Stories by Lilian Chonya on Medium
Kuwa kwenye mahusiano ni jambo moja, lakini kuwa kwenye mahusiano ambayo yatadumu na kuvumilia vipindi vyote vya jua, ngurumo, mvua na upepo mkali ni kitu ambacho watu wachache wanaweza kukifanya.
Watu huwa wanaingia kwenye mahusiano kwa nia na sababu tofauti kila siku na sio wote wanataka mahusiano yatakayo dumu kama Wewe. Sasa kama tayari upo kwenye mahusiano au unatamani kuingia kwenye mahusiano na unataka mahusiano hayo yadumu basi haya hapa mambo 14 ambayo ukiyafanyia kazi basi yatakuwa na mchango mkubwa katika kudumisha mahusiano yako..
Pendaneni au kwa lugha nyepesi mpende kwa upendo wa kweli mpenzi wako pia muonyeshe pamoja na kumwambia. Inawezekana Wewe kuongea sana sio hulka yako basi tumia lugha ya vitendo ambayo ndiyo ina nguvu zaidi.
Uongo mwiko; hakuna kitu kinaumiza kama ukijua umedanganywa si ndio eeh, sasa basi jitahidi kwa kadri unavyoweza kuufanya ukweli kuwa ndio msingi wa mahusiano yako. Unajua wahenga waliwahi kusema kuwa ‘Njia ya muongo ni fupi’ na hawa kukosea niamini Mimi.
Kama kuna tatizo liseme wazi, usitegemee mwenzio afahamu tu- hii tabia ipo sana kwa wanawake na baadhi ya wanaume. Mwenzio akikukosea au akikukwaza mwambie, ukikaa kimya unakuwa unaanza kujenga chuko dhidi ya mwenzio ndani yako mdogo mdogo bila kujua. Jiwekeeni utaratibu wa kuto kulala mkiwa na ugomvi, sulusheni ndio mlale kesho mkiamka ni siku mpya yenye furaha mpya.
Unapo mwomba mwenzio msamaha maanisha.
Usiongelee ma-ex wako- fikiria kama kila mmoja wenu akianza kumuongelea ex wake katika hayo mahusiano, unafikiri upendo utabaki kweli hapo.
Jali hisia za mpenzi wako.
Usihangaike kuwa mkalifu (perfect) Wewe jiwekeze zaidi katika kuwa mtu sahihi kwa mpenzi wako.
Kiburi sio sifa huwa kinaua mahusiano mengi zaidi hivyo hakikisha huwi mtu mwenye sifa hiyo kwa mpenzi wako.
Usilinganishe mahusiano yenu au usimlinganishe mpenzi wako na mtu mwingine.
Usiongelee kuhusu kuachana - huna nia ya kuachana naye kwanini basi uongelee kuhusu kitu hicho? (We mtu mzima ujue) Usipande mbegu ambayoo hauko tayari kuvuna mazao yake.
Mawasiliano baina yenu ndio moyo wa mahusiano yenu, sio lazima ianze meseji au simu yake kila siku, asipotuma au ukiwahi kuamka kama hamuishi wote mcheki (atafurahi huyo na atajua kuwa una mjali)
Unapokuwa mpokeaji kumbuka kuwa mtoaji pia- iko hivi hakuna asiyependa kupokea, kama kila siku anatoa yeye tu ipo siku atachoka, jitahidi na Wewe uwe mtoaji.
Uwe mwepesi wa kusamehe na kusahau — unaweka rekodi ya alichofanya miaka 7 nyuma kwanini alafu kila mkikwaruzana unakisema kwani Wewe ni mtunza rekodi? Na yeye akikufanyia hivyo utajisikiaje? Asee
Msikilize mpenzi wako — hapa siongelei ile kuambiana kuwa nisaidie kukunja nguo, naongelea ile mpenzi amekuja ana mambo yana mtatiza kichwani na anahitaji tu mtu wa kumsikiliza ili ayatoe ya moyoni basi msikilize.
Unaona sasa ili mahusiano yaweze kudumu hayahitaji mbwembwe nyingi sana bali yanahita mtu kama Wewe ambaye tayari una nia ya dhati ya kuyafanya yadumu kwa kufanyia kazi mambo haya niliyo ainisha hapo juu.
Hizi hapa njia 25 za Kumwambia Mpenzi wako Nakupenda
Jumapili ya juzi tarehe 28/7 nilikwenda kumsalimia rafiki yangu mmoja, ambaye tumezoeana sana. Baada ya salamu, alinikaribisha chakula na kinywaji alichokuwa ameniandalia maana anajua Mimi ili nikae bila kulalamika basi msosi uwepo pamoja na Coca cola bariiidi.
Baada ya kumaliza kula nikamshukuru kwa chakula maana kilikuwa kitamu kweli kweli, alipika pilau ya kuku na kachumbari moja matata sana. Sasa katika kuanza kupiga stori zetu za hapa na pale kama marafiki wafanyavyo akanigusia suala la mahusiano yake na hapo ndipo nilipopata wazo la kuandika uzi huu.
Rafiki yangu alikuwa ana lalamika kuwa mpenzi wake ni mgumu sana kusema neno Nakupenda, na yeye anapenda kumsikia akimwambia (usishangae kwani mara nyingi wanawake hupenda kuambiwa na wapenzi wao Nakupenda mara kwa mara, kwao ni kama uthibitisho). Alilalamika sana mpaka kufikia hatua ya kusema anahisi mpenzi wake amemchoka. Ikabidi nimuulize kwani anapokuwa hapa nyumbani siku za mwisho wa wiki hali uwa ikoje?na ni vitu gani huwa anapendelea kufanya au ni nini huwa anamfanyia? Akaorodhesha mambo mengi sana, na hao ndipo nilipopata kufahamu kuwa huyu rafiki yangu bado hajaielewa vyema lugha anayoitumia mpenzi wake kumwambia anampenda.
Kama rafiki ninayejali nikwambia, shemeji yangu anakupenda na leo nataka nikuelekeze njia 25 ambazo ukizizingatia utaona kwa macho yako kuwa huwa anakwambia anakupenda kila siku. Waswahili huwa wanasema kizuri kula na ndugu yako, sasa ili na wewe usisahau hakikisha unaziandika chini njia hizi 25 na moja ya nyongeza ili usije ukazisahau na hakikisha unaizingatia namba 19 kwani ni ya muhimu zaidi.
