Stories by @IsaacGaitano on Medium
Kichwa cha habari cha makala haya ni nukuu ya mwanazuoni na mwanaharakati wa Kibrazili, Paulo Freire, kutoka kwenye kitabu chake mashuhuri na ambacho kimeendelea kuchochea mijadala mikali katika sekta ya elimu ulimwenguni kote, Pedagogy of the Oppressed.
Hiki ni kitabu cha kipekee na maridhawa katika nyanja za elimu, uchambuzi yakinifu wa masuala ya kijamii na fikira tunduizi. Freire, aliyezaliwa mwaka 1921 na kufariki mwaka 1997, alikuwa mwanaharakati, mdau wa elimu na mwanafalsafa.
Maudhui na muktadha wa kitabu ni matokeo ya mazingira magumu ya udikteta yaliyoikumba Brazili kwenye miaka ya 1960, ambapo nchi hiyo ilinuka umasikini wa kupindukia na ukandamizaji wa haki ulirasmishwa. Mambo hayo yalisababisha Freire apelekwe uhamishoni nchini Chile.
Kitabu hiki ni maarufu na kimetafsiriwa katika lugha zaidi ya ishirini na tano. Kwa ujumla, kinapinga sera na miundombinu ya elimu duni zilizopitwa na wakati, zinaendeleza unyonyaji na matabaka na kuwadumaza wananchi. Sera hizo zimeshindwa kuwajengea uwezo na kuwashirikisha wananchi katika kuboresha maisha yao na kuwafanya wajisikie fahari na nchi yao.
Freire anasema kuwa mfumo na sera ya elimu sio neutral, au zisizoegemea upande wowote. Badala yake, zote ni matokeo ya utashi wa kisiasa ambao aidha unamkomboa mwananchi, au kumfanya mtumwa katika nchi yake.
SOMA ZAIDI: Jitihada Zaidi Zinahitajika Kuongeza Ubora wa Elimu Inayotolewa Tanzania
Tafsiri yake ni kwamba, elimu duni imetolewa kama chombo cha tabaka tawala kubaki madarakani na kuendeleza unyonyaji hasa katika kutuamulia aina ya elimu na sera zake. Kwa upeo wa mwandishi, mageuzi na harakati zote za kuleta utawala bora, haki jamii na demokrasia, na katiba mpya haziwezi kutenganishwa na vuguvugu za kielimu, yaani ukombozi wa fikira na uhuru kamili.
Muktadha wetu
Kitabu hiki ni muhimu sana kwa mazingira yetu sasa, ambapo uhuru wa kujieleza, mawazo mbadala, na haki ya kukusanyika zinapingwa na udikteta wa dola unashamiri. Mwandishi Paulo Freire anatoa mwongozo kwa kufuata pale ambapo tunaona hakuna utashi wa kisiasa katika kuleta mabadiliko.
Mabadiliko anayoyagusa mwandishi ni katiba mpya, kuongezeka kwa matabaka kati ya walalahoi na walalaheri, na kushuka kwa ubora wa elimu. Mwandishi anapingana na mfumo baguzi wa elimu ambao unaacha vijana wengi nyuma bila kuwapatia ujuzi mbadala, unaochochea ukosefu wa ajira, na kusababisha kuongezeka kwa ugumu wa maisha na umaskini ambao ni mtaji wa kisiasa.
Kitabu kinabainisha kuwa aina ya elimu na mtindo wa ufundishaji, anaoufananisha na mfumo wa kibenki, ambapo walimu “huweka” ujuzi na maarifa kwa wanafunzi, ni mtindo wa kikoloni, ambapo mwalimu pekee anaonekana ndiye mwenye ujuzi na maarifa yote na wanafunzi ni wapokeaji tu wa taarifa, wanakariri tu. Hivyo sio washiriki kamili wa mchakato wa elimu.
Mtindo wa elimu kama huo ulipingwa pia na Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania, alipoongea juu ya sera ya elimu ya kujitegemea, ndiyo maana Paulo Freire na Mwalimu Nyerere walikuwa marafiki hadi kutembeleana miaka ya 1971.
SOMA ZAIDI: Kwa Kung’ang’ania Kiingereza, Rasimu ya Sera ya Elimu Imeshindwa Kuzingatia Maslahi ya Wengi
Kwa mujibu wa Freire, elimu hii haiwezi kumkomboa mnyonge na maskini. Je, elimu yetu ina tofauti na haya anayosema Freire? Mfano, utasikia wanafunzi zaidi ya asilimia 50 “walishindwa” mtihani hivi majuzi. Je, ni kweli walishindwa ama ni namna nyingine ya kuwakandamiza vijana wasio na hatia?
Na kama kweli walishindwa, je, tunawapa nafasi na elimu gani nyingine mbadala? Na je, tunatengeneza mazingira gani ya kuchochea uvumbuzi, hamu ya kujisomea na ubunifu ndani na nje ya mfumo rasmi wa elimu?
Hakuna uhalisia
Elimu na miundo yake ambayo haiakisi uhalisia wa mwanafunzi, haichochei fikira mpya, ubunifu wala uvumbuzi na mbaya zaidi haivutii watu kuwa walimu, haitufai.
Mfumo wa elimu unatakiwa kuwa rafiki, wezeshi kwa makundi ya watu hasa wa vipato duni ili wajisikie huru kutambua mifumo ya unyonyaji, na kuzalisha jamii ya haki na usawa. Bila hayo mabadiliko, elimu itaendelea kuwanufaisha watu wachache na kushindwa kutimiza lengo lake la msingi la kumkomboa mwanadamu.
Kazi kubwa ya elimu ni kuwajengea nidhamu wanafunzi na kuwafungua kifikra kiasi cha kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha. Lengo la elimu siyo tu kuzalisha watu wenye vyeti vinavyoonesha wamefaulu kwa viwango vya juu.
SOMA ZAIDI: Mheshimiwa Rais Samia, Unaiona Lakini Hali ya Elimu ya Sekondari Tanzania?
Umuhimu wa tafakuri hii ya Freire katika ufundishaji nchini Tanzania ni mkubwa sana. Kuna mkanganyiko na udhaifu wa makusudi katika mfumo wa elimu yetu: kuanzia sera na falsafa ya elimu, lugha ya kufundishia, mbinu za kufundishia, na uhusiano kati ya mwalimu na mwanafunzi.
Leo tunaongea kuhusu vijana wengi kuhitimu masomo, lakini bado hawana uwezo na ujuzi wa kuajiriwa, maana yake, pamoja na mambo mengine, mfumo wetu wa elimu una ombwe na udhaifu mkubwa. Vijana wengi hawana ujuzi na mbinu za kimaisha, au soft skills kwa kimombo, ambazo zinahitajika katika karne hii.
Hatima ya elimu yetu na maendeleo ya taifa hili yapo mikononi mwetu wananchi. Kazi ya kuboresha elimu na utawala bora ni yetu sote. Nionavyo mimi, bado hatuna hasira ya kutosha katika kufanya mageuzi kwenye sekta ya elimu.
Kazi ya elimu iwe ni kutufikirisha, kupanua maono, kudadisi dhana na sera zetu ziwe za uchumi, za taasisi ya kifalme kama ya urais, sera za nje na mahusiano na mataifa, muundo wetu wa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar na dhana ya uzalendo na taifa la “maadili.”
Tupinge mfumo wa elimu unaotumezesha propaganda uchwara na mazingira ya ki-imla ambayo yanawekwa na mamlaka. Mazingira hayo yanakandamiza uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari, hasa katika kuleta taarifa za kiuchunguzi, tafiti huru na mawazo mbadala.
SOMA ZAIDI: Wadau Wasisitiza Utekelezaji wa Vitendo Mikakati Elimu Jumuishi
Ninafahamu kuwa Serikalini kuna mpango mkakati wa kuongeza ujuzi na maarifa, na waajiri wanatozwa tozo ya uendelezaji ujuzi kufanikisha mpango huo. Ninaelewa kuwa tozo hii inatakiwa kutumika katika programu mbalimbali za kuendeleza nguvu-kazi kwenye maarifa na ujuzi mpya. Sasa, sijui ufanisi wake upoje mpaka sasa? Tathmini ya mikakati hii ipoje?
Thamani ya lugha
Tuwekeze na kuboresha hata lugha yetu ya Kiswahili. Dira yetu ya taifa itambue nafasi ya Kiswahili katika elimu na maendeleo yetu. Tuwaache watoto wasome na kupata ujuzi kwa lugha wanayoifahamu, huku tukiwafundisha Kiingereza kama lugha nyingine za kigeni, ikiwemo Kichina. Linapokuja suala la lugha, tusilazimishe kumweka punda nyuma ya mkokoteni kisha tukamtaka auvute kwenda mbele, haiwezekani!
Lugha kama Kiingereza inaweza kuwa ni kichaka cha kuficha tatizo la kukosa ujuzi fulani. Ukishakuwa na ujuzi mkubwa katika eneo, au nyanja, fulani, lugha ni kiunzi kidogo sana, japo ni muhimu.
Wachina wengi wanaokuja Tanzania kufanya miradi huwa na uwezo mdogo wa kutumia lugha ya Kiingereza, lakini kwa sababu wana ujuzi mkubwa katika nyanja zao, lugha haiwakwamishi kutekeleza majukumu yao. Tatizo letu kubwa ni fikira finyu.
Umma unahitaji kuelimishwa na kushawishiwa kufanya maamuzi bora kwa mustakabali mwema wa taifa hili. Propaganda za makusudi kupitia vyombo vya habari ili kuwapumbaza, kuwafubaza, na kuwapotosha Watanzania kwenye masuala nyeti na ya msingi zikomeshwe.
SOMA ZAIDI: Richard Mabala: Je, Kupata Nafasi ya Shule Ni Kupata Nafasi ya Elimu?
