Stories by Tito Magoti on Medium
Hivi karibuni nimemkumbuka sana rafiki na kaka yangu Emmanuel ‘Magesa’ Gamba. Magesa aliaga dunia April 2019 kwa ugonjwa wa homa ya ini. Tulifahamu kwa kuchelewa. Kwahiyo, bahati mbaya, Magesa asingepona.
Nilivunjika moyo Daktari aliponiambia: “kama [Magesa] ana lifetime projects akamilishe ndani ya miezi sita”. Mwezi mmoja baadaye Magesa alifariki.
Chumba cha historia ya maisha ya Magesa kina mafunzo mengi. Rafiki zake na ndugu zetu wanakiri ‘Magesa alikuwa ni shule hai ya udugu, ujamaa, ushirika, na zaidi’.
Mimi na Magesa tukiwa Mbagala katika msiba wa mjomba, Mzee Kaunda, mwaka 2018
Magesa aliondoka ndugu zake tukiwa katika hatua za awali za kuelewa kwanini tuko duniani. Sio tu kuishi, bali kuyagusa maisha ya wengine na wakwetu. Magesa aliyafanya hayo kwa vitendo. Ninasikitika ndoto zake kubwa zilizima ghafla.
Leo ninamshukuru Mungu kwa kuongeza umri. Ninautenga umri huu uwe maalum kwa Magesa. Ninaomba M/Mungu anijaalie kuuishi uungwana wa Magesa.
Keep resting in paradise, Dawg!
Mheshimiwa Waziri Mkuu,
Nakuandikia barua ya wazi kwa heshima kubwa sana!
Ni mwaka wa saba tangu uwe Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CEO JMT hapa chini). Kuna mambo mengi unayojivunia. Pengine ndio maana umedumu katika nafasi yako hadi sasa.
Lakini Mheshimiwa, umewahi kujiuliza wananchi wanasemaje kuhusu utendaji wako kama Waziri Mkuu? Je, umewahi kutathmini umuhimu wa nafasi yako, unachofanya dhidi ya ufanisi unaotarajiwa?
Mhe Waziri Mkuu, bila mpangilio, niruhusu nikukumbushe yafuatayo:
Mwaka 2018 watu zaidi ya 130 walifariki katika ajali ya MV Nyerere, Ukerewe. Ukiwa CEO wa JMT, ulisitisha uokoaji kwakuwa giza liliingia. Serikali ikaenda kulala. Lakini Wananchi walipanda mitumbwi wakawasha ‘karabai’ zao kwenda kuwatafuta na kuwaokoa ndugu zao. Serikali ilikwenda kulala kwa udhuru wa giza, kana kwamba hilo lingesitisha maafa hata kwa nukta moja. Uliunda Tume. Ripoti unayo. Hakuna aliyewajibika.
Nov ‘22, ukiwa CEO JTM, ndege (Precision Air) imepata ajali ziwa Viktoria, Bukoba. Badala ya kuharakisha kuokoa uhai wa abiria, wewe na Serikali yako yote mliamua kuwapa adhabu ya kifo kwa uzembe na kutojali. Watu 19 walikufa kikatili huku wakitarajia msaada wako.
Ni kweli na inasikitisha kwamba haukujali hata kidogo. Uliendelea na shughuli zako. Baadaye sana ukaenda Kagera kupiga picha na manusura wa ajali. Na kusimamia mazishi. Ulionesha utayari na mamlaka katika kusimamia ‘sherehe ya mazishi’ kuliko kuokoa maisha ya watu. Ni sahihi kusema kwamba, ukiwa CEO JMT, kwa uzembe na kutojali, uliruhusu maisha ya watu 19 yadhulumiwe. Inasikitisha!
Ndege ya shirika la Precision Air ikiwa imezama ndani ya ziwa Viktoria, Kegera.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, sio hayo tu!
Mlima Kilimanjaro umeriporiwa kuungua moto majuzi. Haukuitikia tukio hilo kwa wakati. Kuna haja ya kuliandikia UNESCO kuhusu uzembe huu unaojirudia.
Sept 2022 Polisi waliua raia watatu nyumbani kwetu Mara. Pia walimdhalilisha kingono binti mmoja kwa kumvua nguo wakimtaka afanya mapenzi na baba yake aliyevuliwa nguo vilevile. Binti yuko wapi? Serikali ambayo wewe ni CEO wake imefanya nini kando ya ule mzaha wa polisi?
Jan 2022 mfanyabiashara wa madini aliuliwa na Polisi Mtwara. Uliunda Tume. Ripoti yake haijulikani ilipo. Zipo taarifa kuwa makachero waliofunguliwa kesi watakuwa huru, ni suala la muda. Ripoti iko wapi. Nini kimefanyika zaidi?
Mheshimiwa Waziri Mkuu,
Una mamlaka makubwa sana kama CEO JMT. Lakini umekuwa ukitoa maagizo mengi ambayo ni maigizo. Mazingaombwe! Ni maigizo kwakuwa hayatekelezwi kwa vitendo. Kauli zako hazipewi uzito wowote, nikwambie ukweli.
Tangu uwe CEO JMT, umeunda Tume nyingi sana. Ni mara chache utasikia ama kuona Ripoti ya Tume hii ama ile imewekwa wazi kwa umma kusoma na kushiriki utekelezaji. Maagizo yako yanakuwa maigizo kwa mtindo huu.
Machi 2021, wakati wananchi wanamtafuta kiongozi wao, ulilitangazia Taifa kuwa Rais Magufuli ni mzima anachapa kazi. Ulisema ukiwa msikitini. Kumbe Rais alikuwa mgonjwa mahututi. Ukikumbuka tukio hili huwa unajiambia nini?
Mwaka 2016/20 mlitangazia vita ya kiuchumi. Sheria za ulinzi wa rasilimali zikaandikwa ghafla. Mkawaweka wafanyabiashara jela. Mkaunda Tume. Mkaanzisha kampuni ya madini. Juzi mmekiri sehemu ya ulaghai mliofanya katika vita ya kiuchumi. Baadhi ya sheria mmerekebisha. Ulikuwa CEO JMT na bado unadumu.
Profesa Kabudi akikiri kwamba vita ya kiuchumi ilikuwa ni ulaghai
Mwaka 2018/19 na kuendelea, ukiwa CEO JMT, ulishuhudia serikali yako ikifanya dhuluma dhidi ya wakulima wa zao la korosho. Biashara ya korosho hadi leo ni mazingaombwe matupu.
Mwaka 2019 kulitokea tetemeko la ardhi Kagera. Hakuna jambo la maana linalokumbukwa zaidi ya matumizi mabaya fedha za waathirika na kauli za kizembe kama: ‘sikuleta tetemeko,’ na nyingine za ajabu. Ulikuwa CEO JMT.
Tangu 2015 mmetunga Sheria lukuki kwa hati ya dharura. Sheria nyingi zinazobana ufurahiwaji wa haki za kisiasa na kiraia na kiuchumi. Mmeweka rekodi ya kuwa Serikali iliyotunga na kurekebisha baadhi ya sheria hizohizo ndani ya muda mfupi. Ukiwa CEO JMT, jiulize, mlibeba maslahi ya nani?
Ukiwa CEO JMT, maelfu wametupwa jela kwa kesi za uongo. Wapo waliotekwa, walioteswa na kupewa ulemavu wa kudumu. Kuna waliouwawa kikatili. Kuna waliofutiwa kesi baada ya kukaa jela muda mrefu. Yamefanyika ukiwa CEO JMT. Sijawahi kukusikia ukiomba radhi, kujuta ama kuhofia.
Ukiwa CEO JMT, wananchi wengi wamepotezwa. Hawajulikani walipo. Wamo wakosoaji wa serikali. Haujawahi kujishughulisha kuwatafuta ama kuomba msaada wa kuwatafuta.
Sep 2017, Wakili Mwandamizi Tundu Lissu alipigwa risasi 36 jijini Dodoma na ‘watu wasiojulikana.’ Jaribio la kudhulumu uhai wa mtu kiasi kile lilifanywa ukiwa CEO JMT. Hakuna jambo lolote la maana umewahi kufuatia tukio hilo.
Tangu 2016 ukiwa CEO JMT uliruhusu uwepo wa kundi la ‘watu wasiojulikana.’ Waliendesha ‘oparesheni’ dhidi ya wakosoaji wa serikali na zaidi. Watu walitekwa, kuuwawa na wengine hawajulikani walipo.