Njia 25 za Kumwambia Mpenzi wako Nakupenda
Nimekutengenezea list ya miziki unayopenda
Nina zawadi yako
Nimekutayarishia/Nimekupikia chakula unachopenda
Wewe ni mtu muhimu sana kwangu
Natamani ungekuwepo
Nilipita mahali nikaiona hii na nikakufikiria
Huu wimbo unanifanya nikukumbuke kila ninapousikia
Wewe ni wa kipekee sana
Namis tabasamu lako/kicheko chako
Nina mengi ya kukwambia jinsi siku/safari yangu ilivyokuwa
Unafanya maisha yangu yawe ya amani na furaha
Nina jivunia kuwa na wewe
Unanipa sana moyo mpaka najiona naweza kila kitu
Nimekuletea kinywaji chako unachopenda
Mimi ni shabiki yako namba moja
Nimemis kula chakula chako
Mimi ni wako
Nikueletee nini nikirudi
Ninakuthamini sana
Ninamshukuru Mungu kwa ajili yako
Unanipa amani
Napenda jinsi ninavyojisikia kila ninapokuwa na Wewe
Napenda kukuona ukiwa na furaha
Nitumie meseji ukifika/utakapofika
Nakuhitaji
Nipo kwa ajili yako
Ili mahusiano yaendelee kunoga ni muhimu kuambiana maneno mazuri ambayo hata mtu akiwa amekaa peke yake akikumbuka anakuwa anatabasamu mwenyewe na kuendelea kukuwaza wewe tu.
Ni matumaini yangu uzi huu utakusaidia na Wewe kwa namna moja au nyingine kuweza kubaini njia tofauti ambazo mpenzi wako amekuwa akitumia kukwambia anakupenda bila kusema Nakupenda.
Nafahamu unataka sana kujua ni vitu gani ambavyo vinamfanya mtu awe boyfriend bora kwa mpenzi wake. Zipo sifa nyingi na hapa nimeziandika kwa uchache ambazo ni muhimu. Inaeleweka kuwa boyfriend sio kazi rahisi hasa nyakati hizi ambazo binadamu wengi wamekumbwa na ugonjwa wa kupenda kujilinganisha na wengine. Hii inachangia migogoro mingi katika mahusiano hasa kama ukikutana na mtu ambae anategemea mambo makubwa kutoka kwako. Pamoja na yote hayo wewe kama boyfriend inakupasa kuendelea kuishi katika uhalisia wako na kufanya vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wako.
Bila kupoteza muda zifahamu Sifa za Boyfriend Bora:
Mstaarabu
Nadhani unaelewa maana ya kuwa mwanaume mstaarabu. Usitake mambo yaende kwa jinsi utakavyo wewe tu jali na yeye anataka nini. Vile ambavyo ungependa mpenzi wako akutendee na wewe mtendee vivyo hivyo. Usiwe usumbufu.
2. Jithamini na kujijali.
Hakuna msichana anapenda mvulana aliye shaghala bagala atakutambulisha vipi kwa rafiki zake wakati uko rafu?🙄
3. Usiwe na tabia za kitoto
Mwanamke anapenda mwanaume anaye jielewa zile tabia za kitoto nadhani unazijua mara umenuna wiki 2, au kila kitu unaenda kuongea na washkaji zako ziache,mapenzi si ni yenu wawili?Muonyeshe kuwa wewe ni mkomavu na unaelewa vitu unavyo vifanya.
4. Mfanye mpenzi wako siku zote ajisikie kama yeye ni msichana mrembo zaidi.
Hapa si unaelewa cha kufanya? Usitoke na mpenzi wako alafu macho yako yakawa bize kuangalia ngongingo za wanawake wengine utamfanya ajisikie vibaya. Utajisikiaje na yeye akiwa anafanya hivyo kila akiona mwanaume ambaye anavutia?
5. Achana kumuongelea ex wako kabisa.
Stori za kuhusu ex wako hazimuhusu mpenzi wako. Anaweza asikwmabie lakini hakuna msichana ambaye atakaa akusikilize unamuongelea ex wako kila siku, utaanza tu kuona mabadiliko kwenye sura yake na mwisho wa siku ataanza kukukwepa kwani kwenye akili yake wewe bado unampenda ex wako hata kama sio kweli. Muonyeshe mpenzi wako kwamba yeye ndiye mmiliki pekee wa moyo wako na mawazo hivi sasa.
6. Unapokosea Omba msamaha
Kubali kuwajibika kutokana na makosa yako. Huwezi kusema unamlaumu mpenzi wako kwa kosa ulilo lifanya wewe kwanza unawezaje🙆? Omba msamaha na fanya kila juhudi kuepuka kurudia kosa hilo tena.
7. Kuwa mkweli.
Ufanye ukweli kuwa msingi na mazoea katika mahusiano yenu.
8. Panga na mpenzi wako mipango pamoja
Mpenzi wako si ni sehemu ya maisha yako kwa sasa hivyo mhusishe na yeye katika kupanga mipango yenu pamoja. Mfanye ajihisi kuwa yeye ni sehemu muhimu katika maisha yako mshirikishe usiende tu kumpa taarifa kuwa umeamua hivi na vile.
9. Muamini mpenzi wako
Unapaswa kumwamini mpenzi wako. Usiwe na mawazo hasi kuhusu yeye au kuanza kutunga stori katika mawazo yako kumhusu bila kuwa na uthibitisho. Kama huwezi au unashindwa kumuamini ni vizuri ukamwambia au ukasitisha mahusiano kwasababu anayeumia zaidi ni wewe. Unapomuamini mfanye ajue kuwa una muamini na huna shaka nae.
10. Kuwa msikivu na Mpe moyo mpenzi wako
Maisha yamejaa stress za aina nyingi sana, mpenzi wako anapokuja kwako na na changamoto zake msikilize na mtie moyo, mara nyingi mwanamke anahitaji mtu wa kumsikiliza tu lakini ikatokea ameomba msaada wa kimawazo basi usisite kumwambia vile ambavyo unaona inafaa katika kutatua changamoto yake.
Kuna usemi niliwahi kuambiwa kuwa ikitokea uko kwenye mahusiano na mtu na ukataka kuacha nae hakikisha unamuacha vizuri zaidi ya ulivyomkuta. Yaani kama alikuwa ni mtu ambaye hawezi kujiamini basi msaidie ajiamini, kama alikuwa mwoga mfundishe kuwa jasiri.
Wewe kama boyfriend unafanyeje kuhakikisha mpenzi wako anakuwa bora zaidi ya ulivyokutana nae hata kama huna mpango wa kumuacha?