Fasihi ni nyenzo nzuri katika kutunza maarifa na utambulisho wetu. Na katika hili, kuna taasisi mbili kubwa hazilisaidii taifa katika makuzi na uendelezaji wa fasihi kama njia ya kuimarisha uhuru wa maoni, nazo ni Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Mwalimu Nyerere, katika Azimio la Arusha, alifahamu kuwa kuna mfumo kandamizi na jinamizi, lakini huo mfumo unaishi na kuchanua kwa sababu ya udhaifu wetu. Mfumo upo chini ya tabaka lenye nguvu ya uchumi na kisiasa nchini.
Tabaka hilo hutumia vyombo vya ushawishi kuwahadaa wananchi na vyombo vya mabavu kuwalazimisha wananchi wafuate matakwa ya mfumo. Ni wajibu wetu kama wananchi kuupinga mfumo huu, na Pedagogy of the Oppressed inaweza kutusaidia kwenye mbinu za kulifanikisha hilo.
TAFAKURI JADIDI YA NAFSI
KILA tunapofikia tamati ya mwaka imekuwa ni hulka ya wengi kutulia na kufanya tathmini juu ya hatima ya maisha yetu. Ni ishara nzuri kufanya tafakuri yakinifu kuhusu changamoto zilizojitokeza, mafanikio yaliyopatikana katika malengo ya kibinafsi na kitaasisi ambayo yaliwekwa mwanzoni mwa mwaka. Ni zaidi ya umuhimu, kuwa na utamaduni huo wa kujikagua mara kwa mara. Hata hivyo, ni rahisi kufanya mapitio ya vitu fulani ama taasisi, watu wengine na mambo kadhaa ya nje yetu. Naam, ni vigumu mno kujikabili wenyewe; hasa katika aibu zetu, vilema vyetu, kushindwa kwetu na sehemu ya historia zetu hasi.
Kuna maumivu ya kukubali kuwa wakati mwingine sisi wenyewe ndiyo tatizo kubwa,hivyo yanafanya kazi hii ya kujitathmini iwe ngumu sana. Mtu anahitaji ujasiri na ukomavu kujikabili na kujisaili nafsi na nafasi yake hapa duniani. Pale ukifaulu kuishinda hofu ya kukikabili kivuli chetu cha kuacha kuchukulia mrejesho hasi kama chuki, wivu na husda, na kutokuwa wepesi kuwageuzia kibao wale wanaoyaona matatizo yetu, hapo ndipo safari ya kujitambua inapoanza. Ikumbukwe njia hiyo ni kama ilani na dira yako ya maisha pamwe na taasisi, ndugu, marafiki na uhusiano wako na jamii. Kwa muktadha huu, hata Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ili ifanikiwe na kukamilika inahitaji tafakuri jadidi yenye adili ya kila mwananchi.
Baadhi ya maswali ya msingi ambayo hayakwepeki katika safari ya kujitafiti lile lengo mahususi la uwepo wetu duniani ni kama; je, uwepo wangu duniani una maana na lengo gani? Je, nisingezaliwa ni ombwe gani ningesababisha? Je, siku nikifa (maana kifo kipo kama vile kivuli; tunatembea nacho) ni pigo na pengo gani nitaacha? Je, mchango wako ni upi na unajulikana kwa lipi? Je, una projeti na ndoto fulani ya maisha au wewe ni bora liende? Ukipewa nafasi ya mwisho kuishi utajirekebisha nini? Hakika, maisha ni kama kitendawili, huanza kukosa ‘maana’ pale unaposhindwa kutegua unapambania nini zaidi ya mahitaji yako binafsi. Na hiki ndio chanzo kikubwa cha ugonjwa wa sonona ambao huathiri zaidi nafsi.
Mathalani, hili zoezi pevu na endelevu la kujifahamu mwenyewe ni tabia ya lazima na ndio ni kiini cha falsafa ya Sokrates. Aliyeamini kuwa kabla ya kuutafiti ulimwengu, ni vyema binadamu ajitafiti mwenyewe kwanza. Tafsiri yake ni kwamba, maisha bila kujitafakari mwenyewe katu hayajawahi kumfaa mtu yeyote. Ndiyo maana, kujijua na kujitambua ni mwanzo wa hekima zote, alitanabaisha mwanafalsafa Aristotle. Na moja ya raha na mahaba ya binadamu ni katika kujinenea mazuri na kujitabiria siha njema juu ya maisha yake.
Aghalabu, tunakimbizana na upepo wa miadi, ahadi kemkem na kukutana na watu ili tusikike na kuthaminiwa, lakini pengine tunasahau, tunapuuza au kuogopa kukutana na nafsi zetu kwa sababu zinaanika vidonda na udhaifu wetu. Tupo bize kutafuta riziki mpaka tunakosa muda wa faragha na mapumziko. Ni hatari, kukosa ule utulivu na kuogopa ukimya ili ujisikilize, ujikague na kuzama hadi kwenye fundo la moyo wako, kwenye kioo cha ndani.
Kipindi hiki kuwa mbinafsi kidogo, jipe muda wa pekee yako itasaidia kuishi kwa uwiano, utoshelevu na utulivu wa ndani. Upweke si ukiwa. Kuna nyakati huwezi kukutana na ‘wewe’ bila kuwa peke yako. Matatizo mengi ya mwanadamu yanatokana na kushindwa kukaa kimya peke yake ajitafakari alinena Carl Jung (1875–1961). Laiti angelifaulu kukaa kimya, kujipata na kujipatanisha na nafsi yake kwanza, basi matatizo mengi yangeepukika. Kwenye ukimya unajitazama upya na unajikosoa. Kwenye ukimya unajisahihisha na kujihuisha. Kwenye ukimya unajichaji, hatimaye unajipatia nguvu na ari zaidi.
Umuhimu wa Elimu ya Nafsi
Somo la kwanza ambalo elimu ya nafsi inatufunda ni juu ya umbumbumbu au uelewa wetu hafifu juu ya mambo fulani. Kuna faida fulani ya kutojua kila kitu hasa kipindi hiki cha lundo la taarifa ambazo ubongo hauwezi kuzichakata sawasawa. Kwanza anayejifanya mjuaji wa kila kitu ni mtu hatari. Kuwa na udadisi,unyenyekevu na kuwa muwazi kujifunza ni muhimu sana. Kuishi ni kujifunza daima, hakuchoshi wala hakumaliziki. Na maisha bila misingi, tunu fulani na imani ni maisha matupu, yaliyojaa ubatili, figisu na uzengezi. Maisha ya mwanadamu, tofauti na viumbe wengine, ni kuitafuta maana, na hii ndiyo mada kuu. Maana na amana ya kuwepo kwetu duniani, maana ya hatima yetu, riziki, mapenzi na furaha, hali kadhalika, maana ya kukosa na maana ya kupata. Kusudio la maisha ndiyo msukumo na masumbuko yetu makuu na yanayotupa maana inayokamilisha maisha yetu.
Uhuru wa ndani na elimu ya nafsi inakupa mtazamo na msukumo chanya kuhusu maisha, kuchochea hamasa ya kuishi licha ya changamoto zake. Mtazamo chanya wa maisha kadiri ya mshunuzi mbobezi Viktor E. Frankl (1905–1997) unasaidia kuona changamoto za maisha kama alama ya mkato na si nukta, ndiyo maana hata giza husaidia kuona nyota.
Katika safari ya maendeleo binafsi yaani “self-development” kwa kimombo, unatakiwa ujitafakari (introspection) kwa yakini na bila kukoma. Hebu jiulize, je, ukiondoa elimu, ujuzi, kazi, mali, cheo na watu uliowaweka karibu, utabaki na nini kinachoweza kubeba thamani yako? Wakati mwingine watu hawakuheshimu “wewe” bali huheshimu vile vinavyoambatana na wewe; elimu, cheo au umaarufu wako. Wewe ni zaidi ya vitu hivyo vyote, je, wewe ni nani?
Alafu, vuta picha uko mahali, unakutana na WEWE. Je, ungempenda? Ungependa kukaa na kuishi naye? Ungependa uwezo na ndoto zake? Kwa unavyomfahamu, WEWE, angefaa awe nani kwako-rafiki, mwenza, mzazi, mtoto, jirani au? Ungechukuliaje upungufu na haiba yake? Desturi ya kujitafiti na kukutana na ‘mimi’ ni la jadi na endelevu.
Na Isaac Mdindile ni mwanaharakati wa haki za binadamu na mchambuzi wa masuala ya kijamii. Kwa mrejesho anapatikana Twitter au X @IsaacGaitanJr
IFAHAMU HOSPITALI YA ‘CONSOLATA’ IKONDA
UTANGULIZI
Hospitali ya Consolata Ikonda ipo katika mkoa wa Njombe, wilaya ya Makete katika kijiji cha Ikonda, takribani mita 2050 toka usawa wa bahari na umbali wa kilometa 82 kutoka Njombe mjini. Ilianzishwa na kusimikwa rasmi mwishoni mwa mwaka 1963, kwa ombi la wenyeji wa eneo hili la Ukinga chini ya mwakilishi wao Chifu Kiluswa. Huyu Chifu aliomba kwa Wamisionari wa Consolata kujengewa kituo cha afya ili kusaidia kutatua changamoto za huduma ya afya ili kuokoa vifo vya uzazi kwa akina mama na watoto.
Basi hayawi hayawi, ombi la Chifu Kiluswa lilikubalika na kubarikiwa, hivyo ujenzi wa awali ukaanza mara moja. Na mwaka 1968 hospitali ilifunguliwa rasmi na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mwl Julius K Nyerere. Na baadae ulianza ukarabati na uboreshwaji mkubwa wa majengo, rasilimali watu na vifaa tiba vya Hospitali ili kuboresha utoaji wa huduma bora. Leo hii Hospitali ina wodi 11. Ina uwezo wa kulaza wagonjwa karibu 400 na vyumba 6 vya upasuaji.