Ukiwa CEO JMT, umeshuhudia uporaji wa fedha za watu waliopewa kesi za uongo kwa jina la ‘plea bargain.’ Ukiwa CEO JMT, juzi mmeunda tume kuchunguza mwenendo wa zoezi la plea baragain. Unawezaje kuwa na ufanisi?
Waendesha Mashitaka wakiwa na lundo la fedha za ‘plea bargain.’
Ripoti za CAG kila mwaka zinaonesha ubadhilifu wa fedha za umma uliokithiri. Hakuna jambo lolote la maana umewahi kulifanya juu ya ripoti hizo. Hata maazimio ya Bunge kufuatia Ripoti za CAG haufuatilii utekelezaji wake. Haujawahi kujisikia vibaya kufuatia uzembe katika usimamizi unaopelekea wizi unaoandikwa na CAG kila mwaka tangu uwe CEO JMT. Ujasiri wa kipekee sana!
Ukiwa CEO JMT na mshirika wa CCM, kati ya 2016/20, ulishiriki jitihada zote za kuua demokrasia nchini Tanzania. Leo hatuna Bunge sababu ya ubinafsi wenu. Mahakama hali kadhalika. Utamaduni wa ‘uchawa’ nchini ni matokeo ya hofu zenu. Si jambo unalohofia ama kujutIa. Maana hadi leo mnalea viongozi wanaotishia na kuhujumu uhuru wa fikra nchini. Hii ni mbaya sana.
Matukio ya raia kuuwawa wakiwa chini ya polisi ni mengi. Mauaji yanatekelezwa na Polisi. Ukiwa CEO JMT, haujawahi kuitisha uchunguzi wowote huru dhidi ya matukio haya, wala kuchukua hatua — hata za kisiasa.
Mwaka 2018 ukiwa CEO JMT, ulishuhudia polisi wakimuua mwanafunzi Akwilina Aqwilini kwa kumpiga risasi. Mliwashitaki ila baaadaye mkawafutia kesi. Hii ndiyo heshima mliyomchagulia Aqwilina. Hakustahili zaidi?
MKIRU na zaidi na matishio ya ugaidi yamedhulumu uhai wa watu wengi sana. Hakuna taarifa yoyote rasmi ya serikali ambayo wewe ni CEO wake kuhusu oparesheni ya MKIRU, idadi ya watu waliopoteza maisha na mwito wa usalama zaidi. Watu waliofunguliwa kesi za ugaidi kufuatia matukio haya wengi hawajashitakiwa. Wako mahabusu miaka sasa. Azory Gwanda aliuwawa katika muktadha huo pia. Tumejifunza nini. Ufanisi wenu kama Serikali ni upi?
Ukiwa CEO JMT, watumishi wa umma wamefukuzwa kwa uhakiki wa vyeti. Hivi karibuni mmeahidi kuwalipa fidia. Nani alisikiliza hizi kesi, kuna uhalifu, na kwanini fidia? Hamjawahi kuwa na umakini hata kidogo.
Ukiwa CEO JMT, watumishi wa umma wamedhulumiwa stahiki zao kwa miaka sita na zaidi, wakiwemo wastaafu. Hivi, Mheshimiwa, wewe umewahi kuishi bila mshahara ama marupurupu kwa angalau siku moja?
Mwaka 2019/20 Ukiwa CEO JMT, mlifuta haki ya Wananchi na AZAKI kufungua mashauri katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, hata bila aibu kwamba Mahakama hii muhimu ipo nchini, Arusha. Uamuzi huu umelisaidia nini taifa?
Ukiwa CEO JMT, umeshiriki kupuuza utekelezaji wa hukumu za Mahakama za Kimataifa, ikiwemo ya Afrika na ya Afrika Mashariki ambazo Tanzania ni mshirika. Mmeiweka nchi yetu sawa na mataifa yasiyojua wajibu wao kimataifa.
Mheshimiwa Waziri Mkuu,
Kwakuwa orodha ni ndefu, ninaomba nikuulize tena, Mheshimiwa, unajisikiaje na unawezaje kuwa kiongozi wa Serikali iliyofeli, japo kwa haya machache?
Ninajua sina umri wa kukushauri ujiuzulu. Lakini nafurahi kukumbusha tulikotoka!
Tumefika rasmi Gereza la Segerea.
Tarehe kama ya leo mwaka juzi, mie na mshirika wangu Theodory Faustine Giyani tulifika rasmi gereza la Segerea. Haikuwa mapema kujua tuko jela sababu ya matukio tangulizi.
Kimsingi, matukio tangulizi yaliogofya zaidi — Mungu alitusaidia. Tulitekwa tukawekwa kusikojulikana kwa siku nne. Bahati nzuri tukajikuta Mahakama ya Mkoa wa Dar Es Salaam, Kisutu.
Ikiwa tukiihesabu kama bahati kufikishwa Kortini ambako ni salama kiasi, siku kama hii kuelekea sikukuu, wakati mshirika wangu Theo akinihoji kinachoendelea na matokeo yake, akili yangu iliwaza dhamana.
Kwamba, tupate dhamana tuepuke kwenda kula sikukuu jela. Kumbe nilikuwa sijui chochote. Labda, mioyoni mwao walisema: “tulia tukuoneshe hujui chochote.”
Sikufahamu kama tungeona sikukuu mbili za mwisho wa mwaka tukiwa jela.
Hata tulipoteuliwa rasmi kuwa wahalifu, tukapewa mashitaka yasiyo na dhamana, sikuwaza kama tungekaa mwaka na zaidi gerezani.
Lakini, licha ya yote, mioyo yetu imejawa na shukrani sana. Leo tukitazama nyuma tunamuona Mungu na watu wake. Watu wema. 🙏🏽
Jambo linalonikwaza sana ni kuona bado kuna watu wanatendewa kama sisi — hata baada ya mabadiliko ya utawala.
Hata hivyo, nina uhakika, “when the center can no longer hold,” aliwahi sema mwanaisimu mmoja, “things fall apart.”
Happy holidays comrades and friends. John 14:14🙏🏽
Ofisi ya Taifa ya Mashitaka inashutumiwa kutumia makosa yasiyo na dhamana kuwashughulikia watu wasio na hatia. “Mtafutie kosa lisilo na dhamana akapumzike jela,” kama nilivyodokeza katika barua yangu kwa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ni tabia iliyopo. Makosa yasiyo na dhamana ni silaha ya wenye mamlaka inayotumika isivyofaa dhidi ya raia wasio na hatia. Ndivyo ilivyotokea kwa Joel Malugu na wenzake (4).
Joel Malugu na wenzake (4) wako gerezani Segerea tangu Oktoba 2018. Wanatuhumiwa kuhujumu uchumi, shauri namba 83/2018, Mahakama ya Mkoa wa DSM, Kisutu. Kosa la kwanza; kuongoza genge la uhalifu na kufanya biashara ya meno 19 ya tembo yenye thamani ya Tsh. 332,850,000/- bila kibali. Kosa la pili; kukutwa na nyara za serikali — meno 19 ya tembo, bila kibali mnamo tarehe 15/10/2018, Pwani na DSM.
Baada ya kukaa miaka miwili gerezani wakingoja kukidhi dhamana, kwa kugundua wanaelekea kufanikiwa kutoka gerezani, Serikali iliongeza kosa la tatu: utakatishaji fedha. Kwamba walijipatia Tsh. 332,850,000/- wakifahamu fedha hizo ni zao la kosa tangulizi (predicate offence) la biashara ya, na kukutwa na, meno ya tembo.
Joel na wenzake walirudi gerezani wakiwa wanyonge sana. Jitihada za kutafuta dhamana sasa zisingewezekana kufuatia nyongeza ya kosa lisilo na dhamana. “Badala ya kukamilisha upelelezi tusikilize kesi, wanatengeneza kosa jipya, tunyimwe dhamana, na hatuna hela za kubargain,” alisema mmoja wao! Tulishiriki huzuni yao.
Kosa liliongezwaje? M/Mungu huwanyima maarifa wenye hila ili ajitwalie utukufu!
Maombi namba 197/2020 yaliwasilishwa Mahakama Kuu, DSM, kupinga kuongezwa kosa la tatu la utakatishaji fedha. Changamoto ya CORONA iliwalazimu kungoja muda mrefu bila kikao — kwakuwa mahakama mtandao ina maruweruwe mengi. Disemba 23, 2020, Mhe Jaji Mgonya aliamuru wafanye mawasilisho kwa njia ya maandishi.