Kuna wakati inaweza ikakuwia vigumu kujua jinsi ya kumfurahisha mke wako kutokana na ukweli kwamba wanawake ni wagumu kueleweka. Lakini ni muhimu ukaelewa kuwa kila mwanamke ni tofauti na mwingine na kila mmoja ana mahitaji yake tofauti ya kihisia, kiroho, kiakili na ya kimwili.
Kuna mambo mengi ambayo wanandoa wanahitaji kutoka kwa kila mmoja ndani ya ndoa na kadiri muda unavyoenda utagundua kuwa kuna mahitaji ya kipekee ambayo mwenza wako anayohitaji kutoka kwako, mahitaji haya yanaweza kwenda yakibadilika kwani na nyie pia mnakua.
Katika mambo mengi ambayo mke wako anahitaji kutoka kwako haya 4 ndiyo ya muhimu zaidi.
1.Heshima
Mke wako anahitaji na anatamani heshimu siku zote kutoka kwako. Hii inamaanisha utambue thamani ya mke wako wako na kutojaribu kumvunjia heshima hiyo mkiwa wote au mkiwa mbele za watu kwa kutumia maneno au matendo yako. Ukimheshimu mke wako hata wale wanaowazunguka kana ndugu, majirani na marafiki nao watamheshimu. Usiruhusu mtu amwongelee vibaya mkeo na wewe ukiwepo, kumkosea mkeo heshima ni sawa na wewe kukosewa heshima nyie ni mwili mmoja.
Njia nyingine ya kumpa mke wako heshima ni kwa kusikiliza mawazo au maoni yake pamoja na kuthamini mapendekezo yake.
2.Ukaribu na Wewe.
Mke wako anataka kujisikia kuwa yuko karibu zaidi na wewe kuliko mtu mwingine uko nje, ukaribu ambao ni zaidi ya ule wa kimwili wa kushiriki tendo . Anataka uhusiano wenu uwe wa ndani zaidi nikimaanisha ajihisi kwamba mume wangu hata apitie tatizo gani huko nje ataniambia ukweli bila kunificha chochote. Hiki ni kipengele kigumu kwa baadhi ya wanaume kwani wengi wamekuzwa wakiambiwa kuwa mwanaume ni kuwa na kifua na mkeo hatakiwi kujua kila kitu. Hii huleta shida kubwa sana kwenye ndoa nyingi.
Wewe sasa unaweza kuboresha ukaribu wako na mkeo kwa kuanza kuwa mnazungumza mara kwa mara ambapo mtakuwa mkishirikishana kwa uwazi kila kitu, hii itakusaidia hata uko mbeleni likitokea tatizo mke wako atajua mahali pa kuanzia. Mshirikishe mkeo kuhusu matatizo yako na mapambano yako. Kuanzia maswala ambayo unayaona madogo kazini hadi makubwa zaidi. Unapoanza kumshiriki mke wako sio tu itaimarisha ndoa yako, lakini itakusaidia afya yako ya akili pia na kukupunguzia msongo wa mawazo.
3 Anahitaji Umakini wako (attention)
Sio kwamba mkeo hatambui kwamba upo bize na kazi zako anaelewa sana lakini hiyo haizuii yeye kutamani umakini wako kwake au kwa yale ambayo anakufanyia. Mfano: Mke wako amesuka nywele vizuri au kavaa kapendeza inabidi umsifie kwamba kapendeza na anavutia. Inawezekana na pia amekupikia chakula kitamu msifie kuwa leo mke wangu chakula kitamu sana. Hii itamuonyesha kuwa kumbe unaniona na unajua ninacho kifanya, mbona wakati mnaanza mahusiano ulikuwa unamwagia sifa nyingi? Zimeishia wapi?
Mke wako anapokuwa anaongea na wewe msikilize kwa kumwangalia machoni na sio kwenye simu yako au TV jitahidi uwe msikilizaji bora.
4.Anataka umwonyeshe Mapenzi
Hitaji kubwa la mkeo ni kuonyeshwa upendo na kwa mume wake. Mara nyingi sana utasikia mke ana muuliza munewe unanipenda kweli? Ni vizuri basi ukahakikisha hitaji hili la mke wako unalitimiza bila ya yeye kuanza kukuuliza maswali mengi. Kuna njia tofauti za kumwoyesha upendo mkeo ingawa mara nyingi watu huwa tunafikiria upendo ni kumridhisha kimwili au kumnunulia zawadi ni zaidi ya hapo. Ni vitu vidogo vidogo kama kumkumbatia, kumshika mkono mkiwa mnatembea,kumbusu, kumwacha apumzike zaidi siku za weekend na wewe ukamsaidia kazi za ndani. Ni muhimu wewe kufahamu ni namna gani au vitu gani vinamfanya mke wako aweze kuhisi na kujua kwamba unampenda. Matendo na maneno yako unapokuwa unamwambia mkeo kuwa unampenda hakikisha vinaendana.
Je, ni mangapi hapa unampatia mke wako kila siku?
Je Unazifahamu Sifa 10 Za Mke Mwema?
Kuna baadhi ya sifa ambazo karibu kila mwanaume huzitafuta kwa mwanamke ambaye hutamani kutulia naye na kujenga nae maisha. Msichana anaweza kudhani kwamba mwanaume anapokuwa anatafuta mke basi ataangalia sura, au shepu au urembo wake lakini ambacho hajui ni kuwa mwanaume hivyo havizingatii sana kwani anachotaka mwanaume ni mtu ambaye atakuwa nae bega kwa bega katika kujenga familia na kutimiza ndoto zao binafsi na zile za familia yao.
Ili kukusaidia kufahamu vizuri zaidi juu ya kile ambacho wanaume wengi hutafuta katika wenzi wao wa maisha, hapo chini nimekuorodheshea sifa 10 zinazomfanya mwanamke kuwa mke mwema. Hizi nilizo andika hapa ni sifa chache ambazo zinaweza kukusaidia kuwa mke mwema.
Sifa Za Mke Mwema
1. Humwonyesha Mume wake Upendo
Je! unampenda mume wako? unajisikia furaha na amani unapokuwa naye?
Kama utakuwa uliridhia mwenyewe kuolewa na mume wako ina maana kuwa unampenda si ndio? Lakini kumpenda peke yake haitoshi bila ya Wewe kumwonyesha upendo huo kwa vitendo.
