Stories by Amanzi Salum on Medium
Duniani kote kwa ujumla vijana ni kundi kubwa lenye idadi kubwa ya watu kuliko makundi mengine kama wazee na watoto,kundi hili la vijana hata kwenye Nchi yetu Tanzania ni kundi ambalo linaongoza kwa kuwa kubwa na lenye watu wengi sana,Hivyo basi kwa kuliona hilo serikali ikaandaa wizara maalumu ambayo itakuwa ikishughulika na changamoto za vijana na kuunda mikakati ya kuwaendeleza vyema.Hatua hizo ikiwa ni kuwainua vijana kiuchumi na kifkra na taaluma kwenye shughuli zao za kila siku,kutokana na ripoti za Shirika la Kimataifa la Kazi Duniani(ILO) dunia imeshuhudia changamoto kubwa ya Ukosefu wa Ajira na huenda changamoto hiyo ikaendelea kukua zaidi kutokana na Mabadiliko na maendeleo ya kiteknologia tuliyonayo.
Vijana wakiwa bado ni kundi lenye nguvu kubwa kwenye jamii zetu zinazotunzunguka lakini pia wameendelea kuwa mzigo mkubwa ambao anatafutwa wa kulaumiwa au sehemu ya kuutua mzigo huo ni wapi hasa ,vijana wanaendelea kuonekana ni wengi kwa idadi kama ripoti ya shirika la idadi ya watu duniani(UNFPA) zinavyoonesha za vijana ni karibu asilimia 80 idadi ya watu wote duniani.lakini bado haijakuwa kigezo na sababu ya kutufikisha kwenye maendeleo na mabadiliko tunayoyataka na kuota kila siku huku tukiendelea kujipa imani kuwa vijana ni nguvu kazi ya Taifa na tegemeo kwenye maendeleo ya sayansi na teknologia ya leo.
Kuna Usemi wa Kiswahili unasema “Samaki mkunje ingali mbichi,akiiva au kukauka hakunjiki”,Vijana wanaitaji kupata mabadiliko ya namna ya kufikili na maono ya kuwa dunia imebadilika na inaitaji watu wenye kukimbia kama Usain Bolt kwenye kuyaendea maendeleo na sio kukaa na kuamini kuwa kuna atakayefanya na maendeleo yatakufikia kama unavyoitaji,Uzuri wa dunia ya kwetu leo hii imebadilika kwa hatua kubwa sana toka mwaka hule wa Y2K (2000) ambapo wakina Kibwetere na wenzake kule Uganda aliwaaminisha wafuasi wake kuwa ni mwisho wa Dunia na wao wakaamini hii Dunia hii ,Na mimi naamini leo dunia hile imekwisha sasa dunia nyengine yenye kuogopwa kwa vitu viwili Teknologia na Mungu imezaliwa Upya,kwenye huu ulimwengu wa sasa dhamira yako na kipaji kinaweza kukuongoza na kukufikisha popote unapotaka kufika kikubwa ikiwa umeamua kwa dhati na kuchukulia hatua zako na harakati zako za mbio zinazokwenda kama Usain Bolt na kwenye Umakini Mkubwa wa Kufuta Umasikini na Kufikia Maendeleo Endelevu.
(Pichani: Kundi la vijana kwenye picha ya pamoja Kongamano la Vijana kusini kwa Bara la Afrika lilofanyika Tanzania ilioandaliwa na Mulika Tanzania)
Vipindi vya radio na television vimefanya mabadiliko makubwa kwenye kuangazia mabadiliko ya kiuchumi kwa vijana yanafanyika na kusahau kabisa dhana ya kusema hakuna ajira kwenye masikio yetu,vipindi vyenye kuonesha ubunifu na miradi ya kijamii yenye Marengo kuwainua vijana kufikia maendeleo yamekuwa yakifanyika kwa kasi kubwa mfano mradi wa ubunifu wa Afya ya Uzazi Amua ambayo ulisimamiwa na shirika la Sahara na Mulika Tanzania ambao wakurugenzi wa mashirika hayo ni vijana wa ambao wadogo kabisa Bwana Hussein Melele na Jumanne Mtambalike hawajafikia hata miaka 35. Katika dhana ya kutumia teknologia kama sehemu ya kujiburudisha na kujirudisha nyuma kwa sasa nadhani imepitwa na wakati na inapaswa kubadilishwa kwenye mitizamo hiyo badala ya wakati wote kuangalia instagram na Twiiter basi alau upate muda kidogo kwa siku kuyafanyia kazi yale ambayo umeona kwenye mitandao ya kijamii, lakini pia wakati wa kukaa kwenye vijiwe bila shughuli wakati huo huo vijana wengine wakifanya mabadiliko ya kimaendeleo na ubunifu kwenye vituo kama kile cha Tume ya Sayansi pale BUNI nadhani umefika wakati wa kuamua na kutekeleza kwa Sababu mifano na watu wakutuongoza kwa dhati wapo kwenye jamii zetu.