Katika maombi yao, Joel na wenzake walikuwa na hoja (madai) tatu:
Mosi, kwamba Mahakama Kuu iangalie uhalali wa maamuzi ya Mahakama ya Mkoa wa DSM, Kisutu, kuhusu mwenendo wa kesi hiyo.
Pili, kwamba kosa la tatu, utakatishaji fedha, limeongezwa katika hati ya mashitaka isivyo haki ikiwa watuhumiwa wamekaa jela miaka miwili, na baada ya kuona dhamana inaelekea kufunguliwa. Kwamba, walitakatishaje fedha baada ya kukaa mahabusu miaka miwili?
Tatu, kwamba walitakatishaje fedha kwa kukutwa na nyara za serikali ambazo hazijauzwa, kusafirishwa au vinginevyo ili wapate fedha?
Ilikuwa ni madai ya Joel na wenzake kwamba, Jamhuri haikupendezwa kuona wakielekea kupewa dhamana kwakuwa makosa yao ya awali yalikuwa yanadhaminika.
Mahakama iliombwa kubatilisha kosa la tatu katika hati ya mashitaka: utakatishaji fedha.
Kwa upande wake, Jamhuri ilidai maombi hayo hayawezi kusababisha kosa kubatilishwa, kosa limeongezwa baada ya uchunguzi, na kwamba ni kawaida. Waliomba maombi yatupiliwe mbali.
Baada ya kusikiliza pande zote, Mahakama ilijitwalia nafasi yake kutoa uamuzi wa shauri hilo — 04/05/2021.
Mhe Jaji Mgonya ilianza kwa kuonesha kutoridhishwa na namna ambavyo Serikali haikujibu hoja za wapeleka maombi. Serikali ilitegemewa ieleze sababu za kuongeza kosa la utakatishaji fedha miaka miwili baadaye. Haikufanya hivyo.
Katika kufikia uamuzi wake, Mhe Jaji Mgonya alirejea tafsiri ya utakatishaji fedha kama ilivyo katika vifungu (3 na 12) vya Sheria ya Kuzuia Utakatishaji Fedha, sura ya 423/2019.
Mahakama iliichambua hati ya mashitaka katika mizania ifuatayo:
Kwamba, wapeleka maombi (watuhumiwa), walishitakiwa awali kwa makosa mawili mwaka 2018. Kosa la pili, kukutwa na nyara za serikali, walilitenda mnamo Oktoba 15, 2018. Kosa jipya la (tatu) utakatishaji fedha, walilitenda kati ya October 1–15, 2018.
Kutokana na tafsiri ya kisheria ya kosa la utakatishaji fedha, Mahakama ilijiuliza:
Mosi, “kama washitakiwa wanatuhumiwa kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali, ambazo bado hazijauzwa au kusafirishwa, wamepataje mazao ya uhalifu — uuzaji wa nyara za serikali, wakati nyara bado hazijauzwa? Hizo ni nyara ambazo, kimsingi, zitatumika kama ushahidi kuthibitisha shitaka la pili,” alisema Mhe Jaji Mgonya katika uamuzi wake.
Pia, kwamba, “ukitazama hati ya mashitaka, inaonekana watuhumiwa walitenda kosa la utakatishaji fedha kabla ya kukutwa na nyara za serikali. Kama hivyo ndivyo, ni katika mazingira yapi washitakiwa walifanya kosa la utakatishaji fedha wakati tayari wako rumande? Kwa kukutwa na nyara za serikali ambazo hazijauzwa, walinufaikaje na mazao ya uhalifu?”
Pili, kama waliuza nyara za serikali, kungekuwa na uthibibitisho wa mazao ya uhalifu — na labda utakatishaji fedha, tangu awali kesi ilipopelekwa mahakamani. Lakini, hata kama wangekutwa na mazao ya uhalifu — fedha, bado isingetosha kutengeneza kosa la utakatishaji fedha kwakuwa, kitafsiri, fedha zinatakatishwa kutoka katika biashara haramu kwenda katika biashara halali.
Mahakama iliamua kuwa kosa jipya la utakatishaji fedha halina mashiko, ni batili na haliwezi kuongezwa katika muktadha huo. Pia, ili viashiria vya kosa la utakatishaji fedha vitimie, maswali matatu: nani, lini, wapi, na nini, yanapaswa kujibiwa.
Kutokana na maelezo ya kosa la tatu, nani ni washitakiwa wote, lini ni Oktoba 1–15 2018, wapi ni Pwani na DSM. Swali la nne, nini kilifanyika ili Mahakama ijiridhishe namna Jamhuri ilivyopata kosa la utakatishaji fedha, inakutana na maelezo (ya kosa) kwamba: “Wote kwa pamoja walijipatia fedha 332,850,000 wakati wakijua ama kutakiwa kujua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi: kukutwa na nyara za serikali.”
Mhe Jaji Mgonya aliamua kwamba “maelezo ya kosa la utakatishaji fedha katika hati ya mashitaka hayatoshi kutengeneza kosa hilo, hayaoani na tafsiri ya kosa hilo chini ya kifungu cha 3 na 12 cha Sheria ya Kuzuia Utakatishaji Fedha, sura ya 423, 2019.”
Mahakama ilibatilisha kosa la utakatishaji fedha, jambo ambalo limefanya hati hiyo kuwa batili.
Pia, Mahakama ilikubaliana na wapeleka maombi — watuhumiwa, kwamba kosa la utakatishaji fedha liliongezwa kwa nia ya kuwanyima dhamana! Aidha, Mahakama haikuona uhalisia wa kosa hilo kwakuwa maelezo yake hayajitoshelezi, hata tarehe hazioani.
“Ninashangaa kuona siku hizi suala la dhamana katika kesi kama hii limekuwa gumu. Nimeona jitihada kubwa za kuweka ugumu wa kupata dhamana katika makosa ya aina hii, na ndio maana leo hapa mahakamani tuna maombi ya aina hii,” alisema Mhe Jaji Mgonya katika uamuzi wake.
“Wakati mwingine najaribu kuelewa nia ya Jamhuri kwamba pengine watuhumiwa wanaweza kuruka dhamana. Hata hivyo, nakumbuka kuwa dhamana ni haki ya msingi ya kila binadamu, wakiwemo raia wote wa JMT. Dhamana sio upendeleo, bali ni haki kwa mtuhumiwa. Kanuni hii inatambuliwa na Katiba ya JMT, Ibara ya 13(6)(b), inayohusu dhana ya kutokuwa na hatia. Tunapaswa kuifuata.” alisema Mhe Jaji Mgonya.
Ikirejea maneno ya Mhe. Jaji Mweisumo katika kesi ya Tito Douglas Lyimo v Jamhuri, 1979, Mahakama ilisema: “dhamana ni haki ya mtuhumiwa, si upendeleo, labda kama Mahakama itajiridhisha kwamba kwa hoja thabiti za Jamhuri, dhamana itazuia upatikanaji wa haki.”
Mhe Jaji Mgonya alihimiza watuhumiwa wapewe dhamana kwa masharti nafuu badala ya kutafuta sababu za kuwashughulikia, pia, kuzingatia nia ya kutenda haki, kuzuia matumizi mabaya ya taratibu za kisheria, na kuzingatia maslahi ya umma.
Mkasa wa Joel na wenzake, pengine haujaisha! Je, Serikali itakata rufaa? Je, watapata dhamana kwa masharti nafuu? Kuhusu upelelezi, bado ni danadana!
Licha ya Joel na wenzake, wapo mahabusu wengine wengi waliokutana na sarakasi za kuongezewa kosa lisilo na dhamana ili wakae gerezani. Na upelelezi haukamiliki. Hawa ni baadhi:
· Wafanyabiashara wenye tuhuma za kodi, licha ya kunyimwa fursa ya kuona tathmini ya kodi ilivyofanywa, waliongezewa mashitaka ya utakatishaji fedha.
· Wakili Majaliwa Majaliwa na wenzake wakiwa katika harakati za kuomba dhamana, waliongezewa kosa la utakatishaji fedha, wako gerezani Segerea.
· Kuna kijana mdogo alishitakiwa kwa mauaji kwa madai ya kukutwa na sehemu za siri za fisi, kosa limebadilishwa kuwa kukutwa na nyara za serikali na utakatishaji fedha. Segerea tangu 2017. Upelelezi bado!