Unaweza kumwonyesha upendo wako kwa kumbusu, kumkumbatia, kumpikia chakula anachokipenda, kuangalia mechi ya mpira ya timu anayoipenda au kuangalia movie pamoja. Vitu ambavyo unaweza kumfanyia kumwonyesha kuwa unampenda ni vingi sana na pia usiache kumwambia unampenda.
2. Ni Msaada Kwa Mumewe
Hakuna mwanaume anapenda mwanamke ambae atakuwa mzigo kwenye maisha yake. Kama mwanamke kwa namna yoyote ile hata kama hutaweza kumsaidia atakapokuwa amekwama kifedha basi msaidie hata kwa mawazo. Mume wako atakapokuwa na hofu msaidie kwa kumpa tumaini, akija kwako na wazo la biashara msaidie mawazo ya jinsi atakavyoweza kulifanikisha na kama hufahamu cha kusema kwa wakati huo mwambie nipe muda nitafakari nitakujibu kisha ingia google tafuta mawazo huko.
3. Ana Heshima
Ndoa nzuri ni ile ambayo wanandoa wanaheshimiana. Mumeo ni binadamu ana mapungufu yake kama ambavyo wewe unayo ya kwako. Basi ukilitambua hilo inakupasa kumheshimu, na mwanaume anapenda kuheshimiwa awe nacho au asiwe nacho. Usiseme tu unamheshimu mumeo inakupasa kuionyesha heshima ukiwa ndani ya nyumba yenu au nje. Heshimu juhudi zake anazo zifanya kwa ajili ya familia yenu hufahamu ni mishale mingapi anaikwepa ili mpate kula kunywa na kuvaa. Mumeo unatakiwa umsitiri na sio kumwaibisha au kumdarilisha mbele za watu au ndugu.
4. Ni Msikivu
Usiwe mtu mwenye papara ya kuongea, jenga tabia ya kusikiliza zaidi ya unavyo ongea kwani utajifunza mengi sana pale unapokuwa unasikiliza. Nadhani umeshawahi kusikia mtu anaambiwa “msikilize mumeo". Ni muhimu sio tu kusikiliza anachoongea bali pia uelewe anachokisema. Mumeo anapokuita muongee kama unatumia simu iweke simu yako pembeni na sauti uitoe, kama una angalia TV au kusikiliza Redio uache kwanza ukamsikilize, hii ni moja ya njia ya kumuonyesha una mheshimu na uko tayari kumsikiliza kwani utakuwa umempa umakini wako wote.
5.Ana Shukrani
Kuwa mke mwenye shukrani kwa mumeo, kwani mwanaume kama binadamu mwingine na yeye anapenda kupendwa, kuthaminiwa, kusifiwa na kuonyeshwa kujali.
Mumeo anapofanya kitu au anaporudi ameleta kitu mshukuru hata kama ni nyama au mchele hata kipande cha sabuni mshukuru kwa hilo. Usisubiri mpaka afanye makubwa ndio useme asante. Unapomshukuru unamtia moyo na yeye kuendelea kutafuta zaidi kwani ndani yake anajua kuwa unathamini hata hicho kidogo anachofanya. Na nikupe siri siku zote unapokuwa unamsifia mumeo unamuongezea ari na kumtis moyo wa kufanya zaidi. Unapomsifia au kumshukuru kwa anachokifanya ni sawa kunamwambia mume wangu juhudi zako naziona, nazitambua na kuzithamini. Usiache kusema Asante Mume wangu.
6. Ni Mwaminifu
Mnapo aminiana kama wanandoa mnajenga uhusiano madhubuti. Uaminifu ukikosekana hata kidogo basi mahusiano huwa yanayumba. Ni vyema basi mahusiano yenu ukahakikisha mnayajenga katika msingi wa kuaminiana. Mumeo anatakiwa akuamini, na usiwe na ule uaminifu wa kufeki uwe ni ule ambao hata akija kuambiwa mkeo amefanya hivi au vile akatae aseme huyo mnayemsema sio mke wangu kwasababu Mimi wa kwangu namjua. Kwahiyo kama mke inakupasa kuwa muaminifu na mkweli kwa mumeo. Kumbuka uongo au usaliti utaweka doa ambalo halitafutika moyoni mwake.
7. Hapendi Kugombana Hovyo
Hivi unajua kuwa hakuna wanandoa wowote ambao hawagombani?Ndoa inakutanisha watu wawili tofauti,waliolelewa tofauti na wanaofikiria tofauti yaani vitu huwa ni tofauti tofauti ingawa vipo vitakavyo kuwa vinafanana. Utofauti huo wa baadhi ya vitu kuna wakati unaweza ukasababisha mikwaruzano ndani na iwapo itatokea malumbano yakazidi basi lazima uhusiano wao utayumba. Hii inamanishi kwamba kama mke mwema inakupasa kuelewa sio kila kitu lazima mgombane na hata ikitokea mnagombana basi ufahamu kuwa hutakiwi kugombana na mumeo na kumuona kama adui la hasha unatakiwa umsaidie mumeo kutafutia ufumbuzi wa hicho kitu kilichowafanya mgombane. Nyie wawili ni timu moja na sio mahasimu. Usiruhusu nyumba yako ikakosa amani kwa vitu ambavyo hata wewe mwenyewe unaweza kuvitafutia ufumbuzi.
8. Ni Rafiki Wa Mume Wake
Wanandoa wakiwa ni marafiki walioshibana hiyo ndoa itaishi miaka milioni. Hakuna kitu kilicho kizuri kama wanandoa ambao msingi wa uhusiano wao ni urafiki, kwasababu hata wapitiw changamoto ipi wanao uwezo mkubwa sana wa kuimaliza hiyo changamoto pamoja kwa amani. Upendo unakuwa una nguvu baina yao. Jitahidi umfanye mumeo awe rafiki yako tena besti frendi wa kupiga nae umbea (alafu hakuna watu wambea kama wanandoa loh🤗)
Jitahidi kujenga sana urafiki wenye afya na mumeo na utaona aina ya tofauti wa mahusiano baina yenu itakayoleta maishani mwako.
9. Ni Mdadisi
Hapa siongelei kufukua fukua yasiyokuhusu au kutafuta habari zake na kumfuatilia kama kupe. Ukianza hizi tabia ujue kuna mahali wewe unatatizo.
