimuua na tunajua kabisa kwamba mshkaji hakumuua Sauli, hatia obviously inakuwa ya damu isiyo na hatia sio? Ila mfalme anatangaza hatia kwa kule kujisemea kwamba amemuua masihi wa Bwana. Nimeshangaa. Uhai wake kwa uhai anaosema ameutoa wa masihi wa Bwana.
Vinashtua. Ye alifanya kupata sifa tu, ila kwa hili neno na adhabu inayompata ni kwamba anajikuta kwa hii sifa anapata ujira wa kama aliyefanya. Mweeeh. Just nguvu ya ulimi. Kwamba unaweza kukutwisha hatia ya jambo hata hujalifanya au? Nawaza hivi huyu angeongea tu ukweli ilivyokuwa ingekuwaje? Tuwaze hapa now. Shalom!
Unaona nini? What do you see?
1 Sam 31:7 SUV
[7] Kisha watu wa Israeli waliokuwa upande wa pili wa bonde lile, na ng’ambo ya Yordani, walipoona ya kuwa watu wa Israeli wamekimbia, na ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia; nao Wafilisti wakaenda wakakaa humo.
Nimesoma hii sura mara nyingi sana ila hili eneo likanisumbua sanaaa. Kwamba hawa hawa majamaa walioingia kwa vita kushika maeneo wanakimbiaje wanayaacha hapo bila hata kuyapigania jamani?
Hivi unajua ni wameandika wakakimbia, wafilisti wakaenda wakakaa zao kiulainii. Imenisumbua kweli kweli.
Kwahiyo nikaendelea kusoma na kusoma mpaka nilipoona why hawa waliondoka. Biblia inasema shida waliyokuwa nayo. WALIONA. Waliona majeshi yao yakikimbia wafilisti, wakaona watoto wa Sauli wanakufa, wakaona Sauli anakufa.. Wakaogopa, wakaondoka na mwisho wakaja wafilisti kiulainii. Issue yao ilikuwa kuona. Which means wasingeona wasingeondoka si ndio?
Now kuona pengine isingekuwa issue kwa wengine, ingeweza kuwa namna wanapata tu kujua kinachoendelea ili waweze jipanga ila kwa hawa sasa kile wanachokiona kinawakimbiza.
Now hatujui mpango kama ulikuwa kuvuka kuja kukaa au wamemfuata Sauli tu, lakini wanapoona utupu wa nchi, wafilisti wanakaa. Imagine!
Kwamba unaweza umejiingiza kwenye utumwa kwa sababu ya madhara ya kuona. Kuna vitu vingi sana watu wanajikuta wamejiingiza humo au wameharibikiwa na kufanya maamuzi ya haraka sababu ya KUONA, anachoona kinazidi sauti ya kile anachosikia ndani, so anaamua. Anaharibikiwa. Kwa kifupi yaani tunakumbushwa tu, hakikisha unachokazana kukiangalia hiko unakiweza kweli sio kikuweze. Shalom!