Huku tukiwa tunawaita Watu wa Makamo wakiendelea kufikilia kwa ajiri yetu vijana wa leo mtu kama Bw.Joseph Kusaga akianzisha harakati tofauti za kutafuta mawazo bora ya CEO vijana Tanzania,Vijana tumeendelea kusikia na kuachia watu wachache wakishiriki na kupokea Medali na pesa za mitaji kuendeleza biashara zao sisi wengine tukipuuzia na tucheka kwa story nyingi vijiweni za demu huyu mara demu Yule na ikifika mida ya msosi kukimbilia nyumbani kufungua hotpot la chakula.
Vijana wanaendele kuzeeka kwa fikra kwa kukosekana mawazo Bunifu yenye tija ambayo yanaweza kuchagiza Serikali yetu kuwaza zaidi ni kwa namna gani wanaweza kuwasaidia vijana kutimiza hadhima zao, hili linanipelekea hata wakati mwengine nachelea kufikiri kushauri serikali yetu ifute kabisa wizara ya vijana kwa maana tunachokitaka hatukioni kutoka kwa vijana wenyewe, Mawazo na mitizamo ya kimabadiliko imebaki kuwa mijadala inayojadiliwa kila leo kwenye makongamano kama vile ya fursa na mengineyo na sio mtaji kwa kufanya na kutekeleza yanatakikana.
Pichani:Siku ya Ubunifu ambayo ilikutananisha vijana wa Afrika wenye mawazo Bunifu(Sahara Sparks),Kushoto ni Amanzi(muandishi),Jumanne Mtambalike(Mkurugenzi wa Sahara Venture Company),Hussein Melele (Mkurugenzi wa Mulika Tz) na Innocent Mkota (Meneja Miradi Mulika Tz)
Uzee wetu vijana wa kimawazo unapekelea hata wakati mwengine wanapokuwa wazee wamekaa pamoja kwenye vikao vyao vya kupanga maendeleo yetu na kuitaji mawazo ya kijana wasione umuhimu wetu na kusema hakuna haja ya kumleta kijana hapa, hivyo basi ndo maana muandishi aliposema Tanzania kuna uhaba wa vijana wenye fikra tunduhizi zenye malengo na mabadiliko chanya kwenye jamii na kutuletea maendeleo na sio vijana wa ndio mzee na nimesikia,Tuachane na dhana ya Watu wa makamo kufikiria badala yetu sisi wakati sisi wenyewe vijana tukiendelea kuwepo na Kutoshughulika na fursa zilizopo, waunaweza hata ukasikia kauli kutoka kwa vijana wenyewe kwenye vinywa vyao “Hakuna Kazi ndo maana hatufanyi kazi,ikiwepo tutafanya”. Makampuni mengi ya hivi sasa yanatafuta vijana wenye maono na mitazamo ya kubadilisha mifumo iliyoko enzi ya Y2K kuja enzi ya kizazi kipya lakini vijana hao bado wamekuwa wachache na wakati mwengine unaweza kusema hakuna Kabisa.
Sekta mpya nyingi zinaendelea kukua ambazo zinaitaji Vijana wenye Utimamu wa Akili na Kimitazamo kama sekta ya Sanaa na Burudani ,Sekta ya Viwanda na Ubunifu ,Sekta ya Mazingira na Udhibiti na hata sekta ya Habari ambayo kila uchao imekuwa ikibadilika na kuitaji waandishi huru ambao hawafungamani na soko moja la Ajira.