Sio kila kitu ambacho mume wako anapenda au anafanya kinaweza kuwa kukuvutia, hapa inaweza kuwa kazi zake au vile vitu anapenda kufanya tofauti na kazi zake. Lakini unaweza ukaonyesha udadisi kwa kumuuliza kuhusu hicho anachokifanya mfano mwambie akuelezee kuhusu kazi yake, au kama ni shughuli nyingine mwambie akuelezee utashangaa jinsi ambavyo utaweza kujifunza na kuelewa. Jijengee tabia ya kupende kujua na kujifunza vitu kwani inaweza kukupelekea sio tu kufahamu bali pia ukavutiwa nacho alafu ikaibua nafasi ya mazungumzo au kitu mnachoweza kufanya pamoja.
10. Anaonyesha Mahaba
Sidhani kama ulifikiri sita liongelea hili. Ngoja nikwambie ndoa ambayo haina mahaba huwa na misukosuko mingi. Yaani nyie ni wanandoa ila mnakuwa mnaishi kama wapangaji ndani eti kisa mna watoto Weee🙄.
Mke swala la mahaba alitakiwi kupotea baina yenu mbona wakati mnaanza lilikuwepo? Lirudishe usingojee yeye aseme leo nina hamu na wewe, anza wewe kumwambia arudi mapema una shughuli nae maalum chumbani uone kama hajaacha bia mezani. Unapoona mapenzi yameanza kukauka chukua hatua mapema yarudishe anza kwa kumpapasa mkiwa wote mmekaa mnaangalia tv, mkumbatie kwa mahaba, mbusu au mkonyeze. Mapenzi hayatakiwi kukauka baina yenu kama yalikuwepo mwanzo basi yanapaswa kuendelea kuwepo.
Ndoa ni kuheshimiana,kuthaminiana, kujaliana, kuelewana, kusikilizana, kupendana na hivyo ukitaka kupata mume mwema ni lazima kwanza uwe tayari kuwa mke mwema.
Una lolote la kuongezea?Niandikie hapo chini.
Ulishawahi kushika simu yako ukiwa na lengo la kumtumia mpenzi wako meseji lakini hujui uandike kitu gani unaishia tu kuandika “Vipi umeshakula?”yaani hapo hata Wewe mwenyewe lazima ujione sio, na yeye kule akiisoma ataishia kuzingusha macho juu na kusema huyu nae maswali gani sasa haya yaani amekosa maneno ya kuandika? Upo hapo?
Naelewa hakuna mtu ambae hapendi kumwandikia mpenzi wake meseji nzuri ya kuvutia, lakini shida inakuja mara nyingi hujui uanzie wapi au useme nini na wakati huo huo unataka uonekane wa kiutofauti kwa mpenzi wako. Inakera hiyo kitu acha tu. Unataka kutuma meseji ili mchat kidogo lakini ukifikiria nitamchokozaje ili aweze kujibu unaishia kuweka simu chini au kuingia twitter kuangalia leo vayolensi iko mtaa upi au uingie Instagram uangalie habari mpya. Hizo nyakati mwisho ni leo hii usomapo hapa.
Sasa leo nataka nikwambie umefikia mwisho wa tatizo lako, hapo chini nimekuorodheshea meseji 25 ambazo ukimtumia mpenzi wako lazima huko aliko afurahi na tabasamu juu na hata kama alikuwa hapendi kuchat na Wewe utashangaa jinsi atakavyokuwa na moto wa kupenda na kuendelea kuchat na Wewe kila siku.
1. Wewe ndiye mwenye ufunguo wa moyo wangu nakupenda sana.
2. Kila napokuwa naangalia macho yako mazuri huwa najiona Mimi ni mtu mwenye bahati sana kuwa nawe.
3. Wewe ni mrembo, mtulivu, mpole, myenyekevu na mwaminifu. Hakika nimependelewa na Mungu kuwa na Wewe maishani mwangu. Nakupenda sana.
4.Upendo wako umeleta furaha maishani mwangu na ndani ya moyo wangu.
5. Umeifanya dunia yangu kuwa mahali pa furaha kwa sababu uko ndani yake. Umeigusa nafsi yangu kwa njia ambazo maneno hayawezi kuelezea.
6. Toka siku ya kwanza nilipokuona nilivutiwa na wewe, tabasamu lako, uzuri wako, akili yako. Moyo wangu, roho yangu, na mwili wangu vyote ni vyako Mimi ni wako kabisa Nakupenda sana.
7.Kukupenda ni jambo rahisi zaidi ambalo nimewahi kufanya katika maisha yangu na ni jambo ambalo ningependa kuendelea kulifanya maisha yangu yote.
8.Muda/Miaka ambayo tumekuwa sote imebadilisha mambo mengi sana, lakini jambo ambalo halijabadikika ni jinsi ninavyojisikia kila ninapokuwa karibu na wewe ni huwa najiona ni kama ndio kwanza tunaanza uhusiano wetu.
9.Moyo wangu najua uko salama mikononi mwako mpenzi wangu.
10.Baada ya miaka hii yote ya kuwa pamoja nataka ufahamu kuwa bado unawasha moto ndani yangu ambao ni wewe tu unayeweza kuuzima.
10.Sijawahi kujuta hata dakika moja ya kuwa na wewe katika maisha yangu.
11. Wewe ni kipenzi cha moyo wangu na nuru ya maisha yangu. Wewe ni wa thamani zaidi kwangu kuliko kitu chochote au mtu mwingine yeyote, na nitakuthamini milele.
12. Kila siku ninapoamka na kukuona wewe pembeni yangu huwa najihisi kama nipo ndotoni , ndoto nzuri ambayo kamwe sitaki kuamka kutoka katika huo usingizi. I love you
13. Umenipa kitu muhimu sana ambacho pesa haiwezi kununua, Upendo usio na kipimo.
14. Nazidi kukupenda zaidi kila siku inayoitwa leo na nionapo tabasamu lako ndio unanimaliza kabisa.
15. Umefanya maisha yangu kuwa ya thamani zaidi kuliko nilivyowahi kufikiri hapo mwanzo. Umeniongezea vitu vingi maishani mwangu.
16.Upendo wako umekuwa ndio msukumo wangu wa ndani, motisha yangu, na chanzo cha faraja yangu. Kadiri Navyoendelea kuwa na wewe pembeni yangu, ninajihisi kuwa naweza kufanya chochote, sina hofu tena kwa sababu najua ninao upendo na msaada wako siku zote. Nakupenda
17. Kila unapokuwa mbali na Mimi huwa siwezi kuacha kukufikiria na kutamani urudi ili nikishike tena mikononi mwangu .
18. Umeleta nuru katika maisha yangu na kila siku unanipa nguvu ya kusonga mbele zaidi, asante sana kwa upendo wako kwangu.