· Daktari wa binadamu iliyedaiwa kasaidia kutoa ujauzito alipewa kosa la utakatishaji fedha. Miezi nane baadaye, ikiwa upelelezi haujakamilika, alilazimika kununua uhuru (bargain).
· Watumishi wa Umma, Mwita Mataro, Kavishe, Mollel na Haidary, ambao aliyekuwa Waziri wa Maliasili ndugu Kigwangala alitamani kuwaua ati wameua twiga, kwa maelekezo yake walipewa kesi ya utakatishaji fedha. Ripoti ya uchunguzi inaonesha twiga alikufa sababu ya umri, wanaoshitakiwa hawahusiki, hawakuwa zamu!
· Dreva teksi, Mousa Twaleeb, aliyedaiwa kumteka tajiri MO Dewj alipewa kesi ya utakatishaji fedha. Alikaa polisi zaidi ya mwezi, Segerea mwaka wa tatu! Upelelezi bado.
Picha kubwa ni kwamba kosa la utakatishaji fedha linatumika vibaya kwa nia ya kuadhibu watu(humiwa). Hivi karibuni uelekeo ulikuwa kutengeneza mapato kupitia “plea bargain.”
Ninamshauri DPP arejee mafaili yote yenye malalamiko. Watuhumiwa wameandika sana barua. Hawajibiwi. Na kama wakijibiwa, wanakutana na “standard replies,” kwamba: “tumepokea barua tunafanyia kazi,” na blah blah nyingine kama hizo wakati wakiendelea kusota gerezani bila hatia. Malalamiko ya namna hii yanatia doa utendaji, yanaondoa imani ya umma katika mifumo rasmi, yanakaribisha rushwa na kuziba milango ya haki.
Nitakukumbuka daima, kaka Magesa!
Magesa wasu! Emmanuel Magesa Gamba!
“Tito, listen. Tell your guy, if he’s got lifetime projects, he should accomplish within six-month.” Hayo ni maneno ya Daktari mwezi Machi 2019 — kwamba hautaishi zaidi ya miezi sita. Sijui ilikuwaje na nilipokeaje. Lakini, nililia sana. Sikuwa na msaada wowote. Niliwapa taarifa mabroo na rafiki zetu wawili. Tulihangaika kuhimili zile taarifa.
Wakati Daktari anazungumza alinitazama usoni, baadaye akaniambia “nimeuona ujasiri wako.” Hakujua kilichofuata baada ya pale. I had to parade courage ili niwalaghai ndugu waliokuwa wakiningoja nje. Iwapo ningekwama, ingekuwa shida nyingine. Wewe pia ungefahamu kuna shida kubwa kiasi kile, na kwamba hauna miezi sita duniani. Ingekuathiri zaidi. Kaka, ile taarifa ilikuwa ngumu mno.
Tulipambana ku-cover hali ile. Uliruhusiwa kurudi nyumbani. Nikashauriana na Saada, rafiki yako, abaki nyumbani kukuangalia. Japo kulikuwa na ndugu wengine, Saada alijua ukubwa wa tatizo linalotusibu. Saada alikubali. Miye nikasafiri. Siku narejea, baada ya wiki, nilikuwa na taarifa kuwa usiku wake ulizidiwa ukakimbizwa hospitali. Nilifika hospitali tukabadilishana mawazo. Ulikuwa na utulivu japo ulianza kuhofu. Uli-google kuhusu magonjwa, athari na tiba. Sijui kama ulikuwa na taarifa sahihi. Haukukaa sana, ukaruhusiwa kurudi. Ninamshukuru sana Saada kwa kila kitu. Moyo wa kipekee anao.
Tulikaa angalau wiki. Rafiki zetu walikuja kututia moyo. Asubuhi moja ulizidiwa. Tulifikiri ni kawaida. Tukarudi hospitali. Rafiki zetu walijitokeza kutuunga mkono hospitali. Hata hivyo, ilinishangaza kuona unapelekwa ICU. Tulihamaki. Inakuwaje? Tukawa wapole. Japo kwa shida, ukiwa ICU, kila uliponiona uliongea, ulitabasamu.
“Niitie Mchungaji,” ni maneno yako yaliyoniaminisha kuwa ulikuwa na mwisho mzuri. Baadaye ukawa kimya kaka. Wiki nzima huongei. Rafiki zetu walifurika kukuona hospitali na kupiga simu. Walitamani kukusaidia. Wahitimu wa Mzumbe na GESECO walijichanga kusaidia huduma kwako. Baadaye tukawa hatuoni mwanga tena. Kila siku kuna taarifa mbaya. Hakuna progress. Ilikuwa kazi kuhimili na kudhibiti mihemko. Madaktari walifanya kazi kubwa kutuweka sawa. Lakini they had to say the truth.
“Tito we can confirm that there’s ‘brain death,’” alitueleza Datari kwenye kikao. Nilitoka hapo sina nguvu. Niliona imefikia mwisho. Na madaktari walinifahamisha. Protocol za kitabibu zinaelekeza hivyo. Kila hatua na tukio linahitaji idhini. Wiki nzima ICU. Usiku wa kuamkia 26 April, saa saba, madaktari walithibitisha kifo chako. Tulienda hospitali usiku huohuo. Tulishuhudia ukitolewa ICU kupelekwa mortuary. Thought I was dreaming kuona kinachotokea. Kuna rafiki zangu walinifuata hospitali usiku huo. Wengine hatukuonana. Lakini they demonstrated solidarity.
Siku zako za mwisho duniani zilikuwa chungu kwako na kwetu. Tulitangaza msiba usiku huohuo. Ndugu na rafiki walifurika nyumbani. Kwa uchungu sana tulikuaga Dar. Tukasafiri kwenda nyumbani Bunda kukuhifadhi. Nilishiriki misiba mingi lakini wakati ule nilikuwa na msiba nyumbani kwangu. Hata sasa naandika machozi yananitoka. Sikuwahi kusikia kupungukiwa kama kipindi kile. Haupo na hauwezi kurudi kaka.
Kaka ulinipokea Geita High School. Baadaye nikakupokea Chuo Kikuu Mzumbe. Baadaye tukaondoka nyumbani. Tukatafuta sehemu ya kuishi pamoja. Tuliishi Maisha yetu ya kawaida as graduates wasio na mchongo. Itifaki zetu za maisha zilileta uhai kila siku. Rafiki na kaka yetu Emmanuel Nyanza ni shuhuda. Waliotutembelea nyumbani walishuhudia hili. Hatuna kitu lakini tuna furaha, amani na ushirikiano wa hali ya juu.
Kaka kuna wakati tulitengeneza password ya msaada na dharura. “Faza, naandika nikiwa sina option nyingine, tafadhali fanya maajabu” au “Faza, naandika nikiwa na matarajio makubwa kwako baada ya minazi yote kuteleza,” zilikuwa ni jumbe zetu zinazoashiria kuomba msaada wa ghafla. Kila nilipoona jumbe yenye mrengo huo, au wewe ulipoiona, ulifanya kila uwezalo na majibu yake yalikuwa jumbe nyingine, sio kutoka kwako, bali kwa kampuni hii ama ile ikisomeka “Imethibitishwa.. umepokea…” na zaidi. Kaka, ujamaa huu miye na Imma, na ARAMS, na makomredi wengine katika mnyororo huu, tunauendeleza.
Kaka, umeniachia marafiki. Tunaheshimiana. Tunashirikiana. Umeniachia ujasiri, uthubutu na upendo. Ulikuwa na watu ambao wamekuwa watu wangu pia. Watu wema sana. Rafiki yetu Eliakim aliniliza sana wakati tukihangaika kung’amua kitendawili chako cha ICU — siku chache toka tuambiwe ‘brain death.’ “Tito, the guy is used to you. Elders advise umpungie mkono wa kumuaga. Maana hata wakati hawezi kuongea, kila ukiingia wewe alionesha reactions. Muage before we buy advise of medics,” aliniambia Eliakim katikati ya sintofahamu. Eliakim good guy hadi kesho!
Safarini kuelekea kukuhifadhi nyumbani tuliimba maisha yako. Kaka bado tunakuadhimisha. Mshirika wetu Imma Nyanza aliniambia hivi karibuni: “Tito, you know 2019 was a tough year to me,” alisema Imma, na kuongeza: “I couldn’t figure out a couple of tragic things and events. Magesa succumbed to call of his creator. You were abducted and held behind bars for like almost indefinitely. A hell of tough experience. Couldn’t find a reason why a circle was hunt as such. But I am grateful. God is good.”