Na huduma za afya zinazotolewa hapa ni; huduma ya kwanza masaa 24, huduma ya wagonjwa wa moyo, presha na kisukari, huduma ya viungo saidizi (bandia) na huduma ya ushauri nasaha kwa wagonjwa wa HIV na Kifua kikuu. Pia kuna huduma za kibingwa za upasuaji (general surgery); upasuaji wa njia ya mkojo (urology), tezi dume na figo, upasuaji wa matatizo ya maumbile ya kuzaliwa na uzazi kwa wanaume, upasuaji wa sikio, pua na koo. Bila kusahau, huduma ya upasuaji wa mifupa na kufanyiwa mazoezi tiba (physiotherapy).
Kuna huduma ya magonjwa ya akina mama hasa magonjwa ya uzazi. Zinapatikana pia huduma ya vipimo kama Histopathology (vipimo na uchunguzi wa magonjwa ya tishu na seli mwilini), vipimo vya maabara, vipimo vya saratani, vipimo vya mionzi na vipimo vya mfumo wa chakula kwa njia ya haja kubwa (Colonoscopy) na njia ya tumbo. Kwa sasa, hii taasisi pamoja na kutoa huduma ya afya, pia inatoa ajira kwa watanzania wengi, kwa sasa kuna wafanyakazi zaidi ya 349. Haya ni maendeleo makubwa kwa hospitali ya pembezoni kama hii na isiyo ya kibiashara.
DIRA NA DHAMIRA YA HOSPITALI
Kama nilivyosema kuwa hii ni hospitali binafsi na siyo ya kibiashara, inayomilikiwa na kuendeshwa na wamisionari wa Consolata, shirika la kitawa la Kanisa Katoliki linalofanya kazi Tanzania toka mwaka 1919. Ni Shirika la Wamisionari wa ‘Consolata’ (kutoka neno consolation- lenye maana ya kuwa/kutoa faraja miongoni/kati ya watu) lilianzishwa huko Italia mwaka 1901 na mwanzilishi wao ni Padre Yosefu Allamano (1851–1926).
Dhamira na Dira ya hii hospitali inaenda sambamba na lengo la kuanzishwa kwa Shirika la Consolata na kazi yake duniani. Kumbe, kuzaliwa kwa Shirika hili kulitokana na msukumo wa ndani wa mwanzilishi pale alipopata ufunuo wa Mungu ambao unatoka katika kitabu cha Nabii Isaya 40:1 inayosema: “Wafarijini mioyo, watulizeni mioyo watu wangu, asema Mungu wenu”.
Na kwa kweli, Hospitali hii imekuwa ni faraja na tegemeo kubwa sio tu kwa wagonjwa kutoka nyanda za juu kusini, bali pia kwa wagonjwa wengine kutoka pande zote za Tanzania wanaohitaji tiba, ushauri, na vipimo bora.
MAFANIKIO NA CHANGAMOTO ZA HOSPITALI
Kama ilivyoelezwa awali, kuwa sababu na lengo kuu la uwepo wa Hospitali hii ni utoaji wa huduma katika misingi ya ubora, taaluma, utu na ustawi kwa wote. Ukifika hapa Hospitalini ni rahisi kutambua na kusikia kuwa huduma ya afya bora ni kipaumbele na haki yako. Kwa muktadha huu, falsafa ya hospitali hii ni:afya/huduma kwanza na malipo/faida baadae. Na hili ndilo eneo la mafanikio katika kutoa huduma nzuri inayoleta faraja kwa wote.
Eneo lingine la mafanikio ni kuona Hospitali ya Ikonda inatoa na kulipia baadhi ya gharama za huduma kwa makundi maalum hasa: Watoto wote chini ya umri wa miaka 10 na wanawake wanaojifungua (kawaida na upasuaji) wanao toka ndani ya Wilaya ya Makete. Pia wanahudumiwa bure watu wanao ishi na virusi vya Ukimwi, wajawazito wanao subiri kujifungua, na wagonjwa walio shindwa kabisa kulipa gharama za huduma.
Hii karama ya Hospitali kutanguliza utu na huduma kwanza, kumeleta mvuto sio tu kwa wagonjwa, bali hata kwa wataalamu, hasa wataalamu wa afya wakujitolea (volunteers) hususan madaktari na manesi kutoka Ulaya. Uwepo wao unaleta ufanisi mkubwa hasa katika kuboresha utoaji wa huduma, kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo na wataalamu wazawa.
Sambamba na hilo, kuanzia mwaka 2020 Hospitali ya Ikonda ilianza kupokea madaktari Talajari (Medical Interns) waliomaliza masomo yao ili kuja kufanya mazoezi ya mwaka mmoja, kadiri ya taratibu ya Wizara ya afya. Tathmini inaonesha kuwa uwepo wao una mchango mkubwa kwa taasisi na kwa wagonjwa.
Baadhi ya changamoto endelevu ambazo zinaikabili Hospitali ni pamoja na: instability ya wafanyakazi (retention), wafanyakazi wengi wanapopata ajira/vyeo Serikalini na mijini wanaacha kufanya kazi katika hospitali kama hizi za vijijini. Kwa hospitali isiyo ya kibiashara inapata changamoto pale inapotubidi kuongeza mishahara pamoja na kupandishwa vyeo kwa wafanyakazi.
Pamoja na hizo changamoto, Hospitali inaendelea kutoa huduma yake kwa ubora na ufanisi mkubwa, bila kusahau wala kupoteza lengo la uwepo wake la kuwa faraja na tumaini kwa watanzania wengi.
Hitimisho; ni muhimu sana sera na huduma ya afya itazamwe katika ujumla wake, yaani kimwili, kiroho na kiakili. Tutambue kuwa kutoa huduma ya afya bora na kwa bei nafuu kwa wananchi wetu hakutowekezana endapo tutaendelea kuangalia ugonjwa wa watu kama chanzo cha kujitengenezea faida au kuongeza mapato serikalini. Ndio maana, katika sera ya afya Serikali inawajibu wa kuoanisha bima ya afya na hifadhi ya jamii kwa wote. Bila hivyo, huduma mbovu za afya ni chanzo kikubwa cha umaskini kwa watanzania.
Na Isaac Gaitan. Kwa mrejesho anapatikana kupitia Twitter kama @IsaacGaitanJr.
KLINIKI YA MALEZI NA MAKUZI
“Kumbuka; migogoro na kutoelewana katika maisha, ndoa na mahusiano ya kijamii ni jambo la kawaida kabisa. Kwani, migogoro mingi inatokana na tofauti zetu za kimakuzi, kitamaduni, kidini, kijinsia au kimaslahi”
Zamani sio zamani sana, zama na enzi zile tulipokuwa wadogo, mimi na dada yangu tulikuwa wasumbufu mno kwa wazazi wetu na wagomvi gumzo kati yetu. Kwa sababu, wazazi walishinda kutwa nzima kazini na kuchelewa kurudi nyumbani, basi muda mwingi tulibaki nyumbani pekee yetu. Baada ya muda, wazazi walitambua umuhimu wa kuwa na mfanyakazi wa ndani ili akae nasi na kusaidiana kazi za ndani. Basi, tukaletewa dada wa kazi, ambaye kwa kweli alikuwa kama sehemu ya familia yetu kwa utu, upendo na upeo wake.
Yule dada wa kazi ndiye alikuwa kama hakimu wa baadhi ya migogoro na misuguano mingi kati yetu. Kumbuka; migogoro na kutokuelewana katika maisha, ndoa na mahusiano ya kijamii si jambo geni, ni jambo la kawaida kabisa. Kwani, migogoro mingi inatokana na tofauti zetu asilia za kimakuzi, kitamaduni, kidini, kijinsia au kimaslahi. Kwa mantiki hiyo, jambo la kuepuka, ni hii migogoro na kutoelewana/conflicts/upinzani wetu kugeuka kuwa confronts, jaribio la kumpoteza mwingine/kuminya koo, uhuru wake wa kuongea/kuishi.
Basi, sisi kama watoto na kama sehemu ya malezi na makuzi tulipata haki ya kucheza, kujisomea, kusaidia kazi za ndani kama kufua nguo zetu, kuosha nyombo nk. Ama kweli, samaki mkunje angali mbichi, ndio maana tukiwa bado watoto tulifundishwa umuhimu wa ibada, kuishi undugu, nidhamu ya muda, pesa, na kazi. Tulikuwa na ratiba na taratibu fulani ya kufuata.
Mimi natubu kuwa nilikuwa mchokozi na ugomvi zaidi, mfano, nilipenda kuchafua daftari za dada yangu kwa kuchoro vidudu. Na dada yangu, kifungua mimba, alipenda kunizomea na kunizodoa zodoa hasa pale nilipofeli masomo shuleni. Tulikuwa na ugwadu wa ugomvi wa kizaa zaa. Sasa kasheshe na sekeseke la ugomvi ilikuwa ni kukosekana kwa subira kati ya muda ugomvi umetokea na muda wa hukumu (pale wazazi watakaporejea) maana muda mwingi dada wa kazi hakuweza kuleta upatanisho na suluhu endelevu.
Migogoro yetu ilikuwa mingi, maarufu na ilijirudia maradufu. Hivyo ilibidi wazazi wabuni mbinu-tunu za kuzuia migogoro isigeuka vita fulani/confronts. Suluhisho ilikuwa ni kuandaa “daftari la malalamiko na miiko”. Hili daftari niliwekwa mahala peupe kibalazani. Kabla hawajaenda kazini, walitupa maagizo kufuata: “andikeni katika daftari hili ugomvi na matatizo yote mtakayokumbana nayo kutwa nzima”!