19. Umenisaidia kuwa mwanaume/baba bora kwa kila sekunde ambayo umekuwa pembeni yangu. Hakuna mtu ambaye anaweza kunielewa kwa jinsi unavyonielewa wewe.
20. Dunia imekuwa mahali pazuri zaidi kwa sababu wewe upo. Mpenzi wangu wewe ni wa kipekee sana. Natamani ujione kupitia haya macho yangu ya upendo. Mapungufu yako sio kitu na yasikuzuie kutimiza ndoto zako.
21. Upendo wako ndio kitu muhimu na cha thamani zaidi katika maisha yangu, siwezi kukuchukulia kikawaida au kuja kusahau jinsi nilivyo na bahati ya kuwa ya na wewe.
22. Sasa hivi siweza kufikiria maisha yangu bila wewe, ninafuraha sana kwa kuamua kunipa moyo wako, na wewe unao moyo wangu sasa na hata milele.
23.Wewe ni malkia wangu na wa moyo wangu.
24. Tangu siku ya kwanza tulipokutana, nilijua ya kuwa wewe ndiye mwanamke unayenifaa, upendo nilionao juu yako ni mkubwa zaidi ya uwezavyo kufikiria.
25. Malkia wangu wa nguvu uzuri wako, akili yako, hekima zako sio rahisi kuelezea kwa maneno.
Mapenzi ni vionjo, huitaji kuwa romantiki unachohitaji ni mpenzi wako akuone kuwa unamjali pamoja na meseji nzuri kama hizi ambazo zitaongeza vionjo na utamu kwenye mahusiano yenu. Achana na zile meseji za umekula au unarudi saa ngapi anza kumtumia mpenzi wako meseji hizi, hata kama amekununia kwa wiki nzima ukimtumia makombora ya hizi meseji utayeyusha kabisa hasira zilizokuwa ndani yake juu yako.
Kazi kwako.
Tupo katika kipindi ambacho wasichana wengi wanatafuta wanaume wa kuwaoa, kiasi cha kwamba baadhi ya wanaume wanachukilia hiyo kama fursa ya kutembea na wasichana tofauti wakiwa ahidi ndoa na mwisho wa siku wanawatafutia sababu wanawaacha. Wanawake wengi wanabaki na vidonda moyoni na wengine huwa wanafikia hatua ya kufanya vitu vya ajabu kutokana na kuumizwa.
Sasa kama na Wewe ni mmoja wa msichana ambaye unatafuta mwanaume wa kuja kufunga nae ndoa na kuanza familia pamoja leo nimekuandalia listi hii ya vigezo au ishara ambayo itakusaidia kufahamu kama uko na mwanaume sahihi.
Mwanaume yeyote ambaye anajielewa na yuko siriasi na Wewe lazima utaziona hizi tabia 21 kutoka kwake:
1. Hatojaribu kukubadilisha ili uwe jinsi anavyotaka yeye
2. Uko huru kuzungumza nae kuhusu kitu chochote bila kufikiria atakuonaje
3. Unapofikiria kuolewa nae, haufikirii sana kuhusu sherehe ya harusi bali ule muda ambao mtaanza kuishi pamoja
4. Anajitoa sana kwa ajili yako na Wewe pia unajisikia fahari na furaha kufanya hivyo pia kwa ajili yake.
5. Unaweza kulia mbele yake bila kujisikia vibaya au kuona aibu.
6. Akikwambia “Nimekumis” unajua hajasema tu bali ana maanisha kweli na hapa siongelei kufanya mapenzi🙄
7. Uko huru kupanga au kumwambia mipango yako.
8. Anakwambia mipango yake na anasikiliza ushauri unaompatia.
9. Haruhusu mtu au watu wakuvunjie heshima uwepo au usiwepo.
10. Mnaweza kuwa mbali lakini mapenzi yenu hayapungui.
11. Yupo karibu na familia yako hata kama hasaidii kifedha lakini anahakikisha kama kuna tatizo atajitahidi aweze kuitatua.
12. Ukiwa na stress zako ukija kwako anakusikiliza uongee mpaka yaishe moyoni mwako.
13. Anaheshimu mipaka yako, anakujali na kukuthamini.
14. Anakuamini na Wewe unamuamini.
15. Anakusifia mbele za watu.
16. Anapenda kuona ukiendelea mbele, atakusapoti, kiakili, kiroho hata kifedha kama anayo.
17. Anakusifia ukipendeza na anapenda kukuona unapendeza.
18. Mnafanya vitu pamoja na hakuna kati yenu anaye boreka.
19. Hata mnapopishana kauli yuko tayari myamalize kabla hamjalala ili kesho muamke mkiwa na furaha.
20. Mnaweza kukaa wawili tu mahali na kila mtu kati yenu akafurahi.
21. Anapofanya kosa anakiri na kuomba msamaha.
Hizi ni baadhi ya tu ya vigezo vya mwanaume ambaye unafaa kuolewa naye. Ila sasa na wewe unapoangalia vigezo hivi hakikisha na Wewe una tabia ambazo zitamfanya hata yeye aseme kuwa hapa nimepata mke.
Majuzi katika pita pita zangu katika mtandao mmoja, nikakutana na post ya mdada mmoja ambaye anaomba msaada wa kisheria ili aweze kutengana na Mume wake kwasababu amechoka kupigwa kila siku. Kama kawaida watu wakawa wanakomenti pale kumlaani na kumtukana yule mwanaume. Katika kusoma zile komenti sikuona hata moja ambayo inamuulize yule dada maswali magumu(labda kwasababu wengi waliokuwa wanakomenti ni wanawake)nikaishia hapo kuendelea na mambo yangu mengine.
Baadae nikaanza kutafakari tena hilo swala la huyo mdada na kwa siku mbili mfululizo nilikuwa najiuliza maswali mengi sana, mengine nikapata majibu, mengine nikayatuma kwa watu wengine ili nao waniambie majibu na mawazo yao. Baada ya kupitia majibu yote, nikagundua vitu kadhaa ambavyo wengi tunavipuuzia lakini ni vya msingi sana ila kikubwa ni kuwa kuna wakati mtu anakuwa anaogopa kujiuliza maswali magumu. Unaweza kujiuliza nina maanisha nini?