Kaka Magesa, wewe, Imma na miye, tumeishi pamoja. Tuna ujamaa uliovuka udugu. Licha ya kupungukiwa, haupo na tungetamani uwepo, Imma na miye tumekubaliana kuona kusudi badala ya tatizo. Kusudi la Mungu. Maisha na kifo chako, kaka Magesa, ni mapenzi ya Mungu. Ulikuwa na ndoto zako. Pia ulipalilia ndoto zetu siku kwa siku. Uliongoza maombi, wewe na Imma mpate kazi rasmi. Hatimaye mkapata. Tulifurahi sana. Tukamshukuru Mungu. Ungekuwa hai, ungekuwa mbali. Mungu ni mwema.
Wewe na Imma ni Waadventista-wa-Sabato. Jumamosi mlikuwa na playlist yenu. Nami vivyohivyo nilikuwa na playlist ya jumapili. Ilikuwa heri wakati wote. Maisha yetu pamoja yalinifunza vitu vingi, ninashukuru daima.
Kaka, tulifahamu ugonjwa wako kwa muda mfupi. Mwanzoni, kama ulcers, lakini baadaye, kwa kuchelewa, tukaambiwa ni homa ya ini. Ilikula ini na hatimaye ubongo.
Leo miaka miwili tangu ututoke. Kaka, mioyo yetu imejawa na shukrani.
SUMMARY: Ni kuhusu vilio vya haki dhidi ya mfumo wa haki jinai nchini.
Mheshimiwa Rais, licha ya uwepo wa misingi ya kitaasisi na kisheria katika uwanda wa haki jinai, bado kuna changamoto zinazotia doa suala la utoaji haki nchini. Barua hii inabainisha masuala machache ambayo kama yakifanyiwa kazi tutapunguza vilio vya haki na kuleta unafuu na ufanisi. Kwa hali ya sasa, kama alivyowahi kusema Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwamba: “hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo,” nami nasema, matatizo yapo kama ambavyo nitafafanua hapa chini. Wito wangu ni kwamba tuyakubali na tujisahihishe.
Mheshimiwa Rais, katika uendeshaji wa mashitaka ya jinai, husuani makosa yasiyo na dhamana, Mahakama haina sauti yoyote zaidi ya kusikiliza upande wa mashitaka (Serikali) wanasema nini. Utamaduni huu umebarikiwa na sheria, husuani Sheria ya Mwenendo wa Mashitaka ya Jinai (CPA). Lakini je, inapaswa kuwa hivi? Kwamba, pasi na mwongozo wa Serikali, Mahakama haiwezi kufanya lolote? Ukifungua kesi kukosoa mwenendo wa shauri lako, kwa mfano; tegemea ugumu katika shauri hilo. Kesi itaondolewa mahakamani, utakamatwa papo hapo na kushitakiwa kwa kesi hiyo hiyo. Kama ulishakaa miaka minne jela, utaanza upya kwa kuwa shauri ni jipya. Hivi ndivyo Mahakama inavyopokwa mamlaka na Serikali ambayo ni upade katika kesi. Kwa ujumla, kuna matumizi mabaya ya kanuni ya nolle prosequi.
Mahabusu mmoja aliyekaa gerezani kwa miaka 10 amekumbana na kadhia hii. Akiwa ameongea na mashahidi 19 wa Jamhuri, tayari kwa utetezi, kesi ikaondolewa mahakamani (nolle prosequi), akakamatwa papo hapo, akashitakiwa upya kwa kosa hilo hilo, Mahakama hiyo hiyo. Hadi sasa bado yupo gerezani akiambiwa upelelezi haujakamilika. Ukijiuliza upelelezi upi tena? Hupati jibu. Lakini hii ndiyo taswira ya jinsi mambo yanavyofanyika katika mnyororo wa haki jinai. Nafasi ya Mahakama? Sio kwa ubaya, ila ni sahihi kusema kwamba Mahakama haina mamlaka. Ni mgogoro wa kisheria? Labda! Lakini endapo Jamhuri ingetekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kusingekuwa na mateso kupitia Mahakama kwa watu wasio na hatia kama inavyofanyika sasa. Na kwa kuwa Mahakama ni chombo cha utoaji haki, inategemewa ifanye zaidi ya hiki kinachofanyika sasa hivi. Mahakama na taratibu za haki jinai zisitumike kama mhuri wa kuhalalisha mateso kwa watu wasio na hatia.
Mheshimiwa Rais, katika makosa yasiyo na dhamana, kazi pekee ya Mahakama ni kujiridhisha kama dhamana imezuiwa, kisha kuahirisha kesi kwa maelekezo ya Jamhuri. Wimbo huu unaweza kuimbwa kwa miaka mingi, kwa kadri Serikali itakavyoona vema. Kama kesi ni ya kubumba au yenye nia ovu, mtuhumiwa atakaa gerezani kwa muda unaowapendeza walioamuru iwe hivyo. Ni ajabu kwamba mateso haya kwa binadamu wenzetu yanahalalishwa na ukimya wa viongozi na wananchi.
Kuna vijana walishitakiwa wakiwa na umri kati ya miaka 12 na 14 (watoto wadogo). Kesi yao ilijaa danadana. Ilianzia Mahakama ya Watoto. Baadaye Mahakama Kuu. Iliondolewa mahakamani wakakamatwa na kushitakiwa upya zaidi ya mara mbili. Baadaye, wakiwa hatua ya kujitetea, Jamhuri ikakatia rufaa uamuzi mdogo wa kupokea nyaraka. Wakakaa mwaka na nusu bila kwenda Mahakamani wakisubiri kikao kusikiliza hiyo rufaa katika Mahakama ya Rufani. Baadaye, wakaletewa wito wa kwenda Mahakama Kuu tena. Kwahiyo, kikao cha Mahakama ya Rufani hakikufanyika. Muda ulipotea bure. Walipoitwa Mahakama Kuu katikati ya mwaka 2020, Serikali ikawasilisha ombi la kuondoa kesi Mahakamani (nolle prosequi) — baada ya miaka kumi ya kukaa gerezani bila hatia. Ikumbukwe kwamba, walishitakiwa wakiwa watoto wadogo. Wametumia utoto wao wote gerezani. Wamekosa huduma stahiki kwa mtoto: elimu na malezi. Wamepoteza malengo na matarajio yao. Wametumikia adhabu bila kutiwa hatiani. Jambo hili ni baya sana. Hakuna aliyenufaika na mateso hayo. Hata polisi na waendesha mashitaka hawanufaiki kwa vyovyote vile. Mfano huu ni mmoja kati ya mingi. Kwanini inashindikana kuchora mstari kati ya wahalifu na wasio na hatia, kila mtu apate stahiki yake?
Mheshimiwa Rais, ukiwauliza watu walioko magerezani leo wachague kati ya kuishi na kufa, kati ya kumi utapata angalau mmoja ambaye yuko tayari kupoteza maisha kwa kuwa haoni maana ya kuwa hai huku akipata mateso. Huu ndio uhalisia. Mateso wanayopitia hayamithiliki. Sababu ya mateso haya iko bayana. Kuna watumishi wa umma hawatimizi wajibu wao na hakuna anayejali, labda wewe utaliona hili. Mimi najiuliza, hivi kweli tuna utawala wa sheria nchini Tanzania? Ukiwa kizuizini ukauona upande wa pili wa sheria, utaona jinsi suala la haki za binadamu linavyopigwa danadana Tanzania. Kuna dhana miongoni mwa watumishi wa umma kwamba wimbo wa haki za binadamu tumeletewa. Hawako tayari kuuimba. Lakini je, ni kweli kwamba hatupaswi kuheshimu utu wa mtu? Unapojenga barabara, usipoitumia wewe, itawafaa hata majirani zako. Tendo lolote jema, kwa vyovyote vile, litamfaa mtu. Mfumo imara wa haki jinai utaleta unafuu na faida kwa taifa letu. Tuchukue hatua. Tutajikwamua kutoka hapa tulipo kwa kuwa na mgawanyo rasmi wa mamlaka. Serikali itimize wajibu wake. Kusiwe na upendeleo na uonevu. Mtu ashitakiwe kwa haki na kwa wakati. Mwenendo wa mashitaka udhibitiwe. Mahakama irejeshe(we) mamlaka yake kama chombo cha utoaji haki. Sheria zote zinazoleta ukakasi katika mnyororo wa haki jinai zifutwe. Hii ni kwa ajili yetu na vizazi vijavyo. Tunaweza kufanya vizuri zaidi ya sasa.