Hivyo, kwa mfano, mimi baada ya kuzomewa tu, badala ya kurudisha zomeo/tusi au kumpiga dada yangu, naenda kuandika/kuieleza hiyo kesi na hisia zake kwenye daftari. Lilikuwa ni daftari la kidemokrasia bila ghasia. Na dada yangu pia alikuwa na haki ya kujibu tuhuma na kujitetea kwa wino. Na yeye akitukanwa au nikimgomea kazi fulani, badala ya kunipiga, anaenda kuandika hilo tukio. Utadhani, ulikuwa kama utani ama mchezo fulani, lakini ulitusaidia kuzieleza hisia na kupunguza hasira-hasara zetu. Watoto wadogo ni watu kamili wenye hisia kama sisi watu wazima. Hata kama wakati mwingine hawawezi kusema wazi wazi, ukweli ni kwamba akili zao ni kama dodoki linalonyonya kimya kimya yale wanayoona tukisema na kutenda. Na watoto wetu wanajifunza zaidi kwa kuiga, kushuhudia na kuhisi kuliko maelekezo na maagizo.
Kwa muktadha huu, pamoja na kutatua/kuepusha taharuki, daftari lile lilitusaidia kujilea na kujielewa zaidi, lakini. Nguvu na hasira za kupigana zilipotelea na kufukiwa kwenye wino-maandishi na ile kumaliza tu kuandika na hasira ilipotea. Wazazi wakirudi, walipitia daftari na mara nyingi walijawa na tabasamu nyusoni kwa yale waliyoyasoma.
Kuna wakati walilazimika kutukanya au hata kuadhibu, lakini mara nyingi ile tu kuandika tayari iliponya majeraha na karaha zetu. Si haba, kusema kimaadili na kadri ya hii mantinki, kuwa moja ya kanuni- anuwai ya kujifunza kuishi vizuri ni kuandika hasa hisia zetu. Kwa hiyo, ile kuhamasisha na kuhamisha mawazo toka kichwani hadi kinywani, kutoka mikononi hadi kwenye karatasi, ni zoezi linalotibu na kuratibu hisia zetu wakati mwingine linatibua na kutoa utaratibu fulani. Ofkozi, zoezi la kuandika ni kusuka maneno, ni ibada fulani inayogusa na kuifunza nafsi, hakika ni therapeutic exercise. Ili kuandika lazima kufikri na kukiri/kutubu. Hata ukiwa na gagasuko la akili, andiko linasaidia kupalilia na kupangilia ubongo, mihemko na ulimwengu wetu wa ndani.
MALEZI LEO NA KESHO.
Kama wazazi sio tu wazaaji mara nyingi tunahangaika sana ili kuwajengea watoto wetu maisha bora, kwa kuwanunulia vitu na kuwapeleka katika shule nzuri, jambo ambalo ni muhimu mno, lakini mara nyingi tunasahau ukweli kwamba malezi endelevu na mtambuka ndio liwe jukumu na kipaumbele chetu kama wazazi. Kwamba ubora wa mahusiano kati yetu na watoto wetu ni takwa kuu na la kwanza kwa watoto wetu.
Jukumu letu la kudumu kama walezi walowezi ni kuwasaidia watoto wetu kujenga mtazamo chanya, mpana na sahihi wa maisha toka utotoni. Huo mtazamo chanya utawasaidia kujiamini na kujituma na hata kuwa na nguvu ya kufanya mambo makubwa katika maisha kwa kudra na kadri wanavyokuwa. Hapa nitaoroshesha baadhi ya amri na kanuni za malezi ya leo na kesho, ni amri ambazo hazichuji wala kupitwa na wakati.
-Mosi, waaminishe watoto wako kuwa upendo wako kwao sio kwa sababu ya utii wao kwako. Bali ni upendo wa kweli na bure, usio na masharti wala mashaka. Ni upendo kama wa kimungu usio na mipaka wala sio deni fulani.
-Pili, weka desturi ya kuwaomba msamaha watoto wako. Mazoea ya kusema “mtu mkubwa au kiongozi hakosei ni mbaya na inalea umungu-mtu. Kuomba msamaha ni ubinadamu na sio udhaifu. Unapoomba msamaha unamfundisha mtoto kuwa sisi ni binadamu tuna mapungufu yetu na kwamba mahusiano sio ushindani fulani wa kwamba nani ni sahihi daima. Kuonesha kuwa wazazi ni wajuaji wa vitu vyote sio sahihi.
-Tatu, siri kubwa ili mahusiano yoyote yawe tengamavu na endelevu ni mawasiliano. Usizungumze na mwanao au mwenzako huku unafanya jambo jingine. Usimsikilize ILI kumjibu. Sikiliza tu, sikiliza yote hata ambayo haongei kwa maneno. Na usipotezee wala kudharau kusikiliza stori za kitoto alizonazo mwanao leo, akikua utatamani akwambie mambo yake muhimu lakini hatokuruhusu wala kufunguka. Unayoyaona madogo kwako, kwa mtoto ni mambo mazito. Sikiliza kwa makini bila makato!
Na mwisho, malezi yoyote yanahitaji nidhamu na kiasi fulani-lazima kubalanzi-usimlee mtoto kimayai sana wala usimlee kikatili mno. Kila jambo kwa kiasi na kasi yake.
Twitter @isaacMaverickjr
https://udadisi.com/uchaguzi-wa-brazil-watanzania-kama-tunataka-tujifunze-nini/
THE PRINCE
“Kama mwana mfalme na kabila lake wanataka kubaki madarakani, basi hima na imla, wajifunze uongo, uswahiba na kutukuza maovu” Niccolo Machiavelli (1469–1527)
Ndugu msomaji, naamini katika pilika na pitapita zako hasa katika viwanja na nyanja za siasa umewahi sikia au kuitwa jina la “machiavellian” hivyo unajua harufu ya neno hilo. Ni kama vile kutwaa na kuitwa “delusional” kama ambayo Wabrazili wanavyomwita waziwazi Rais wao Jair Messiah Bolsonaro. Ambaye harakati zake za ‘the strategy of chaos’ za kupindua demokrasia, kupinga chanjo dhidi ya Uviko-19 na kutetea udikteta waziwazi zina mgharimu kucha kila uchao.
Naam, katika anga za kiutawala mtu “machiavellian” ni yule kigeugeu, mwongo na dhaifu kwa kukosa mikakati mbadala. Tabia ya nchi ya machiavellian ile ya siasa za propaganga, za uswahiba na kukwepa majukumu ya kikatiba. Na mbaya zaidi ni kushamiri kwa genge fulani (a shadow state) lenye nguvu za kiuchumi, za giza na ushawishi mkubwa bila mipaka ndani ya serikali mpaka kuhodhi taasisi za kidemokrasia kwa faida zao binafsi.
The Prince ni kitabu maarufu kilichoandikwa na Nicolau Machiavelli mwaka 1513. Kwa kinagaubaga, kinasimulia na kutoa ushauri kwa viongozi namna ya kuendesha nchi na kubaki madarakani kwa nguvu na kwa namna yeyote ile. Ni kitabu maarufu na chenye ujumbe wa kushtua -licha ya kupambwa kisanaa zaidi. Lengo la mwandishi ilikuwa ni kuamsha watu usingizini na kukataa utii-upofu. Na hasa kuanzisha mapinduzi ya kiimani kwa wasomaji kwa kutumia silaha ya maneno/fikra mpya na mbadala. Katika sura ya 18, kwa mfano, tunasoma “mwana mfalme lazima alinde na kutunza imani yake, atimize ahadi zake,na yeye mwenyewe aoneshe kujiamini na kuaminika” alisema Machiavelli. Ni vyema na haki kwa mwanamfalme asimamie kauli zake au ajiuzulu kwa kushindwa kibarua kuliko kila mara kulalama na kutupia lawama gizani na kwa wafuasi wake wakati yeye na mfumo mzima ndio umeoza.
Hiki kisa cha Machiavelli pia kinasimuliwa katika riwaya “Richard III” ya William Shakespeare. Huyu mwandishi nguli na maarufu anasimulia visanga na chokochoko za madaraka. Tazama, anashauri kuwa ili kuhami demokrasia na uhuru ni lazima kwanza tuwe raia waadilifu, wacha Mungu na kujenga taasisi imara. Tunahitaji demokrasia kuliko inavyotuhitaji sisi. Na kuliko, mkataba na matabaka kama tulivyo sasa, tunahitaji Agano jipya la kikatiba (ambalo ni holistic, yaani kupigania mfumo mzima wa uchumi na kisiasa ambao unatetea maslahi mapana ya raia wote. Ingawa, Katiba mpya sio hirizi kiunoni, ila ni kiunganishi na tiba habibu katika ombwe kubwa la kiuongozi tunalopitia.
Mathalani, kitabu cha “The prince” ni mkusanyiko wa mafunzo ya kifarisayo na kikatili. Ni nasabu feki bila haya wala aya katika zama hizi za uwazi na uanaharakati-hai. Uongozi unapokosa dira, utu na legitimacy hukimbilia mabavu, kupandikiza chuki na sheria/tozo kandamizi badala ya diplomasia na sharia rafiki.
Pamoja na kujitapa kama nchi ya uchumi wa kati na dona kantri, nchi ya Machiavelli ilijaa ubaguzi wa kisiasa na kukosa maadili hata kwa baadhi ya viongozi wa dini na taasisi zao-wengi walikuwa wasaka tonge tu na walikaa kimya hata pale upotevu wa tunu za kitaifa ulipoonekana waziwazi. Pamoja na kutumika kisiasa, pia walikosa ujasiri wa kupinga ukiukwaji halaiki wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora. Walikengeuka na kugeuka mbwa-mwitu katika ngozi ya kondoo kama inenavyo misaafu mintarafu. Na wananchi nao walivumilia tu uraia na rai yao ya kuishi.