Nyakati hizi uwenda vijana waliohitajika sio hawa vijana waliokuwepo leo uwenda nyakati hizi ziliitaji vijana wakina Bill Gates na wengine ambao kwa sasa ni wazee kabisa,Kuchukua hatua hakutoshi kwa kusikiliza mijadala na kuingia kwenye makongamano na kuchangia mada tu ila kunaitaji utashi wa kushiriki na kufanya kweli kama vijana wenzetu kule Mkoa wa Simiyu walioanzisha kiwanda cha Chaki au wale pale keko walioanzisha makampuni na viwanda vya Useremala.
Pongezi kwa vijana wote wanafanya mabadiliko na maendeleo kwenye sekta tofauti Tanzania wakiendelea kuonesha uwezo wao mkubwa wa kufikilia na kutekeleza mambo mbalimbali.Tupunguze Mijadala isiyo na tija na maana kwetu badala kukaa na kujadili siku nzima Siasa kwenye mitandao ya kijamii basi badala yake tushiriki kugombea na kuhamasisha maendeleo kwenye jamii zetu,lakini pia badala ya kula bata na kutoka na marafiki kila siku basi angalau tuanzishe miradi yenye tija ambayo inaweza kuongeza ajira kwa vijana wenzetu kwenye mtaji mdogo kabisa unaotumia pesa kila siku kupigia maji,lakini pia badala kufanya matumizi yasiyo ya lazima kwa namna yoyote ile basi tuanze kutazamia kuwekeza kwa maono ya hali ya juu kabisa, leo hii tunaitaji kuwa na wakina Mo zaidi ya Mmoja ,lakini tunaitaji kuwa na makampuni kama Sahara Venture ,Mulika Tanzania, Clouds Media Groups ,Wasafi Label ,Konde Boy Label na zenginezo nyingi zaidi zikiwa kwenye mikono ya vijana.
Miongoni mwa mashirika kumi na tano yaliyoungana kwa pamoja kwaajili ya kutoa maoni ya muswada wa sheria lilikuwepo shirika moja tu lililokuwa likiwakilisha mchango wa vijana ,wanawake na watu wenye ulemavu michango na maoni yao yanafikiwa kwa ufanisi Zaidi kwenye muswada wa sheria wa vyama vyama vya siasa nalo ni Mulika Tanzania ambalo ni shirika linaloendeshwa na vijana wa Kitanzania lenye dhumuni la kuchochea maendeleo ya jamii na kuwezesha ushiriki wa vijana katika masuala ya kijamii.Shirika hili limekuwa linafanya kazi kwa karibu sana na vijana na limejikita hasa katika maeneo muhimu matatu ambayo ni elimu ya uraia na ushiriki kimaendeleo, kazi na maisha bora, na elimu ya haki za binadamu.Lakini pia ni moja ya Shirika lililoshiriki kwenye kutoa maoni ya muswada wa vyama vya siasa.
Zikiwa tayari zimepita takribani wiki mbili sasa tangia kukamilika kwa kamati ya Bunge ya Katiba na sheria kukamillisha kazi yake kuyapitia na kuyachambua maoni ya wananchi na wadau kuhusu muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya siasa.Tasisi na asaki za kiraia zilikutana Mjini Dodoma Kwa Zaidi ya wiki moja kupitia na kuja na mapendekezo kwenye muswada huo mbao unawenda kuwalenga vyama vya siasa na Watanzania wote kwa ujumla.Asasi hizo ni kama vile Mulika Tanzania,Tanlap ,Tamwa,Thrds, Wildaf ,DignityKwanza,Lejf ,CRC,Seka Associate Advocates, Tawla ,Tifld na Envirocare zilitazama muswada huu kwenye jicho ndani Zaidi kwa makundi ya kijamii kama vile vijana na wanawake . Maeneo makuu ambayo yalipitiwa na kutolewa maoni ni kama yafutayo,
Swala la Msajili kuomba taarifa kutoka kwenye Chama ,muswada umeligusia hili kwenye ibara ya 5B ulimpa madaraka ya msajili kuomba taarifa yoyote kutoka kwa mtu yoyote kwenye chama ,iwe kiongozi au mwanachama tu wa kawaida na kama mtu huyo angeshindwa kufanya hivyo,angekabiliwa na adhabu na faini ya shilingi za kitanzia milioni moja hadi tatu na kifungo cha meizi mitatu hadi sita au vyote kwa pamoja.Kamati zilipendekeza kuondolewa kwa Madaraka hayo kwa msajili wa vyama vya siasa na imeridhia kuwepo kwa adhabu moja wapo kifungo au faini na sio vyote kwa pamoja.
