Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Machaguo ya safari kwenye ukurasa huu ni sampuli ya huduma za Uber na huenda baadhi yake zisipatikane mahali ambapo unatumia programu ya Uber. Ukiangalia ukurasa wa wavuti wa mji uliko au uangalie kwenye programu, utaona safari unazoweza kuomba.

X small

Teksi za eneo lako -> sasa ziko kwenye Uber

Safari rahisi kwenye teksi zilizo karibu.

search
Navigate right up
search
search
Navigate right up
search

Jinsi ya kusafiri kwa Taxi

1. Ombi

Fungua programu kisha uweke mahali unakoenda katika kisanduku cha “Unaenda wapi?”. Baada ya kuthibitisha kwamba eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda ni sahihi, chagua Teksi.

Baada ya kukutanishwa na dereva, utaona maelezo ya gari lake na unaweza kumfuatilia kwenye ramani anapokuja kukuchukua.

2. Safari

Hakikisha kwamba maelezo ya gari yanafanana na maelezo unayoona kwenye programu kabla ya kuingia kwenye gari.

Dereva wako anajua mahali unakoenda na ana maelekezo yatakayokufikisha kwa haraka, lakini unaweza kumwomba atumie barabara mahususi wakati wowote.

3. Shuka

Utatozwa kiotomatiki kupitia mbinu yako ya malipo iliyo kwenye faili, kwa hivyo unaweza kushuka kwenye gari pindi unapofika mahali unakoenda.

Kumbuka kumkadiria dereva wako ili kusaidia Uber iendelee kuimarisha usalama na kufanya kila mtu afurahie. Pia unaweza kufikiria kumpa dereva wako kiinua mgongo.

Sababu za kutumia Teksi

Chaguo

Pata safari inayokufaa kwa kubofya mara chache tu.

Urahisi

Omba teksi katika dakika chache—wakati wowote na popote.

Bei unayoonyeshwa mapema

Lipa bei ile ile uliyoona mapema mwishoni mwa safari.*

Weledi

Madereva wa teksi walio na leseni kamili wako tayari kukupeleka mahali unakoenda.

Usalama

Uber huupa usalama wako kipaumbele kila wakati.

Safari kote ulimwenguni

Kuna njia zaidi ya moja ya kusafiri ukitumia Uber, haijalishi mahali ulipo au unakokwenda baadaye. Angalia programu ili uone ni machaguo yapi ya safari yanayopatikana karibu nawe.*

1/9
1/5
1/3

*Bei ya mapema unayoonyeshwa huenda ikabadilika ukiongeza vituo vya kusimama, ukibadilisha mahali unakoenda, ukibadilisha barabara au muda wa safari kwa kiasi kikubwa au ukipitia kituo cha kutoza magari ambacho hakikujumuishwa kwenye bei ya mapema unayoonyeshwa. Isitoshe, unaweza kutozwa ada ya muda wa kusubiri kwa muda unaochukua kwenda kwenye gari katika eneo la kuchukuliwa au ada kwa ajili ya muda unaotumika katika kituo cha kusimama ukiwa safarini.

Taarifa inayopatikana kwenye tovuti hii ina madhumuni ya kutoa maelezo pekee na huenda isitumike katika nchi, kanda au jiji lako. Inaweza kubadilika na huenda tukaibadilisha bila kukuarifu.