Kutoka kwenye kitabu tunajifunza kwamba mapambano na tija ya kupigania haki na ukombozi wa kweli ni ya kila mmoja wetu. Ni mchakato na mapambano ya muda mrefu, hivyo lazima yafanywe sehemu ya utamaduni wetu, kwa maana hata hili la watawala wetu kujiona wafalme, juu ya sheria na kugawana vyeo kiswahiba na kiitikadi, kufanya juhudi za maksudi kukwamisha harakati za kupata #Katiba Mpya, kukosa agenda endelevu na mbadala za kitaifa, is just a point of an iceberg. Shida zetu ni kubwa zaidi. Tusijidanganye kupita njia za mkato. Tabia za watawala kama the prince ni matokeo ya utamaduni, mapokeo na mienendo ya kisiasa ya muda mrefu.
MZIZI WA TATIZO NI WA KITAMADUNI
Matatizo yetu mengi sio ya mtu mmoja mmoja au taasisi fulani pekee, bali ni matatizo mamoja, yanayoingiliana toka bara hadi visiwani. Bado tunafanya mambo kimazoea sana, au kwa kufuata sheria, mapokeo, maagizo fulani toka juu hata bila kuyadadisi. Kwenye jamii zetu kuna urasimu mkubwa katika taasisi zetu kutokana na uwepo wa ngazi nyingi za kimamlaka na uelewa wa tamaduni zetu ni mdogo na finyu. Kumbe utamaduni zaidi ni hali na tabia yetu ya ndani katika kujitambua kama jamii, kama chanzo kujiamini, kujituma kufanya kazi kwa bidii na uaminifu. Na pia utamaduni ni to nurture our collective imagination and creativity.
Kiini cha tatizo ni fikra finyu na hulka ya kutenganisha utamaduni katika mipango ya maendeleo yetu. Wengi wetu tunafikri utadamuni ni kucheza ngoma mbele ya watalii, kuhifadhi vitu vya kale na maendeleo ni vitu tu. Kuna dichotomy kubwa kwenye jamii yetu. Utasikia, “tusijadili na kuchanganya utamaduni, dini na siasa kwani hayo ni mambo binafsi na yasiyobadilika”(wakati utamaduni si suala la asili kama kuzama na kuchomoza kwa jua, bali suala la kibinadamu). Matokeo yake itikadi, ujadi na udini zetu zinapewa umuhimu kuliko utaifa na imani zetu, ambazo ni za enzi na muhimu zaidi.
Hakika kuna mengi ya kujitafiti, hivi identity, self-image and reputation yetu kama taifa ni ipi? Tunajitambua, tunajipambanua vipi na tunatambulika kwa lipi na namna gani kama taifa na mbele ya mataifa? What is our new ‘Tanzaphilia’? what is the ‘Tanzania Brand’? haya na mengine mengi ni baadhi ya maswali miiba kutoka kwa marehemu Balozi Juma Mwapachu katika kitabu chake; ‘Tanzania in the Age of Change and Transformation’ (2018).
Hatari ya kutojitambua na kutambulika mtambuka kama binadamu na kama taifa ni kubwa mno, ni kuenenda kiholela na bora liende bila dira na malengo yakinifu na endelevu. Na zaidi ni kuzaa jamii ya kinafiki. Tazama mienendo za maofisa serikalini kabla na baada ya kufariki dunia kwa hayati Rais Magufuli. Kipindi chake hawakuweza kuhoji kauli za Rais hata pale alipokosea na kudanganya umma, baada ya kifo chake sasa wanatoa ama kutenda yale waliyopaswa kufanya kipindi cha uhai wake.
Ndio maana, binafsi sishangai kwamba licha ya mapungufu lukuki ya Katiba yetu ya 1977 bado tunaifinyanga na hatuifuati, na zaidi tunaona hilo ni kawaida tu. Hitaji la kuwa na Katiba mpya na sheria rafiki tunaona sio kipaumbele wala sehemu ya maendeleo yetu. Na wale watanzania wenzetu ambao kimsingi ni haki yao kujieleza na kudai Katiba mpya badala ya kuwapongeza tunawadhihaki na kuwawinda deliberately eti sio wazalendo. Hakika, tupo gizani/cave kama mwanafalsafa maarufu Plato alivyosimulia ile “the Allegory of the Cave katika kitabu chake “Republic” karne ya IV a.C.
Wote tunajua kuwa uwazi, ushawishi na haki ndio siasa za kweli hasa katika zama hizi tukufu za udadisi na uvumbuzi. Na kwa kweli, siasa ni huduma na dhamana adhimu. Katika muktadha wa siasa kuna kujipendekeza sana kwa watawala na kuukanyaga ukweli kwamba wananchi ndio wenye nchi. Kinachotokea ni kwamba mtawala, angalabu wa kidikteta, huughilibu umma kwa upande lakini kwa muda mfupi, inshallah! Na umma nao, kwa kujipendekeza hutii kama mti kufuata upepo.
Hitimisho, tujisahihishe maana muda tunao. Na zaidi nyenzo na enzi bado upo upande wetu. Mosi, tukatae kuwa waumini watiifu katika kuendeleza sera za kikoloni tena kwa mbwembe kubwa. Tumekuwa watumwa wa sheria za ovyo za kifalme. Alafu, tunataka amani bila haki, maendeleo bila katiba mpya, mazungumzo bila maridhiano na ukweli. Wapi na wapi? inawezekana vipi? Kulikoni, kujitoa uelewa kuwa hayo yote ni sehemu mbili za shilingi moja? Na pia, kuna haja kubwa na haraka za to decolonize (kujivua ukoloni wa ndani) zile mila, sheria kakasi na kadhia zake. Tulinde na kutetea utu na maslahi mapana ya watu wote, hii ndio iwe sera na falsafa yetu.
Na @IsaacGaitano.
KUMBUKA, KIFO CHAKO…….
Private Arquivos
Ni saa moja usheni hivi asubuhi. Ni siku mpya ya uhai na hali ya hewa ni ya haki kwa wote. Mara ghafla, bin vu, napata meseji kwenye simu yangu. Ni taarifa maafa ya msiba wa rafiki yangu Mzee Fazenda alimefariki bila mpako kwa mlipuko wa UVIKO-19. Ni balaa toka bara hadi visiwani. Baada ya kuhakiki, nilijisemea moyoni kuwa kwa kweli, kifo ni fumbo na pigo lisilotabiriwa wala kutibika.
Nilipata wazimu na nilichelewa kuamini kuwa kifo kinauwezo wa kumeza uzima wa mtu mazima mazima hivi. Kabla ya kuanza safari kwenda msibani, nilisafiri kifikra juu ya hatma/ maana ya maisha yetu. Maisha yana maana/kusudi gani kama tunakufa au licha ya kifo?
Na eti, kifo ni mapenzi ya nani, ya Mungu au ya kiasilia/kibiologia/evolusheni pale seli za mwilini zinapokufa au kuzeeka?
Na je, kwa namna gani binadamu tuna uwezo na uhuru wa kurudisha kifo nyuma au hata kuzuia kifo? Kwa sababu kuna vifo vinavyozuilika kama vile vya ajali, vya kukosa dawa au vile vya vita. Kumbe, sio kila kifo ni mapenzi ya enzi za miungu. Binadamu tuna nyenzo za kuishi maisha marefu na bora zaidi kama tukiamua na kujipanga.
Kwamba, maisha ni zaidi ya kifo na wema unashinda maovu, hilo tunalijua mchana wa jua. Na maisha yana kanuni-anuai na miiko yake, moja ikiwa ni kuwa tusikikawaidishe kifo, ndio kusema tusidogoshe maisha yetu. Tuvunje na kuvuka huu mtego wa kitamaduni wa kuhalalisha vifo kwa bei chee. Hata tragedy ya maisha sio kifo bali kile (ndoto, fikra, ari) tunaacha kife/kioze ndani yetu wakati tukiwa bado hai alisemaga Norman Cousins. Maisha kuliko mapambo na mapambio ni mapambano. Sio mbio bali mchakato. Ni mapambano dhidi ya maadui kama magonjwa, ujinga na umaskini au kati ya nguvu/itikadi za giza na zile za mwangaza kama alivyonena mwandishi Ngugi wa Thiong’o. Na, maisha yanadai tuwe na kiasi katika kila kitu hasa zama hizi za kasi na makasia ya utandawazi na teknologia. Tulinde afya yetu kwa lishe, mahusiano bora na mazoezi, tujenge imani ya kiroho na kuishi maisha ya jumuiya, tutunze mazingira ili nayo yatutunze. Tunaishi mara moja, maisha ni mamoja, yanaingiliana na kushabahiana.
Mr Fazenda, mzee wa makamu na mkarimu haswa. alikuwa mtu na nusu kama wasemavyo waswahili. Ofkozi, alikuwa mzee kiumri lakini kimwili alikuwa mbichi na akili pevu sana. Pamoja na umri wake kusonga mbele, alijawa hekima kama za mfalme Daudi na bado aliweza kwenda msalani peke yake na kujihudumia. Maana umri ni lazima, lakini busara ni azma kama wasemavyo walimwengu.
Basi tulianza msafara wa kumsindikiza marehemu katika nyumba yake ya milele. Kama vile katikati ya viganja vyetu kuna michoro inasomeka; momento mori yaani kumbuka kifo chako, vile vile, katika ya lango la kuingia makaburini kulipambwa harufu na herufi hizi: “Kumbuka wewe ni mavumbi na katika lundo la mavumbi utarudishwa”. Kama huamini tazama kioo cha kiganja chako! La hasha, maisha ni fumbo kama mkato na mnato wa pumzi zetu.