Lakini Pia Kamati ya mtandao wa Asaki za kiraia ulitoa mapendekezo ya kumfutia au kumuondolea madaraka kifungu kinachompatia msajili mamlaka ya kusimamisha au kufuta chama kwa sababu ya kutopeleka taarifa kwa msajili.
Kinga ya Msajili wa vyama vya siasa kupitia kwenye Ibara ya 6 ya Muswada ulipendekeza kinga ya msajili ,naibu msajili na maaafisa wake kutoshitakiwa Mahakamani kwa lolote walilolifanya au kuacha kulifanya kwa nia njema. Kama ya imependekeza na serikali imeridhia kufutwa kwa kifungu hicho ili kibaki kama ilivyokuwa katika sheria ya vyama vya siasa .
Kuhusu Tunu ya Taifa za kuzingatiwa na vyama vya siasa Muswada kupitia kifungu cha 6A (5) kinachoanzishwa kwa ibara ya 7B ya muswada ulipendekeza vyama kuzingatia muungano wa Tanganyika na Zanznibar ,Mapinduzi ya Zanznibar ,Demokrasia ,Utawala Bora ,Kupinga rushwa ,maadili ,uzalendo ,mwenge wa uhuru na amani na utulivu kwenye utungaji wa sera ,uteuzi na uchaguzi wa viongozi Kamati zilipendekeza kuwepo kwa usawa wa kijinsia,Ushiriki wa watu wenye Ulemavu na kuwepo kwa vijana na ujumuishi wa jamii kama tunu ya kuzingatiwa na vyama.
Vyama vya Siasa na Harakati,Muswada kupitia kifungu cha 6 (A) (6) kinachoanzishwa na Ibara ya 7 ya muswada vyama vya siasa vilizuiwa kuwa kama vikundi vya kiharakati au vya msukumo, kamati imependekeza na serikali imelidhia kufutwa kwa kifungu hicho.
Muwakilishi wa Shirika la Umoja wa Maitafa la Vijana Tanzania ya vijana Bwana Johnbest Mwahaja “MSAJILI wa vyama vya siasa amepewa mamalaka makubwa sana au amepewa lungu kubwa kiasi kwamba hata kuvunja na kikuka baadhi ya vifungu vya katiba yetu,lakini pia tunaweza kutumia mitandao ya kijamii kama vile platform ya twiiter tunaweza kupitisha maoni yetu na mawazo yetu na hata mimi binafsi Napata taarifa nyingi kupitia huko”.Vijana,watu wenye ulemavu na wanawake ni makkundi ambayo yanapaswa kupewa matazamo wa kipekee kwenye kila hatua inayogusa mstakabari wa Nchi na taifa kwa ujumla kwani ni wengi na hawashirikishi kwenye kusemea matatizo yao na changamoto zao,Ni vyema sana kwa safari hii makundi haya yalivyoshirikiswa kwa kupitia Tasisi zao.
Wakati dunia inakili kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii kukuwa kwa haraka na kasi iliyotukuka,watu wote duniani katika malika na umri tofauti waidhinisha kuwa maisha yao na nyakati zao kuzitumia zaidi kwenye mitandao ya kijamii na sio shughuli nyinginezo,maisha ya wanachi mmoja moja yanathiriwa na nyakati ya teknologia na mabadiliko haya pengine yanataka kutupeleka kwenye hatua nzuri na njia ya mafanikio kwa watu wote.