Iko hivi mahusiano ya ndoa ni tofauti sana na mahusiano ya uboifrendi na ugelofrendi 🙃. Ndoa ni muunganiko, ni kiapo,na ni maagano ambayo wawili wanayaingia mbele ya Mungu wanaye muamini kupitia imani zao na mbele ya viongozi wao wa dini na kiroho ili kwenda kuanza maisha pamoja. Kwanini unafikiri Kitendo tu cha Wewe kusema nataka kuoa au kuolewa na mtu fulani kinawafanya wakubwa wako ndani ya familia wakuulize kwanza maswali mengi?Ni kwasababu wanataka walau wa kiwango kidogo wapate kumfahamu huyo mtu hata kwa ufupi kupitia wewe ili kuweza kijiridhisha kuwa unafanya maamuzi sahihi.
Hivyo vyote vinafanyika kukusaidia Wewe ingawa hutoona hivyo kwa wakati huo lakini ndiyo iko hivyo. Maswali wanayokuuliza ni kwasababu wao wanayaishi au hata walikuwa wanayaishi hayo maisha ya ndoa hivyo wanafahamu vitu ambavyo Wewe huvifahamu, na kwasababu wanakujua nje ndani usibishe😊
Sasa nina maanisha nini ninaposema Kama hakujali Kimwili hatokujali Kiroho?
Labda nikwambie tu, mtu wako uliyenaye sasa hivi tabia zake unazifahamu fika na unajua kabisa hii tabia inaweza kuwa ngumu kwake kuacha na hii anaweza akaacha. Sasa kasumba inayo wakumba wengi (hasa wanawake) ni kufumbia macho baadhi ya tabia wakiamini kwamba tukishafunga ndoa atabadilika au nitambadilisha, pia kuna baadhi ya tabia ukiziona wewe mwenyewe unajua hii naweza kuvumilia, hii siwezi ndio maana kabla ndoa haijafungwa huwa unaulizwa Je uko tayari kuolewa na fulani?
Sasa upo kwenye mahusiano na mtu anayekupiga na hata hamjafunga ndoa ni kipi basi kinakufanya uamini kuwa ataacha mkishafunga ndoa?utambadilisha vipi mkishafunga ndoa? Umepigwa mara ya kwanza hujachukua hatua yoyote (hata kiberiti hujakitingisha)unadhani ataacha? Ngoja nikwambie unafahamu vile mtoto anavyomjaribu mzazi wake kwa kufanya kitu sasa mzazi akikaa kimya mtoto naye atasema kumbe hii ni sawa lakini mzazi akisema mtoto nae atajua kuwa hii sio sawa,ndivyo hivyo na wewe unatakiwa uwe. Usipigwe mara ya kwanza ukakaa kimya eti kisa unataka ndoa hapana, mbona yeye humpigi kama mbwa mwizi? Mjaribishe basi kumpiga kama anavyo kudunda wewe kisha muulize vipi unajisikiaje? Huo ni mwili wako inabidi hauheshimu kukutia alama au ukilema wakati kwenu alikutoa huna alama au hicho kilema sio sawa. Usiende kuingia ndani ya ndoa ambayo utaishi kwa kugugumia, kwa kujutia na kwa kulia kila siku kisa unapigwa au unafanyiwa vitendo vingine vya ajabu.
Kama ambavyo Wewe unaujali na kuupenda mwili wako ndivyo vivyo hivyo mwanaume/mume wako anatakiwa aujali pia. Na siku zote mwanaume anayeujali mwili wako atakujali na kiroho. Atakuombea, atakuwa anamshukuru na kumsifu Mungu kwa kumpatia mke ambaye ni wewe. Furaha yake ni kuona mke wake ana Amani, furaha na Afya njema, na ikitokea umeumwa utaona jinsi ambavyo anaongea na Mungu ili afya yako irudi. Na hakuna ndoa tamu kama ndoa ambayo wanandoa huombeana, huwaziana mema, hushirikiana na kujaribu kutatua tatizo pamoja na sio kumuona mwenzako ndio ana tatizo.
Hizi tabia za mwanaume wa namna hii utaziona hata kabla hamjafunga ndoa, mwanaume au mwanamke mwenye hofu ya Mungu ndani yake utamuona tu. Matendo yake yatajifunua kwako. Mema hayajifichi na mabaya huonekana fanya uchaguzi na maamuzi sahihi ili kuepuka kujutia mbele ya safari.🤗
Leo katika harakati zangu za maisha ya kila siku ili kuhakikisha naendelea kuifanya familia yangu ile, ivae vizuri na kuishi mahali salama, nikakutana na mdada mmoja kwenye bajaji ya kuchangia ana lalamika sana kwenye simu huku machozi yanamtoka.
Ndani ya bajaji tulikuwepo watu watatu tu, Mimi, Yeye na dereva ambaye naye alikuwa yuko busy na kazi yake kwahiyo hata kilichokuwa kinaendelea huku nyuma hakukijua. Wakati naendelea kumtafakari huyu dada na maneno ya uchungu ambayo alikuwa anaongea na huyu mtu mwingine wa upande wa pili kwenye simu, ghafla nikaisikia simu yangu inaita na ikanitoa kutoka katika mawazo niliyokuwa nayo kwa wakati huo.
Baada ya kumaliza kuongea na simu yangu, nikamwangalia huyo dada wa pembeni yangu ili nimsabahi nikakuta amejifunika usoni na mtandio wa kijora chake cha rangi ya chuichui alichokuwa amevaa. Nikataka nimguse bega lakini mkono wangu ukawa mzito ila kwakuwa bado alikuwa analia kwa sauti ndogo na ya chini nikajikaza na kumgusa begani. Wakati nataka kumsalimia nikashangaa maneno ambayo nilikuwa nimepanga kuanza nayo yamepotea na kuanza kumwambia moja kwa moja kuwa pole usilie sana ndoa zina changamoto sana.
Aliniangalia na kuanza kulia tena, nikaishiwa maneno na wakati natafakari nini cha kusema akaanza kuniambia yaani Mimi huyu mwanaume nimemvumilia katika mengi sana,nimemsaidia sana, nimejitoa kwake sana ila leo hii maisha yameshakaa kwenye mstari ananiambia hawezi kunioa kwasababu wazazi wake wamekwisha mtafutia mwanamke mwingine hivi kweli? Hapo mbona nilishusha pumzi kwa nguvu na nikaishiwa pozi kwasababu kwa kumwangalia tu huyu dada anaonekana ni wale wadada wapambanaji.