Madhalan, hakuna atakaye niwakilisha kufa. Kifo ni changu, ni haki na milki yangu, maana hakuna aliyezaliwa wala kuishi mbadala na badala yangu. Kifo ni tendo la kidemokrasia, la kiungwana la hali ya juu sana. Na mara nyingi,kifo kinakuja kwa kunyata nyata sambuli ya upepo mwanana hakionekani ila kimezagaa zagazaga kama dagaa wa Tanganyika tayari kutusindikiza mahala pema peponi maana mimi binafsi kama vile mwandishi Dante Alighieri siamini uwepo wa mahali pa moto wa milele.
Marehemu Mzee Fazenda na maiti nyingine kwa pamoja walibebwa na magreda na kufukiwa kaburini kama vile wamekuwa mizigo fulani. Binafsi, niliona hilo ni tendo la ukatili na ubutu bila ubuntu. Ni ustaarabu gani huu tunaishi, ambapo taratibu tunasahau kwamba sisi sio herufi na tarakimu fulani. Sisi sio majivu, hata kama tukichomwa, bali tu cheche na chemichemi hai. Ndio maana, simulizi nyingi za uumbaji za Kiafrika zinataja maji na mwanga kama viumbe wa kwanza kuzaliwa. Tena tunashauriwa na falsafa ya Tao, tuwe kama maji; maana nje na ndani mwetu tumejaa maji zaidi. Tena kiongozi anayetaka kuhimili mihimili na mabadiliko ajifunze — kuwa kama maji, atililike. Asiwe na roho ya jiwe ya ukatili, ya kutuna na kutoambiliki kamwe. Bali ajivike unyenyekevu na usikivu zaidi.
Zama hizo sio zamani sana, tulifundishwa umuhimu wa kushiriki misibani. Siku hizi, tumebinafsisha hata maombolezi na mazishi, ni usiri na mapambo kupita kiasi, ili kuficha makali na ukatili wa kifo, tunachoma ganzi uchungu wake. Bado kidogo tutaanza kukodi watu ili walie na kuomboleza kwa niaba yetu. Hii sio hulka nzuri maana kifo pia ni fursa, kinatuhumanize sana. Enzi hizo utoro kwenye misiba ulitafsiriwa kama ushirikina, kumbe kushiriki ni kusafiana nyayo na nia, ndugu yangu msomaji. Basi, ibada za mazishi ziliongozwa na wazee wa weledi “vasikimafu” jina lao kule uheheni. Ibada zina simbolic value, yaani zinalegeza makali na zinaeleza yale ambayo hatuwezi kuyasema kwa maneno, maana maneno daima hayatoshi au wakati mwingine yanapwaya. Fikra hazionekani,ni haba/fukara kufafanua fumbo, ombwe na umbo la kifo. Ukweli u bayana, Allah/Mungu ni fundi katufumba vitu vingi.
Bado nakumbuka, baadhi ya tenzi za rohoni kule makaburini zilinena haya:
Kifo ni alarm sio haramu.
Kifo ni kumbushi tuishi kwa hamu na ghamu
Ardhi ina hamu na damu zetu,
To nurture nature.
Ardhini tunarudi kwa hadhi.
Urithi ni zetu hadithi.
Wafu ni maua bila tusiyaue.
Kiasili, kati ya viumbe vyote, ni binadamu tu anayelia na kuwaweka wakfu wafu. Na baadhi ya makabila yanatunza na kuzika wafu ndani ya nyumba, kwamba marehemu bado ni sehemu ya familia. Binafsi, bado nashindwa kutafuna na kumeza hii desturi ya kuchoma maiti, licha ya kwamba ni njia nzuri ya kutunza mazingira kuliko kuzika ardhini. Kikwetu ile tu kusimika mwili ardhini kuna thamani kubwa, kwanza sisi tu ardhi, walatini wanaita humus, na ndio asili ya neno unyenyekevu, kifo hutunyenyekeza.
Labda, hivi virusi vya korona vimekuja kutukumbusha tuwe wanyenyekevu mbele ya mama dunia kwa ujumla. Maana hata wataalamu wanasema uzito wa virusi duniani unazidi uzito wetu binadamu.Na ardhini ndipo tunachuma tiba na vyakula, hata madafu yanatoka ardhini, na ardhi ndipo wamelala mabibi na mababu zetu. Ardhi sio tu udongo au maada, ni kiumbe hai. Sisi binadamu ni wadogo na tunaihitaji zaidi ardhi kuliko yenyewe inavyotuhitaji sisi.
Hitimisho; tujadiliane; nini fikra zako kuhusu kifo?Unafikria kifo ni mwisho wa yote au kuna maisha baada/mbadala ya kifo? Kwanini? Na je, mawazo yako kuhusu kifo yanabadilika badilika? Kila tunapopumua tunasogeza kifo mbele. Kifo hakielezeki, hakizoeleki wala hakizeeki. Na ukweli, ni kwamba ile kuzaliwa tu, tunaanza kufa taaratibu mwendo wa taarabu bila tabu, na kwasababu, tuna haki na uhakika wa kifo, binadamu anaona kifo sio tishio wala mwisho kwake, msala na mtenenge ni kufa bila kujua kwanini na kwaajili ya nani uliishi. Ni kuishiwa sera na kuishi jela na jehanamu. Tunapotafuta riziki zetu, tusisahau kuishi.
Kwa marehemu wote hasa wa UVIKO-19; Inna lillahi wa iina ilayhi raji´un. Raha ya milele uwape Ee bwana na mwanga wa milele uwaangazie.
Alamsiki
Kitu ambacho kizazi hiki kinahitaji kufundwa zaidi ni NIDHAMU katika kila kitu, iwe ya kazi, muda, mahusiano na pia USTAHIMILIVU ambao sio sawa na uvumilivu.
Katika nyakati nyeti za uwazi na utandawazi, maisha bila mtandao hayawezekani. Huduma za internet sio starehe tena, zimekuwa ni haki na wajibu wa kiraia. Iwe taasisi, kazi au biashara zake zozote zile, zinahitaji mtandao fulani ili kujiimarisha na kuendelea kuwepo duniani. Ni ukweli kwamba, mabadiliko yaletwayo na utandawazi, yanakuja kwa kasi ya hali ya juu na ni makubwa kuliko uwezo wetu wa kuyahimili. Leo watu wanasema sio kabla ya Kristu na baada ya Kristu bali kabla ya google na baada (mbadala) ya google. Changamoto na faida ni nyingi katika karne hii ya Habari na Teknologia. Ndugu mpenzi msomaji, leo nataka tuongelea kuhusu teknolojia na afya hasa ya akili.
Tunakua na kushinda kwenye (na) dunia ya mitandao mbalimbali, (huu ni uhalisia sio nadharia tena) kama Facebook, Instagram, whats up, nk. Naam, ya mtandaoni ni mengi, kama wasemavyo walimwengu. Kama vile mitandio kwa akina mama, mitandao imekuwa kama kitambulisho chetu kipya cha uwepo wetu duniani. Mtu yupo tayari kukosa pesa ya kununua chakula, lakini sio pesa ya vocha ili kujiunga na mitandao. Lakini, uhalisia wa maisha ni tofauti na yanayoonekana na kuoneshwa mitandaoni (virtual versus real life).
Mtandaoni kila mtu anaonekana meno nje, ameyapatia maisha, ametoka na kutoboa kweli kweli. Hali zetu duni tunazionea aibu, hivyo tunazificha uvunguni. Hii mbinu haisaidii, ni butu. Tunajenga kizazi kinachokosa kujiamini, bali legelege, kinashindwa to face the real life challenges. Kizazi kinajianika masaa 24 mwambaoni mwa mitandao. Wataalamu wanasema, unapotumia simu na mitandao ya kijamii, ubongo wetu hutoa kemikali inayoitwa Dopamine, ndio maana unapopokea ujumbe fulani unajisikia vizuri. Mtu anaamka asubuhi, cha kwanza, bila hata sala ya shukrani, ni kuangalia na kusalimia wafuasi wake mtandaoni, kabla ya ndugu zake hapo jirani.
Hii kemikali ya Dopamine (wananeurosciencia wanaelewa vizuri zaidi) ndio inakufanya ujisikie raha unapovuta sigara, bangi, unapocheza upatu au kunywa pombe. Kumbe, hii kemikali ina uraibu (addiction) mkubwa.
Tukiwa wadogo tunahitaji kukubalika na kupendwa na wazazi, walezi wetu. Bila shaka, ni haki yetu. Kijana anapoingia kubalehe,anahitaji kukubalika na kundi la rika lake zaidi kuliko wazazi wake. Hapo unaanza kuwategemea na kutaka kuwaridhisha marafiki zake na kufuata mkumbo. Ili kuhimili stress za kipindi hiki, ndio watu hugundua vilevi, sigara, mitandao au mchumba ili kukubalika.
Ukiwauliza vijana wengi sasa kuhusu urafiki, wanasema marafiki wao wengi ni rafiki-jina. “Rafiki” ambaye labda hawajawahi hata kuonana. Huyu kijana akipata shida haendi kwa watu, bali anaona ni kawaida kugeukia mitandao kutatua shida yake.
Nisemacho ni hiki: Hakuna tatizo kwenye kubeti, kunywa pombe wala matumizi ya mitandao, tatizo ni kutokuwa na balance ya matumizi. Tatizo ni kutawaliwa na pombe, sigara na mitandao, mpaka kukosa muda wa kuwa pekee yako, kuwa na familia na marafiki halisi. Sikiliza: ukiwa na marafiki, wachache ndio vizuri. Urafiki wa kweli ni nadra na ni gharama. Wengi tunaodhani ni marafiki ni washikaji na wasindikizaji tu wa kupita. Chagua marafiki vizuri bila ulafi wala unafiki. Usaliti mbaya hadi ahera ni kuisaliti nafsi yako takatifu, yaani kujikufuru, kutokujisamehe, kujihukumu kwa makosa usiyoweza kuyarekebisha, kulazimisha matamanio yasiyowezekana, kusubiri wengine wakuletee furaha na kuishi bila kutumia vipawa vyako. Usijisaliti. Jikubali!