Tabaka la vijana ni mdau wa kwanza kuathiriwa na upepo wenye dhoruba zito la tehama kwenye kurasa za kijamii,tafiti iliyofanyika huko ughaibuni kwenye chuo kikuu cha karifonia imethibiti kuwa vijana hupoteza muda wao zaidi kwenye kurasa za kijamii kwa ajili ya kuwasiliana na marafiki na kutoa mawazo yao yasiyo na mantiki kwa jamii zao husika wakati mwengine,vijana wanapaswa kuendana na tehama kwa kuwa wepesi kusoma na kuongeza ujuzi wao kwa kupitia mitandao ya kijamii na sio kupoteza muda kwa mambo yasiyofaa katika jamii.
Umri wa kijana ni tunu ambayo inapaswa kulipiwa kwa namna yoyote ile lazima utailipa tu kwa wakati wowote ambao utakuwepo duniani,midhali upo hai na mzima wa afya. Vijana wamekuwa wakitumika na walengwa tofauti duniani ambao wenye madhala mmoja kwa mmoja kwao au tabaka lolote kwenye jamii zao,kutokana kuwa na uwezo mzuri katika uchambuzi na kutoa maoni vijana wa namna hii wamekuwa wakitumika na wanasiasa na watu wa magharibi kwa ajili ya kuleta uchochezi na vulugu katika jamii zao hili tu malengo yao yakamilike.Unakuta kijana mwenye tahaluma na uwezo wa hali ya juu kutokana na kutoelewa au kuangalia jambo kwa jicho pevu wamejikuta mstari wa mbele kwenye uchochezi na kuondisha amani kwenye mataifa yao.
Maisha yetu yana deni na deni la ubaya na kufanya jambo lisilofaa malipo yake ni hasala na upotefu wa uhai wa ndugu na jamaa zetu wenyewe,vijana wamekuwa wakilalamika matatizo yao kwenye mitandao ya kijamii badala ya kutumia njia ya mitandao ya kijamii kama njia ya kufanikiwa na kutoa ufumbuzi wa changamoto zao balada yake imekuwa zahama na matanga yasiyokwisha na vilio vya muda mrefu sasa.Kurasa za kijamii ni njia bora zaidi kwa vijana wanaofanya shughuli tofauti kutangaza mambo yao na kujitengenea nafasi ya kuona mafanikio.
Ukurasa za kijamii zilianzishwa kwa malengo na dhamila tofauti dhamila hizo zikiwa nzuri kwa namna ya kurahisisha na kutengeneza njia njia nzuri ya mawasiliano baina yetu yani kufanya dunia kuwa kijiji kimoja,hapa watu wamagharibi wamefanikiwa kwani leo aliyekuwa bara la asia anaongea na bara la afrika kama kwamba mtu na jirani yake walichangia ukuta mmoja wa nyumba,lakini pia kurasa hizi zimetufanya kurahisisha shughuli za masoko na ufanyaji biashara baina yetu na kutufanya kufanya biashara zetu kwa urahisi na kutuwekea masoko ya uwakika,pamoja na mafanikio mengine mengi zaidi ya kupata taarifa na uhuru wa kupeana habari kwa wepesi na muda mfupi.
Jamii ya kizazi kipya chenye mafanikio ya kuona dunia yenye kasi na mwendo usiokifani,sasa basi kufatia matumizi na umiliki wa kurasa hizi kulikofurutu Ada,sheria mpya zimeundwa kulinda haki za mitandao na tehama kwa ujumla na kuweka taratibu nzuri za matumizi ya kurasa za kijamii bila kuvunja maadili na miiko ya tamaduni zetu hata hivyo pia haijaishia hapo kulinda amani na tunu ya maisha bora na yenye afya baina yetu ndo maana sheria hizi zipo na zitaendelea kuundwa kwa masirahi ya mataifa yetu bila kuogopa wala kuhofia vile vigelegele vya watu wasiojua umuhimu wa maisha ya amani na furaha,kwenye taifa lolote lile kunakuwa na adau aidha wa ndani au nje ya taifa hilo wakati mwengine adui huyu huwa adui hata bila kujijua,lazima tujikinge na kujiadhali na madui wa taifa letu.