Kuhusu upelelezi usio na kikomo
Mheshimiwa Rais, upelelezi usio na kikomo kwa baadhi ya makosa ya jinai ni kero kubwa sana. Hata katika makosa yenye ukomo wa upelelezi, bado ni changamoto kutekeleza matakwa ya kisheria. Mahakama haifanyi vizuri katika hili. Kuna ukomo ila mtuhumiwa haachiwi kwa kuwa eti atakamatwa hapo hapo na kurudishwa upya mahakamani. Aibu gani hii? Hali ilivyo, ukamilishwaji wa upelelezi katika makosa yasiyodhaminika limeachwa mikononi mwa Serikali. Kwamba, ni hiyari yao kufanya upelelezi kwa muda watakaohitaji. Japo hii ni sawa kama mshukiwa hayuko kizuizini au hajashitakiwa, lakini mtu anaposhitakiwa, akatupwa gerezani kusubiri hatma yake, ukomo na udhibiti wa kimahakama katika upelelezi ulipaswa kuwa lazima. Sheria zetu zimeruhusu watu wachezee maisha ya binadamu wenzao kadri wanavyotaka.
Mheshimiwa Rais, ukiniuliza mimi kama tuna sababu ya kujikosoa kama taifa nitajibu ndio. Kushitaki kabla ya uchunguzi, au kuchelewesha upelelezi, ni jambo lisilokubalika katika jamii ya wastaarabu. Jamii zilizostaraabika huzingatia utu, haki na maslahi ya mtu wakati wa kushughulikia tuhuma dhidi yake. Mashitaka huja baada ya upelelezi. Kama ni uchunguzi, mshukiwa anahakikishiwa haki zote ikiwemo haki ya dhamana. Jambo hili yafaa lijumuishwe kwa vitendo katika mnyororo wa haki jinai nchini.
Mheshimiwa Rais, usikubali kila unachoambiwa, kwamba tunakwenda vizuri. Washukiwa wanakaa vituo vya polisi kwa zaidi ya mwezi mmoja na hili hautalikuta kwenye taarifa za mahabusu wanaolala vituo vya Polisi (occurence book). Wanajua wanavyofanya ili kupoteza kumbukumbu. Wapo watu waliokaa vituo vya polisi zaidi ya mwezi. Baadaye tena wakae gerezani miaka na miaka wakisubiri upelelezi ukamilike. Mtu aliyedaiwa kumteka tajiri Mohamed Dewij, alikaa Kituo cha Polisi zaidi ya mwezi mmoja. Na sasa yuko gerezani zaidi ya miaka miwili na upelelezi wa kesi yake haujakamilika. Ni hatari kuona haya yakifanyika chini ya uangalizi (na ukimya/idhini) wa viongozi wetu.
Mheshimiwa Rais, wapo ambao kesi zao zinasikilizwa. Lakini hawawezi kujihakikishia kupata haki kwa wakati. Mwenendo wa kesi nyingi hauridhishi. Kuna maahirisho yasiyo na msingi japo sheria inakataza. Mashahidi hupelekwa kwa kusuasua. Upande wa pili wa sheria (unaotokana na utashi wa Serikali) ni mchungu sana kuufahamu licha ya kuuishi. Upelelezi bila kikomo wala udhibiti wa mahakama ni hatari kwa mustakabali wa haki zetu. Mfumo wa “peleleza-kamata-shitaki” utasaidia kudhibiti matumizi mabaya ya mamlaka. Mifumo ya haki jinai, kwa sasa, inatumika kurasimisha mateso kwa watu wasio na hatia. Ikiamuriwa ushughulikiwe, ni moja kwa moja, hadi watesi wako watakapoona imetosha. Serikali inafaa ijikosoe, ifanye kwa ajili ya watu. Tubadilishe sheria zibebe dhana ya haki zaidi. Serikali ilenge kutenda haki, haki tu. Vilio vya haki visiposikilizwa ni hatari kwa ustawi wa Taifa. Umoja wa kitaifa ni kitendawili kama baadhi yetu wanafanywa mateka katika ardhi yao.
Kesi za kubumba, mashitaka ya hila
Mheshimiwa Rais, waathirika wa huu uonevu ni wengi zaidi ya wanaosikika. Katika kilichotajwa kuwa vita ya kiuchumi, vita ya madawa ya kulevya, vita dhidi ya wakosoaji wa Serikali ya awamu ya tano na wakati mwingine, chuki za wenye mamlaka dhidi ya watu wenye uhuru wa kiuchumi, wasomi na wenye fikra huru, yote kwa ujumla, yamesababisha lundo la mahabusu wenye kesi za kubumba wasio stahili kuwa gerezani. Wapo walioko uraiani kwa dhamana huku kesi zao zinaendelea.
Sipendi kumnyooshea mtu kidole. Lakini kwa nafasi yako una uwezo wa kutambua nani aliasisi na anaendeleza tabia hii chafu. Ofisi ya Mashitaka ya Taifa (NPS) na Jeshi la Polisi na idara nyingine ni washirika katika hili. Kuna task force ambazo zimeshamiri sana. Kukosekana kwa mgawanyo sahihi wa mamlaka na uendeshwaji wa ofisi hizi muhimu bila kujali taaluma, utu wala hofu kwa Mwenyezi Mungu kumechangia ongezeko la kesi za namna hii kwa miaka mitano iliyopita.
Mheshimiwa Rais, watu wa kada zote ikiwemo watumishi wa umma, wafanyabiashara, wasomi, wanaharakati na wanasiasa, wamekuwa waathirika wa mchezo huu mchafu dhidi ya ubinadamu na utu. Ninadhani kwamba kuna haja ya kurejea malalamiko lukuki yaliyowasilishwa na hawa watu — wao binafsi ama kupitia kwa Mawakili wao — katika ofisi mbalimbali ili kupata mwafaka. Ninashauri wapewe kipaumbele watu walioko magerezani na vizuizini kwa kuwa kukosa uhuru hata kwa dakika moja, ukijua huna hatia, ni mateso makubwa sana. Pia, kesi zote za kubumba na rekodi za jinai zenye mrengo huu zifutwe. Nafuu itolewe kwa wote walioporwa mali zao.
Mateso katika vituo vya polisi
Mheshimiwa Rais, watu wa Mungu wameteswa sana. Mateso yasiyomithilika. Sio lazima ikutokee ndio ukubaliane na mimi kwamba watu wanateswa. Mshirika wangu Mdude Nyagali, ambaye sasa analipa gharama ya kuikosoa Serikali yake, aliwahi kutoa ushuhuda wa mateso aliyopata akiwa mateka kizuizini mikononi mwa dola la awamu ya tano. Licha ya kwamba Mdude awalitaja watu na taasisi zilizoshiriki kumtesa, hakuna aliyechukuliwa hatua hadi sasa. Mateso yapo ni wakati mwafaka wa kujisahihisha.
Wapo watu wana ulemavu wa kudumu kutokana na vipigo wakiwa chini ya polisi. Idadi kubwa ya mahabusu walioko magerezani walikiri makosa yao wakiwa vituo vya polisi. Ilikuwaje? Walishughulikiwa. Polisi huwa wanahitaji uwape ushirikiano ambao kwao ni kusema kile wanachotaka kusikia, sio kile unachotakiwa kusema. Kazi ya uchunguzi haifanyiki kisayansi wala kitaalamu. Inafanyika kwa nyenzo za mateso. Unamminya mtu makende ili akiri kosa, halafu iweje? Wapo waliolazimika kukatwa uume kwa kuwa wakati wa mateso waliingiziwa “spoku” kwenye mrija wa mkojo katika uume, ikasababisha kansa ambayo hutegemei itibiwe kizuizini au gerezani.
Mheshimiwa Rais, zipo task force. Zimeundwaje, na kwa nini zinafanya majukumu ya kipolisi? Kwa wanaofahamu, maana ya task force ni mateso, mateso, mateso. Watu wameteswa sana na hivi vikundi. Hakuna sababu ya kuukimbia ukweli. Mjadala kuhusu task force upo tangu enzi wa Bunge la vyama vingi — Mhe. Godbless Lema, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (CDM), aliwahi kuligusia na hivi karibuni katika Bunge la chama kimoja, Mhe. Nape Nnauye, mbunge wa Mtama (CCM), amerudia suala hili. Ni mabavu, mabavu, mabavu. Usiingie kwenye 18 zao.