Ikitokea umeketi na umeiweka simu yako mezani, haijalishi kama umeigeuza juu au chini, hiyo inatuma ujumbe kwa wale ulionao kuwa wao sio muhimu kama hao unaongea nao kwenye simu. Mitandao ya kijamii bila nidhamu na weledi inaanza kugeuka kama madawa ya kulevya, hivyo kuleta uraibu mkubwa. Baada ya muda, taaratibu kama taarabu, uraibu unaharibu mahusiano na watu, utakugharimu muda na pesa ili kutibu afya yako.
Kitu ambacho kizazi hiki kinahitaji kujifunza ni NIDHAMU katika kila kitu, iwe ya kazi, mahusiano na ustahimilivu ambao sio sawa na uvumilivu. Kuna baadhi ya vitu muhimu maishani kama mapenzi, furaha ya kweli, kuridhika na kazi, kujiamini, stadi za maisha ni vitu vinavyochukua muda kupatikani. Achana na njia za mkato mnato. Maana mitandao inatufunza kupata/kutafuta vitu kwa namna ya haraka bila jasho (immediatism).
Bila nidhamu na ustahimilivu katika dunia ya leo, kunaleta ongezeko la matukio ya kujiua, sonona, matumizi ya vilevi na kuwa misukule fulani, bila kusudi la kuendelea kuishi. Na zaidi, ni kupunguza ufanisi na ubunifu kazini. Unamuuliza mtu vipi kazi yako, anajibu; “kawaida tu”. Au unamwuliza vipi mahusiano yako, anasema; “aah hivyo hivyo tunakomaa. Anaonesha kutoridhika na chochote hapo, ila basi tu atafanyaje. Hatuna budi kujenga uhusiano na watu wanaotuzunguka, kusalimiana, kusaidiana na kujenga roho ya kuaminiana.
Hivyo kuanzia leo, jipe malengo ndugu yangu. Usichaji simu mbele ya kitanda, unapozungumza na watu au upo chakulani, weka simu mbali. Enzi na wekeza katika ushirikiano kuliko kushindana na watu. Achana na roho ya ubinafsi na umimi. Mwisho; ukitaka kuishi kwa furaha na amani: kwanza punguza matarajio juu ya watu. Pili, wajibika kwa matatizo yako. Huwezi kuumizwa wala kuangushwa na mtu au kitu usicho na matarajio nacho.
Follow on Twitter @IsaacGaitano
Kabla ya kufundwa jandoni. Nilijifunza kuhusu jinsia. Jinsi utofauti na upekee kati ya msichana na mvulana ulivyo taji la utajiri. Nilidhani mvulana ni yule anavaa kaptura na msichana ni yule anavaa gauni, tayari na hiari kwa kuolewa. La hasha, ilikuwa akili pimbi na pofu, sikuona, kama wengi wenu, kwamba mwanadamu ni zaidi ya kuoa,na kuishi kwa mkate tu.
Maana, kuna kuona na kutazama. Kutazama ni hulka ya kibiologia, ila kuona ni maamuzi. Wengi hatupendi kuona, because it compromise, maono yanawajibisha. Macho pamoja na kuona, haswaa, yana kazi ya kutoa machozi. Lakini, eti utasikia mitaani: “mwanaume hatoi machozi!” Kivipi?, wakati kila kitu maishani ni mapenzi na enzi? Kwa kweli, jamii inatuchanganya!
Pamoja na hilo, ningali mtoto, pia nilipaliwa na swali pacha: namna gani kujua jinsia ya mimea na wanyama, ambao hawavai suruali wala sketi? Kwa maana, utofauti wa jogoo na tetea, zilionekana usoni na jogoo ndiye mwenye kilemba kichwani na aliwika. Mawazo yangu kuhusu ndoa na mahusiano zilikuwa za VITU kama suti, gauni nyeupe, nyumba nzuri, maua kwa mke. Mke/Mume “mkamilifu” na wife/husband material kama wasemavyo kule bongoland.
Siku moja tumeketi uvulini, baada ya chakula (maombi na maongezi ya faragha yanataka uwe umeshiba) mimi,baba na mama, wakati tunachapa soga basi nikatumia ile nafasi kuuliza swali lililonichefua muda mrefu:
-Baba, namna gani naweza kutambua kama paka ni jike au (na) dume?
-Mama alinikazia uso na kutoa sauti kavu. “Isaac, hapana! Isaac, hapana!”. Hayo ndiyo maneno aliyatamka. Kweli, maneno huumba na kuumbua!
-Baba alicheka kwa ulimi na meno, akajibu kwa maneno haya: “Ni rahisi, paka dume ndiye mwindaji na jike ndiye mtunza watoto”. Nukta. Lilikuwa jibu la haraka na automatiki hivyo. Ingawa, ipo hivyo katika jamii nyingi, ila leo hii mke anaweza kuwinda na baba akatunza watoto na kupika. Na maisha yakaendelea, bila mbingu kuanguka! Maisha yanaenda kwa kasi sana!
Nilitikisa kichwa, kukubali maelezo ya baba bila KUAMINI, kwa sababu, mwangwi wa uso na sauti ya mama kwangu bado ulinena juu zaidi, kuwa nilikuwa nakanyaga ardhi katazwa. Baadae sana, katika kuwaza na kuwazua, nilitambua kuwa mama alijibu vile, ili kuninusuru, labda baba angeweza kunifokea kwa sababu ya maswali yangu mwiba.
Na kama baba angesema uhalisia wa mambo, kimantiki ningeweza kuhitimisha kwa kupinga mtizamo na mfumo dume, unaodumisha jamii. Kwamba mwanamke ni dhaifu, ajifunze kupika vizuri ili aolewe, abaki jikoni na mwanaume daima ni shupavu, hatoi machozi, kitu ambacho si kweli na ni hatari (toxic masculine). Mafao na mafanikio ya mwanamke ni zaidi ya kuolewa na kuzaa watoto. Heshima yake isifungwe katika kuwa na pete kidoleni.
Naam, kadri nilivyokua upeo na maono yangu kuhusu mapenzi ulikaribiana na yale niliyaona kati ya jogoo na tetea. Bado nilitatizwa na kushangazwa na hali ya jogoo kumfukuzia tetea aliyejitetea kwa kukimbia. Bado jogoo alimkamata na kumpanda juu. Huu mchezo upo kwenye siasa zetu pia, chama chenye nguvu-dola pamoja na kudhalilisha mihimili na vyama vingine, bado kinaminya haki za msingi za wananchi wake. Chama kinajiona kina hatimiliki na kura turufu ya kufanya lolote, hata kuweka mifukoni taasisi nyingine. Tunahitaji kuhami demokrasia.
Siku nyingine, baada ya muwasho wa maswali, ilibidi nimfate tena mzee, siku ile akiwa pekee yake. Nilimbadika swali, kwa nini majogoo walifanya kitendo kile cha ushamba na kinyama?
-Mzee alijibu kwamba kile kitendo cha jogoo kumpanda tetea ni adhabu kwa jinsi tetea alivyo na makasoro yake. Maelezo yake hayakutosha, nilipandwa na chuki. Jibu lake lilinifunulia wito wangu; kutetea haki za wanyonge. Kutoka siku ile, jogoo walinikoma kwa mawe na manati. Kikweli, jamii imewajaza wanawake wanka katika kudai haki. Na mbaya zaidi ukiziwi katika kukemea vitendo vya kikatili batili dhidi yao.
Jamii inawadanganya wanawake kujiona wamefikia “expire date” “mitumba fulani” wanapofikia umri kama vile miaka 30 hivi. Utasikia kauli kama; “yeyote atakayekuja sasa naolewa naye” bila hata kuangalia kama kuna upendo wa kweli katika raha na shida. Kumbuka hili: Mtu anaweza kuwa mpenzi wako, lakini akawa hatoshi kuwa mke/mume na zaidi mama/baba wa watoto wako. Tusafishane matongotongo na tuone vajameni! Tuimbe kwa pamoja kuwa ukatili/udhalilishaji wa kijinsia ni hasara sio kwa wanawake tu, bali kwa jamii nzima.
Siku nyingine tena, nilikuwa na mama mitaani. Ghafla niliona mwanamke pembeni anahangaika na kuteseka, alikuwa anaficha tumbo (mie nilifikri ni kitambi cha kawaida) la ujauzito kwa aibu. Nilichomoza jicho la pili na kusema: “mama ona tumbo la yule mwanamke……”
Kabla sijamaliza sentensi, mama alinikatiza. Na kuniamuru kurudi nyumbani, na yeye angebaki na yule mama kumsaidia. “Labda sikuruhusiwa kuona na kuongea vile wala kutaja mwanamke mjamzito” nilijisemesha. Ndio, tuliambiwa tusisema “mwanamke anajifungua” bali ni “mgonjwa tu”.
Wazo mjarabu na mtambuka hapa ni kwamba toka enzi, iwe nyumbani au shuleni, ilikuwa nadra sana kushirikishwa mambo ya wasichana kama vile hedhi & pedi, ukeketaji, kwa nini wanawake ni maskini zaidi, masuala ya uzazi, mimba na ndoa za utotoni, ilikuwa ni miiko fulani. Nakumbuka wazazi walinikataza kata hata kusimama na kuongea na wasichana. Na dada yangu alipofikisha umri fulani, aliulizwa kwa nini haolewi, lakini hilo hilo swali halikuelekezwa kwa kaka.