Fikra na hekima za wakoloni naanza kuziona na kusikia pia kuhisi harufu yao inaludi kwenye ngozi ya mtu mweusi,si kwa kutushikia mtutu au kuja na kioo na kubadilishana na dhahabu na almasi bali kwa kutusihi na kutuamlisha kwa maandishi akidai haki na uhuru,eti mkoloni leo nae anadai tupate uhuru na anataka karamu yetu iandike kila linaloonekana kwenye bara letu kila baya na mazuri machache tuishie kuyajua wenyewe hataki kusikia mazuri tukitangaza kwenye kizazi chake,huyu kweli ndo mkoloni mwenye rangi nyeupe na nywele zenye kalikiti.
Hata wenye elimu ya tasnia hii habari tunawaita wanadhuoni wasisitiza kuruhusiwa karamu zetu kumwaga wino na kusema na kusemea jamii yenye sauti ambayo haisikiki,lakini nani atachukua kipaza sauti hiki na kusemea haya kama kila amwagae wino na maandishi haya tunayazuia kwa kutumia kigezo kuwa wanatishia uhuru wetu,tuache waandike waandike kile wanachokiona lakini cha msingi na maana wasije kuvunja furaha na tabasamu letu na kutupeleka kwenye vilio na simanzi za kila mara.
Majuma machache yaliyopita mkuu mwenye sauti alitishia karamu mbili zenye wino na kuziambia ziwe butu haraka kama zikiendelea kumwaga wino na kumaliza karatasi kwa maandishi hayo basi atawekwa kwenye kizuizini,lakini si mara ya kwanza kwa wakuu kusema na kutamka haya wakaweza hata kutunga sheria kali na kuweza mazingira ya kila mwenye karamu hasitumie karamu yake kwa misingi ya vitisho na ulagai.
Mi namkumbuka sana yule halisi na yule tanza wote hawa walitumia karamu vizuri badala yake wakuu walisema kuwa hawatufai na wanatishia furaha na tabasamu wakazuiwa hata pia yule nchi nae,makala na tahariri zao zilitufunza na kutufanya wakati mwengine tuone madhaifu ya watawala hii ni nzuri na inatija kwa vijana wetu wawe wazalendo na wenye kupenda nchi,masirahi ya nchi yetu mbele na kisha masirahi ya mtu mmoja mmoja.
Kauri,hekima,busara na heshima hii ndio siha ya viongozi wa kitanzania kuwafaliji na kuwajali watanzania wote kwenye nyakati zote hao ndio viongozi bora na tunawakumbuka kila siku ya maisha yetu watanzania,uwoga na kufanya kazi kwa hofu,migomo na kukosa uwadilifu huu sio uwongozi au kiongozi wa kitanzania,matarajio ya mabadiliko ya kiuchumi wa tanzania unaendana sambamba na utawala bora na kusikilizwa kwa wananchi,mabadiliko yasiyo na utawala bora ni sawa na kishada bila muongozaji.
Tusivae miwani meusi nyakati zetu hazituruhu bado tupo kizani panaitaji taa zenye mwanga mkali zaidi na kukemea kila jambo baya na kuzuia mabaya na kuhamasisha utekelezaji wenye tija kwa wananchi,basi nakwambia karamu butu zimekuwa hazifai tena makazi yake kwenye jalala na huko zitachomwa moto kwa unafiki ulitukuka kutudanganya watanzania hata baya kulisifia na kubadili fikra zetu kwa kutumia vyombo vyao pale linapotokea jambo ambalo tunapaswa kujadili kwa pamoja wao buti wamekuwa wa kwanza kutubadili,masikio yetu yamekuwa hayasikii hata macho yetu hayaoni tena kwa baya yanayotekea kwenye jamii zetu sababu kuu ni uhuru wa maandishi na karamu zilizo butu.
Achane karamu ziandike kama kweli nyie ni wasafi na watenda haki,achaneni tunoe karamu zetu na tujaze wino wa kutosha,maandishi yawe mazuri na yenye kuvutia kama mtatekeleza yenye kwa wakati na kwa haki,maandishi haya hayabadili fikra zetu kama ni uwongo lakini maandishi haya yatatukasilisha na kutuchukiza na kuamsha hasira zetu mapema sana kweli mnayotenda na mnayofanya hayana tija kwetu na kutupeleka kwenye maisha magumu na yenye hasira na kukosa furaha kama zamani.