Baada ya ukimya kama wa dakika tano kabla sijaanza kuongea bajaji ikasimama na abiria mwingine akaingia alikuwa ni Mama mtu mzima tukamsalimia na safari ikaanza tena. Yule dada akachukua tena mtandio wake akajifunika usoni na kuanza kulia tena kwa sauti ya chini. Nikambonyeza begani na kumwambia najua una uchungu lakini je umeshajaribu kuongea nae huyu mwanaume ili upate kusikia kauli yake ya mwisho kuhusu hili swala? Akasema yaani hapa nimetoka kwake na bado anakazania kuwa ndoa na Mimi haitawezekana hawezi kwenda kinyume na matakwa ya wazazi wake.
Nimembeleleza sana na nikamkumbusha tulipotoka kwasababu tumekuwa wote kwa miaka 5, lakini amesema haiwezekani Mimi nitafute tu mtu mwingine niendelee na maisha yangu. Akasema inaniuma kwasababu nyumbani kwetu wote wanamfahamu na wanajua ndio atakuja kunioa, lakini ona sasa nitaenda kuwaambia nini wazazi na ndugu zangu?
Mara yule Mama wa makamk aliyepanda akatugeukia na kusema mwanangu si bora umshukuru Mungu badala ya kulia kwasababu kwanza hujui amekuepusha na nini huko mbele ya safari, na pili huyo hakuwa wa kwako kwasababu laiti angekuwa ni wako ambaye Mungu amekuandalia basi asingefanya hayo. Akasema hebu fikiria kama mngefunga ndoa na miaka miwili ndani ya ndoa unaanza kugundua ana mahusiano na wanawake wengine huko nje, ungejisikiaje na hapo labda una mtoto tayari?
Mshukuru Mungu hili limetokea mapema kwasababu Mungu amekwisha kuandalia mtu wako na yupo, huyo ametumika kama daraja la kukusaidia Wewe kwenda kumfikia aliye wako kiroho na kihisia. Usipoteze muda wako kulia lia unapoteza Machozi yako. Baada ya kusema hayo yule Mama akamwambia dereva wa bajaji amshushe kituo cha mbele kwani amefikia.
Baada ya yule Mama kushuka nikamwamgalia yule dada tena, nikakuta ameacha kulia na anatoa miwani yake ya jua kwenye pochi ili aivae. Kisha akaniambia huyu Mama ameniambia mambo ya msingi sana siwezi kuendelea kumlilia mtu ambae sio wa kwangu kuanzia sasa hivi nitakuwa namshukuru Mungu tu. Yote ambayo niliweza kujifunza wakati nipo naye nitayatumia katika maisha yangu, nitaendelea kupambana ili atakapokuja wa kwangu anikute nimeshajiandaa tuanzie pale ambapo kila mmoja atakuwa amefikia.
Kiukweli nilishangaa kuona mabadiliko hayo ya ghafla kutoka kwake na kabla sijasema chochote dereva wa bajaji akatugeukia na kusema tumefika mwisho wa safari naomba nauli, kila mtu akatoa nauli yake tukashuka na wote tukaendela na mishe zetu za siku hiyo. Wakati natembea nikawa nayatafakari sana maneno ya yule Mama yalikuwa ni machache lakini yaliyobeba ujumbe mkubwa ndani yake. Nikagundua kumbe ni kweli kuna wakati mtu unaweza kuwa unang'ang'ania kitu au mtu na sio wako au chako. Nikakumbuka mengi sana lakini nikajikumbusha na maneno ya yule mama kuwa mshukuru Mungu kwakuwa hujui amekuepusha na kitu gani huko mbele.
TAHADHARI:
KAMA UNA MIAKA CHINI YA 18 USISOME KILICHOANDIKWA HAPA
Ni kweli kwamba mwanamke ameumbwa kuwa na aibu na ni kitu ambacho binti pale anapovunja ungo tu anaanzwa kufundishwa. Lakini sasa hizi aibu kuna mahali hazitakiwi yaani inabidi mwanamke uziweke pembeni hasa kama uko kwenye ndoa.
Katika kuzurura kwangu huwa napata nafasi ya kuketi na wanawake tofauti na Mimi hupenda kuwauliza maswali tofauti hasa yanayohusu mambo ya ndoa na familia kwa ujumla ili nami nipate kujifunza.
Nilichogundua wengi ambao nimeweza kuzungumza nao wana mawazo fulani ya jinsi mwanamke anavyopaswa kuwa ndani ya nyumba kitu ambacho sio kibaya lakini wengi wanasahau kuwa ndani ya nyumba huwa kuna kitu kinaitwa Chumbani kwa Mke na Mume.
Kuna baadhi ya wanawake wanawaonea aibu mpaka waume zao wakiwa chumbani wanashindwa kusema kitu anachotaka. Anaweka kimitego mwanaume ukute ameshachoka na mizinguko ya siku nzima anakuwa hakuelewi unaishia kununa,sasa ukishindwa kusema Mumeo atajuaje?
Ngoja sasa nikwambia Mambo ambayo wanawake wengi wanashindwa kuwaambia waume zao.
Nataka Kufanya mapenzi na wewe Leo
Katika wanawake 10 basi ni 2 au 3 tu ndio wanaoweza kuzungumza hivi mbele ya waume zao. Wengi wanafikiri wataonekana ni wahuni au malaya, lakini sio kweli kwasababu huyo ni mumeo na moja ya jukumu lake ndani ya ndoa yenu ni kukuridhisha kinwili sasa ukishindwa kusema na kutegemea mpaka aanze yeye kama umezidiwa na hamu yeye atajuaje?Unajua mwanaume ni kiumbe ambaye hapendi kupindisha kona nyingi kama anataka mchezo atakwambia tu basi na wewe nwambie ni mume wako.
Leo hujanifikisha kileleni hili nalo huwa ni tatizo wengi hapa hawaongei kabisa eti wanaogopa kuwaudhi waume zao. Wewe unajua kuna wakati vikizidi ndio unakutana na mtu ana visirani havishikiki. Ni haki yako kufika kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.
Huwa nafurahi ukinishika hivi au vile au hapa na pale wakati wa tendo.
Ukiwa ndani ya chumba chako na mume wako aibu zako ziache mlangoni na uzifungie nje humo ndani ni kufurahishana nafsi na kama unashindwa kumwambia kwa mdomo mtumie meseji. Na kuongea na mume wako kuhusu mambo haya sio umalaya au uhuni, inatakiwa iwe kitu cha kawaida baina yenu unafikiri kwanini nyumba ndogo haziishi kwasababu wengi wao wanafahamu kuna sheria za subuleni na sheria za chumbani na ukiwa mbele ya mwanaume aibu na haya zako zifungie kabatini furahia maisha.