Na zaidi, msichana ilibidi ajilinde asipoteze ubikira wake kabla ya ndoa na kuwa mke msamalia mwema daima. Hayo yote yalinichanganya! Kukosa huu ushirika na ushirikishwaji, kunachangia sana kufumbia macho visa na mikasa katili dhini ya wanawake inayotiririka damu kila uchao katika jamii zetu. Tuungane kukemea, lakini zaidi kuelimishana.
Just imagine, mwanamke kama hana watoto na hajaolewa anadharauliwa na kuitwa majina ya ajabu ajabu. Na mwanamke anapokuwa amefanikiwa na kujitegemea, anaambiwa asijioneshe sana atakosa mume. Mambo mengi yasiyofaa kama kudhalilisha wanamke, kuzuia msichana asirudi shule kisa mimba, ukeketaji, yanafichwa nyuma ya pazia la “kulinda mila.” Fikra hizi ni sumu. Ndio maana, sishangai leo hii, tunachangishana michango zaidi watu kuolewa na kuoa kuliko kusomesha au kufungua biashara. Sherehe ya ndoa inapewa maana kuliko ibada yake. Kumbuka, kamati ya maisha ya ndoa ni muhimu kuliko ile ya sherehe. Tujisahihishe!
Katika moja ya semina nilihudhuria, mtoa mada alisema kuwa: “Kuoana kuna masharti yake ya awali kama ; kwanza kujitambu na kujielewa vizuri, pamoja na kujimudu kiuchumi. Ndoa ni maagano sio mraba wa mkataba fulani”. Nafikri, hata tendo la ndoa ni zaidi ya kukutana kimwili, ni zaidi ya mikuno na kukata viuno, ni jinsi ya ndani kabisa ya kuonesha upendo. Na upendo pekee katika ndoa hautoshi, lazima kuinuana kiuchumi na kimakuzi.
Kutokuolewa sio doa, hakumpungizii mtu, utu na heshima yake. Hata lugha zetu tuzibadilishe, “sio mume anaoa na mwanamke anaolewa” bali wanaoana. Ndoa inapogeuka ndoano ya kukabana koo haifai. Tufungue macho kuona, ili tuwe sehemu ya suluhisho. Alamsiki!
By @ShussaJane and @IsaacGaitano
Era uma tarde fresca, céu brilhava, suando luz. Estávamos sentados à sombra de árvore pau-brasil, lá na comunidade Pedra Preta- Serras da Amazônia legal, jogando conversa fora. Após de atravessar o rio Maú, flechar peixes e tomar banho nu. Na aldeia não havia espelho, a gente se adivinhava em poças d’água.Porque o espelho, ali imóvel, também nos olha quando dele nos cercamos. Prefiro espelhar-se nos desvãos da alma.
E falávamos e debatíamos sobre política indigenista, educação, desequilíbrio ecológico, os movimentos sociais e sobre a futuro da humanidade. Antes de oração aos anjos e antepassados, o Tuxaua Zé do Facão, de pé no chão, fez uma conclusão com um fio de voz:
“Lembra-se que nós indígenas e parentes somos como essa árvore. Duas coisas são importantes na luta: a direção para cima, para o céu aberto; e enraizamento para baixo, para a terra escura. Ninguém vive sem esperança, mas também não vive sem memória”.
Até hoje lembro o tom da fala do Tuxaua e sua ressonância com as múltiplas acontecimentos na atualidade e suas complexidades. O episódio caótico do assassinato de George Floyd, no último dia 25 de maio, por exemplo, trouxe para a frente de todos os debates a questão dos negros, indígenas, e do racismo ambiental, privilégio brancos, enfim do próprio sistema capitalista que se alimenta dos “oprimidos” para sobreviver.
Visto como “outro” e diferente pela sociedade ocidental, que se acredita branca e prototípica do que seja a humanidade, a história dos negros trazidos da África e escravizados deste lado de cá do mundo foi sempre narrada por outros. Falava-se sobre os negros, a respeito deles. Mas não se ouvia a voz dos próprios, a não ser em alguns nichos que os mesmos negros ocuparam com tal genialidade e competência que era impossível inviabilizá-los.
Refiro-me aqui à música, a religiosidade afro, à dança e outras formas da arte. Porém, mesmo nestas áreas, o discurso que se fazia ouvir era de lamento, dor, gemido sob a opressão de um discurso que seria apropriado pelos que ocasionaram aquela dor.
Em bom português, hoje uma perspectiva libertária supõe a descolonização do imaginário e linguagem social, que por sua vez, implica em conhecer diretamente os sujeitos mantidos em condição de subalternidade, garantindo-lhes o direito à expressão, à enunciação da sua palavra. Eliminando uma seleção de memória que não favorece o conhecimento do passado e a construção de pertença a grupos subalternizados. Sobre essas ideias grávidas e outros ensaios, estou lendo o livro: Ideias para adiar o fim do mundo por escritor indígena, Ailton Krenak.
Ola, a descolonização é mais do que a retirada do dominador do território, uma vez que a colonização produziu formas de ver o mundo e criou uma forma particular e colonizar- named the economy of desires. O próprio colonizado enquanto sujeito foi forjado dentro do horizonte da colonização, no seio da violência inominável, mas também com sofisticação acadêmica e muitas sutilezas estéticas.
Vale destacar que, no projeto de civilização europeia, definir-se humano era separar-se de conjunto da natureza e viver de acordo com regras “civilizatórias”, o que implicava na diferenciação do “Outro” ( no sentido daquele cuja existência opositora me constitui, enquanto sujeito e me dá sentido existencial no estabelecimento de diversas linhas demarcatórias na forma de leis, fronteiras, hábitos e características físicas e culturas.
È interessante observar que, quase no mundo todo, fruto dessa mentalidade “civilizatório” houve um processo sistêmico-político e religioso de converter os povos originários em pobres. Mas esses povos não se interessa em ser como nós. Mas a história ocidental é ferramenta feroz de converter os outros “diferentes” em pobres. E é isso o que está acontecendo na Amazônia. De pobres vão virando consumidores. É uma técnica mais sofisticada aplicada hoje em dia de colonizar e explorar o outro.
Tirar a tiro a sua terra, língua, a religião acaba virando pobre. E essa palavra “pobres” é problemática, pois em algumas línguas indígena aqui e la na africana, ela não existe. Toda tentativa de tratar o outro como pobre (segundo a nossa visão, claro) e portanto como alguém que tem que ser educado, civilizado, salvo, é estar sendo cúmplices de todo esse sistema neoliberal de destruição que só pensam em produzir mais pobres. É urgente promover a capacidade de diferir, ser diferente, sem ser desigual.
Meu trabalho pastoral aqui reside justamente de colaborar (sinergia), eco-solidariedade com os indígenas a lutar para que eles mesmo definem seu próprio rumo e caminho. É uma decisão árdua e dura. O futuro do mundo é híbrido, multifacetada, de congregar muitas histórias do povo. “De conjugar a sabedoria ancestral com os conhecimentos técnicos contemporâneos” disse Papa Francisco. Precisamos ver isso, não apenas enxergar. Isso é dar um lugar à memória a essa população esquecida como assinala a historiadora Solange Rocha. Um espaço para debates públicos, socializar conhecimentos científicos e saberes populares, a partir da divulgação de novas narrativas.
Nas minhas andança aqui no Brasil tenho encontrado saberes trazidos pelos africanos como o uso de turbantes, de cavanhaque, cultivo de arroz de Haussá (Nigéria) etc. E o costume entre os brasileiros, de jogar um pouco de bebida para o santo, eram (é usado pelos africanos para partilhar com os mortos e as divindades que acreditavam poder interferir na realidade dos vivos.
Para dizer, que o Brasil, sendo o maior nação neolatina do mundo, tem tudo para ser a maior civilização dos trópicos. O Brasil pode ser útero, embrião de nova sociedade, diversa dentro da única casa comum, a mãe terra. E tem o que nenhum outro país do mundo tem na mesma extensão — a Amazônia. Mas tem também um gabinete de negacionistas da mudança do clima e nos direitos existenciais dos povos.
E entre os povos nativos podemos aprender muitas lições. Vejo que, a percepção desses “condenados da terra” é mais apurada do que a gente. Lembro numa viagem indo visitar algumas comunidades, estava chovendo, eu estava tremendo de medo. Medo do mato, trovões, bichos e garimpos. Aí alguns indígenas ficaram rindo de mim, dizendo que sou muito teimoso, preciso me identificar com a natureza. Me ensinaram de aceitar os imprevistos e os desastres da vida. Sim, eles são especialistas em fim do mundo. Viver com pouco, portátil. O chamado “pessimismo alegre” do filósofo François Zourabichvili.
Esse espírito do pessimismo alegre é muito comum entre meu povo na África. No meio da dor, guerra, a gente cantamos e dançamos e rimos. São situações dramáticas que ninguém aguenta, mas que não nos impede a se distrair e se divertir. É a forma como se realiza culturalmente o rito de passagem da vida deste lado para a vida do outro lado, onde estão os anciãos, e os guardiães do povo, de seus ritos e das normas éticas. Afinal, a vida é maior que ficar chorando dos desafios.
Vale repetir, que todos temos nossas raízes na África, embora a grande maioria o desconheça ou não lhe dê importância. Mas é decisivo que nos reapropriemos de nossas origens, pois elas, de um modo ou de outro,estão inscritas no nosso código genético e espiritual.
Por fim, os indígenas são pessoas que de fato vivem no presente no melhor sentido possível. Vivem o agora, o kairos, sem pressa nem agitação. Isso me irritava muito, no início da minha chegada aqui. Tive a tentação de cobrar deles em serem rápidos e modernos. Mas descobri que, eu que tinha que mudar a visão das coisas aqui. Aprender desaprender!
Segue no Twitter; @IsaacGaitano