Mheshimiwa Rais, ili kuona ukubwa wa tatizo, na kwa minajili ya kujali, ni vema kuangalia upya suala la haki za mshukiwa chini ya polisi au mamlaka flani. Maandishi katika sheria zetu kuhusu taratibu za haki jinai kwa sasa ni sawa na gheresha tu. Kwamba na sisi tuna sheria. Ila utekelezaji wake, japo zote sio sheria nzuri, unategemeana na utashi. Kuna wakati Tanzania iliongozwa kwa kadri kiongozi anavyoamka. Haya mambo yalishuka hadi kwa watendaji wa chini. Ukiwa chini ya polisi au task force wenye nia ovu utaona kuwa uko mbali sana na sheria, mbali na dunia wanakoishi binadamu. Tujikosoe!
Makubaliano ya kukiri kosa, au plea bargain
Mheshimiwa Rais, kabla ya kutungwa kanuni za utekelezaji wa sheria ya “makubaliano ya kukiri kosa,” ilikuwa vigumu sana kuona utekelezaji wa sheria hiyo katika jicho la haki. Licha ya shabaha nzuri ya sheria hii, utekelezaji wake unaleta walakini. Sheria hii imekuwa mbadala wa upelelezi katika makosa ya uhujumu uchumi. Kwamba, ili umalize kesi, lipa fedha ondoka ukaendelee na shughuli nyingine. Wangapi wanamudu nafuu hii ya kinyonyaji?
Mheshimiwa Rais, pamoja na mambo mengine, ni muhimu kubainisha kwamba makubaliano hayafanyiki kwa hiari ya pande zote, hususani upande wa mshitakiwa ambaye anakuwa na njia moja tu ya kumaliza kesi yake — yaani kukiri kosa. Wakati mwingine, hakuna majadiliano na kama yatafanyika, basi ni geresha kwa kuwa mshitakiwa hupewa chaguo moja ambalo, hata hivyo, ataliafiki kutokana na mazingira aliyopo. Mawasiliano yanafanyika gizani. Hakuna vikao (rasmi) wala kumbukumbu za majadiliano kwa ajili ya rejea. Nafuu hii inategemea utashi wa waendesha mashitaka. Utatembea umbali mrefu kuipata. Rushwa katika zoezi hili haitajwi hadharani kwakuwa haupo ushahidi wa moja kwa moja, lakini je, hatuna sababu ya kuchunguza?
Mheshimiwa Rais, tunaweza kuboresha; zoezi lifanyike kwa uwazi na bila shuruti — angalau chini ya usimamizi wa taasisi huru kama Mahakama. Makubaliano yanayofanyika nje ya Mahakama na kusajiliwa Mahakamani upo uwezekano kuwa hayamaanishi kauli moja! Tujikosoe!
Makosa yote yawe na dhamana
Mheshimiwa Rais, ninaheshimu maamuzi ya Mahakama ya Rufani ya hivi karibuni kuhusu suala la dhamana, kwamba zuio la dhamana liendelee kuwepo kwa baadhi ya makosa. Lakini ni maoni yangu kwamba bado tunahitaji mjadala na mwafaka juu ya suala hili. Kuna haja ya kuwekeza jitihada kung’amua namna ya kudhibiti utolewaji dhamana kuliko kujielekeza kuzuia dhamana. Mahabusu ni wengi magerezani kuliko wafungwa. Kwa nini? Wamenyimwa dhamana, upelelezi na uendeshaji wa kesi unachukua muda mrefu, miaka hadi miaka. Ninapendekeza kwamba uamuzi wa kuruhusu ama kuzuia dhamana uwe wa Mahakama kuingana na mazingira ya kesi husika. Tuondokane na sheria inayozuia dhamana na kuondoa nafasi ya Mahakama. Kuamua haki, wajibu na maslahi ya mtu iwe kazi ya Mahakama sawa na Ibara ya 13(3) na 107 A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ukuu wa Katiba unabakia kwenye maandishi kama kuna sheria zinazokinzana na Katiba — kama hii ya kuzuia dhamana kwa nasibu bila utaratibu na bado zinatumika. Majirani zetu Zanzibar, Kenya, Uganda wameondokana na utaratibu huu usiofaa.
Mheshimiwa Rais, kwa upande mwingine, ruksa ya dhamana kwa watuhumiwa itaondoa mashitaka ya hila, kama yale ya “mchagulieni kosa lisilo na dhamana akakae jela.” Itadhibiti rushwa na urasimu, itapunguza msongamano magerezani, itatilia mkazo dhana ya ukuu wa Katiba na Kanuni zake, mathalani: “mtuhumiwa kutokuwa na hatia hadi ithibitishwe, mgawanyo wa mamlaka na uhuru wa mahakama,” na kudhibiti upelelezi.
Mheshimiwa Rais, kwa sasa, idadi ya mahabusu inatumika kama kiashiria kuonesha utendaji kazi wa watu flani. Lakini je, idadi ya mahabusu inaendana na idadi ya kesi zinazokamilika kwa mwaka? Wangapi wanakutwa na hatia? Wangapi wanaachiwa? Majibu ya maswali haya yanachukiza! Kiwango cha watu wanaoteswa bila hatia kiko juu sana. Watu waliokaa mwaka na zaidi gerezani ni wengi kuliko wenye siku moja hadi miezi sita. Hii sio sawa.
Mheshimiwa Rais, kauli za hivi karibuni za Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma na wadau wa haki jinai kuhusu dhamana zinaashiria hitaji la mwafaka mpya. Kwa kuwa, kwa sababu zinazotabirika, imeshindikana kutengua sheria kandamizi inayozuia dhamana kupitia Mahakama, ninaishauri Serikali kuiangalia upya kwa manufaa yetu sote. Ninaamini kwamba inawezekana watuhumiwa kupewa dhamana kwa udhibiti na uangalizi wa mahakama — kama inavyofanyika Zanzibar, Kenya na Uganda. Tubadili sheria hii.
Mahakama mtandao
Mheshimiwa Rais, Mahakama ya Tanzania imeanza kutoa huduma kwa kutumia mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Mfumo huu uliokuwa katika majaribio, umetumika zaidi wakati wa janga la COVID-19, tangu Machi, 2020. Shabaha ni kurahisisha ufikiwaji wa huduma za kimahakama. Mahakama, kwa bahati mbaya, imerasimisha matumizi ya TEHAMA bila maandalizi stahiki. Mahakama (na Wizara ya Sheria), kwa ujivuni, imetaja mfumo huu kama sehemu ya mafanikio yake.
Wakati Mahakama ikijipongeza kuendesha mashauri kupitia mtandao, wapo wanaoihesabu hatua hiyo kuwa ni uongo, dharau na kutokuheshimiana. Uongo kwa umma, dharau na kukosewa heshima kwa mahabusu. Kwa nini? Kwa sababu Mahakama Mtandao inafanya kazi ya kuahirisha kesi — mara nyingine kwa Hakimu mmoja au karani, ajabu! Hakuna uhakika wa kuonana na hakimu au mwendesha mashitaka wako. Umeme au mtandao vikifeli, siku imeisha, rudi baada ya siku 14. Siku 14 baadaye, una uhakika wa kukutana na hali ileile uliyoiacha.
Mheshimiwa Rais, maboresho — utayari, fedha na maarifa — yanahitajika ili mfumo huu ulete nafuu na ufanisi uliokusudiwa. Miundombinu (majengo na vifaa) ya Mahakama na Magereza iboreshwa kukidhi mahitaji ya teknolojia. Magereza wana unafuu hawapeleki mahabusu mahakamani hususan Mahakama ya Mkoa wa Dar, Kisutu. Lakini athari za mfumo huu kwa mahabusu ni kubwa. Wanakaa gerezani bila mawasiliano na Mahakama kwa muda mrefu. Ikitokea mahabusu akateswa, hana mahali pa kukimbilia. Ufuatiliaji wa kesi pia unakuwa mgumu. Kurasimisha mfumo sio jambo baya. Lakini urasimishaji uendane na mahitaji ya walaji.
Watoto, watu wenye ulemavu na wageni
Mheshimiwa Rais, licha ya uwepo wa mahabusu na mahakama za watoto, si ajabu kukuta watoto wadogo katika magereza ya watu wazima. Tabia wanazojifunza haziwasaidii. Wanakosa elimu, malezi na hifadhi ya jamii. Chakula na matibabu duni ni hatari kwao. Watoto ni waathirika wa ulawiti magerezani — japo haitatokea upewe taarifa rasmi. Ninakusihi, mulika eneo hili, tujali watoto wetu.
Mheshimiwa Rais, mahabusu wenye matatizo ya afya ya akili wapo wengi magerezani japo wanapaswa kuwa hospitali. Mtu anayekula magazeti, au kinyesi, au kula jalalani, anakaa gerezani ili iweje, kwa faida ya nani? Wanateseka na kuathirika zaidi. Wanafungiwa vyumba vya peke yao bila uangalizi makhsusi. Wanalazimika kusubiri upelelezi ukamilike mwaka hadi mwaka. Uelewa wa kawaida ni kwamba wanahitaji huduma kabla ya kushitakiwa. Polisi na Ofisi ya Mashitaka warejee mashauri ya watu hawa, hatua stahiki zichukuliwe. Heshima na utu wao ni vema vikalindwa.
Wageni, tabaka la wakimbizi na watafuta hifadhi, japo miongoni mwao kuna wenye sifa za kutamkwa kuwa wahalifu, wapo pia wasio na hatia. watu hawa, kwa ujumla, wanapokamatwa hutupwa vituo vya polisi (mbele ya kamera) na kuitwa wahamiaji haramu, kisha katika mazingira ya hofu na ugeni, wasiweze kujitetea, hutupwa gerezani. Ni vema kuchunguza kesi za namna hii ili watafuta hifadhi, wasiostahili mateso na adhabu, wabainike na wapewe nafuu wanayostahili.
Mheshimiwa Rais, wanawake magerezani wana mahitaji makhsusi ambayo hawaruhusiwi kuyapata. Marufuku ya taulo za kike, kwa mfano, ni kitendo cha kikoloni na kikatili sana dhidi ya utu wa mwanamke. Wenye ulemavu, watoto au ujauzito, wako hatarini kwa kuwa, kwa vyovyote vile, mazingira ya gerezani hayawezi kumfaa mtu wa hali hiyo. Miundombinu na huduma za jamii ziboreshwe kukidhi mahitaji makhsusi ya wanawake.
Hali ya magereza yetu
Mheshimiwa Rais, zipo sheria za kikoloni zinazoninyima haki ya kukuambia yafuatayo. Lakini nalazimika kukusimulia, na moja ya ombi langu ni kufutwa sheria hizo. Ni imani yangu kwamba mazungumzo haya hayatahesabika kama uchochezi kwakuwa sina nia ovu. Mahabusu magerezani kwa sehemu kubwa hawaishi kwa kufuata sheria bali amri na maelekezo ya siku kwa siku ya askari magereza — hata kama hayatokani na sheria, na si ya haki. Ukipata nafasi ya kuwasikiliza mahabusu ambao sasa ni zaidi ya elfu kumi magerezani, utasikia mengi. Ukaguzi magerezani ni zoezi linaoacha maumivu makubwa kwa mahabusu. Licha ya shabaha njema, kubaini vitu visivyohitajika, askari magereza hugeuza zoezi hili kama nyenzo ya mateso kwa watu wasio na silaha, na hawawezi kupambana. Ukaguzi upo wa aina mbili. Mosi, mahabusu wanaporudi kutoka mahakamani ama kushukiwa kuwa na kitu visivyohitajika — kilevi, fedha au silaha — hukaguliwa. Pili, kaguzi maalum chini ya askari magereza (wa kikosi maalum).
Mheshimiwa Rais, upekuzi si hoja lakini utekelezaji wake ndio tatizo. Ni ukoloni, ukatili, na tishio dhidi ya utu wa mtu. Mahabusu, bila kujali umri, wanavuliwa nguo ili wapekuliwe. “Vua nguo, ruka kichura, kohoa, chuchumaa, simama juu.. chini,” ni maelekezo yanayozingatiwa katika upekuzi. Ukisikia “niletee kinyesi chako,” utatakiwa ukajisaide kwenye ndoo ulete ushahidi kuonesha hujabeba kitu tumboni. Ndoo moja inatumiwa na mahabusu wangapi? Ni aibu! Udhalilishaji katika zoezi hili haumithiliki. Hakuna faragha. Ni wapi, duniani, penye wastaarabu, ambapo huu mfumo wa kifedhuli bado unatumika? Heshima kwa utu wa mtu imekuwa hiyari badala ya sheria.
Mheshimiwa Rais, askari magereza wa kikosi maalum, hawa usiombe wafanye ukaguzi. Ni kama nyuki wamekuvaa. Ukisikia filimbi, lala chini subiri kuvua nguo, kipigo, matusi na kila aina ya mateso watakayokuchagulia, kwa nyenzo wanazotaka. Hufuatiwa na uharibifu wa vyakula, nyaraka na mali za mahabusu. Wasipokunywa, basi kwa nadra sana watamwaga soda, maji, au maziwa — mali za mahabusu, bila sababu. CCTV camera za magerezani zina kumbukumbu ya matukio haya ya kinyama.
Lakini je, upekuzi huu ni sahihi? Tumepita hapa au pale penye ukaguzi wa hali ya juu. Lakini sikumbuki ulazima wa kuvua nguo, kupigwa, kuteswa na kuharibiwa mali katika upekuzi. Wanachofanya askari kwa mahabusu ni ukatili na jinai. Kero hii itatuliwe haraka. Askari magereza wakumbushwe kwamba mahabusu sio wahalifu na kwamba hata wahalifu wanatekeleza adhabu kwa mujibu wa sheria. Kiwango cha uvunjifu wa sheria magerezani kiko juu sana.
Mheshimiwa Rais, huduma duni za afya ni tatizo sugu. Ninakushauri uweke kipaumbele cha huduma za afya kwa mahabusu. Ni binadamu wenzetu ambao hawajatamkwa kuwa wahalifu. Na hata kama wangekuwa wafungwa, bado wana stahiki zao kama binadamu. Huduma duni na mazingira yasiyoakisi afya ni hatari kwa maisha ya binadamu. Dawa na vipimo ni lazima viwepo wakati wote. Malazi duni yanayosababishwa na msongamano wa mahabusu magerezani ni kero isiyo ngeni masikioni na midomoni mwa viongozi wa juu zaidi wa nchi hii. Kama gereza lililokusudiwa kuhifadhi mahabusu 800 linabeba mahabusu zaidi ya 2000, jiulize hali ikoje. Msongamano unatisha. Kwenye magereza mengi, godoro jembamba la futi tatu kwa sita linalaliwa na mahabusu zaidi ya wawili. Wanalalaje? Ndio maisha tuliowachagulia, na bado sio wahalifu. Msongamano utapungua kwa kuruhusu dhamana, kufuta kesi za hila, na kupeleleza na kusikiliza kesi kwa wakati. Haya yote yako ndani ya uwezo wa Serikali unayoiongoza.
Wito
Mheshimiwa Rais, kwa kuwa tulikubaliana kuwa jamii ya watu wastaarabu, tunalazimika kutumia mifumo rasmi kuendesha maisha yetu ya siku kwa siku. Ni kwa mantiki hii hii, utendaji usioridhisha wa mamlaka za Serikali unaathiri haki, wajibu na maslahi ya watu. Katika barua hii, angalau kwa kila hoja, nimebainisha nini kifanyike. Kwa kuwa unaweza kuona mbali, ninakusihi uitikie wito wangu kwa haraka ili kunusuru hali za mahabusu wa sasa na watarajiwa.
Katika kushughulikia tuhuma zozote za jinai, sheria zizingatiwe. Aidha, zipo sheria mbovu. Ninashauri zifanyiwe marekebisho kwa manufaa yetu sote kama taifa. Ondoa mamlaka mikononi mwa watu kwa kuwezesha taasisi zifanye kazi kwa ufanisi, zitathminiwe na kufuatiliwa. Utendaji kazi wa polisi, katika eneo hili hauridhishi. Polisi (DCI) wakikwama usitarajie ufanisi kwa Ofisi ya Mashitaka ya Umma (DPP). Dhibiti rushwa katika mnyororo wa haki jinai. Ondoa muingiliano wa kimamlaka unaojitokeza kati ya Mahakama na Serikali. Zuia maelekezo ya Serikali kwa Mahakama. Mahakama huru ni muarobaini wa mambo mengi.
Mungu ibariki Tanzania.